Muhtasari wa Ujauzito wenye Hatari kubwa

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2023

Ujauzito wenye hatari ni nini?

Hakuna ufafanuzi mmoja rasmi wa ujauzito wenye hatari. Kwa ujumla, ujauzito wenye hatari unamaanisha:

  • Wewe au mtoto wako ana uwezekano mkubwa kuliko kawaida wa kugonjeka au kufa

  • Matatizo kabla au baada ya kujifungua yana uwezekano mkubwa kuliko kawaida wa kutokea

Hali fulani, zinazoitwa mambo hatarishi, hufanya ujauzito kuwa wa hatari kubwa. Matatizo yanaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua, au katika wiki zinazofuata baada ya kujifungua.

  • Madaktari hufuatilia ujauzito wenye hatari kwa makini sana

  • Ikiwa ujauzito wako unachukuliwa kuwa wenye hatari kubwa, unaweza kutumwa kwa daktari, kliniki au hospitali maalum

  • Kupata matibabu sahihi kunaweza kuokoa maisha yako na ya mtoto wako

Ni nini kinachoweza kufanya ujauzito wako kuwa hatarini zaidi?

Baadhi ya sababu za kawaida zinazofanya ujauzito wako kuwa hatarini ni pamoja na:

  • Umri (wasichana wa umri wa miaka 15 au chini na wanawake wenye umri wa miaka 35 au zaidi wako katika hatari kubwa)

  • Kuvuta sigara, kunywa, au kutumia dawa za kulevya

  • Kuwa na uzani mdogo sana au uzani mkubwa kupita kiasi

  • Kuwa na matatizo wakati wa ujauzito wowote uliopita, kama vile kuwa na kuharibika mimba au kuzaa mtoto mapema sana (premature) au mdogo sana

  • Kuwa na matatizo ya kiafya, hasa shinikizo la juu la damu, kisukari, matatizo ya moyo, na ugonjwa wa selimundu

  • Matatizo kutokea kwenye ujauzito wako, kama vile kondo lako la nyuma linapokua mahali pasipofaa au linapolegea mapema zaidi—kondo la nyuma ni ogani ya mviringo, iliyo bapa, ndani ya mfuko wa uzazi ambayo huunganisha mtoto na kiunga mwana.

  • Kupata maambukizi wakati wa ujauzito, ikijumuisha maambukizi ya figo, magonjwa ya zinaa, na mengine mengi

  • Kuwa na mimba ya watoto zaidi ya mmoja, kama vile mapacha au watatu

Nini husababisha vifo vya akina mama?

Viwango vya vifo kutokana na ujawazito vinatofautiana kote ulimwenguni. Nchini Marekani, wanawake vifo 24 hutokea kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa. Vifo vingi kati ya hivyo vingeweza kuzuiliwa kama mama angepata huduma ya matibabu mapema katika ujauzito. Sababu za mara kwa mara za vifo vya akina mama zinajumuisha:

  • Kutokwa na damu (kuvuja damu kutokana na uzazi)

  • Preeklampsia (aina fulani ya shinikizo la juu la damu ambalo hutokea wakati wa ujauzito)

  • Kuganda kwa damu kwenye mapafu

  • Maambukizi

  • Matatizo ya kiafya yaliyokuwepo kabla ya kuwa mjamzito

Ni nini husababisha vifo vya watoto wachanga?

Baadhi ya sababu za vifo vingi vya watoto kabla au mara tu baada ya kuzaliwa ni pamoja na:

  • Kuzaliwa mapema zaidi (zaidi ya wiki 3 kabla ya tarehe iliyotarajiwa)

  • Kasoro za kuzaliwa

  • Maambukizi

  • Matatizo ya kondo la nyuma (ogani iliyo ndani ya uterasi ambayo hubeba lishe na damu hadi kwenye kijusi)

  • Matatizo wakati wa kuzaliwa, kama vile mtoto kushindwa kupumua

  • Ugonjwa unaosababisa vifo vya ghafla vya watoto wachanga (SIDS, kifo cha mtoto mchanga mwenye afya njema anapokuwa kwenye usingizi)

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mimba yako iko katika hatari kubwa?

Madaktari huchunguza hatari ya ujauzito wako ikiwa:

Madaktari hushughulikia vipi mimba zilizo hatarini?

Madaktari watakutibu wewe na ujauzito wako kwa uangalifu sana. Huenda ukahitaji kwenda kwa daktari au kliniki maalum ambayo inatibu mimba zilizo katika hatari kubwa. Huenda ikakubidi kumwona daktari mara nyingi zaidi kuliko wanawake ambao hawako katika hatari kubwa. Unaweza hata kuhitaji kutembelewa na muuguzi nyumbani kwako.

Ikiwa una tatizo fulani la kiafya linalofanya ujauzito wako kuwa wa hatari zaidi, madaktari watalitibu tatizo hilo. Lazima uhakikishe unameza dawa zote ambazo daktari wako hukuagizia na kufuata lishe yoyote maalum unayopewa.