Mtoto Aliyezaliwa Kabla ya Wakati (Kabla ya wakati wake)

Imepitiwa/Imerekebishwa Nov 2023

Je, mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati ni nani?

Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati wake, pia anayeitwa mtoto wa kabla ya wakati wake, anazaliwa mapema sana. Ujauzito kamili huwa wa wiki 37 hadi 40, kwa hivyo mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati wake anazaliwa wakati wowote kabla ya wiki ya 37 ya ujauzito.

Watoto wa mapema ni, kwa uwezekano mkubwa watapata matatizo katika kuzaliwa na baadaye. Watoto waliozaliwa kabla ya wiki 23 wana uwezekano mkubwa wa kutoishi.

  • Kwa sababu watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao walikuwa na muda mfupi wa kukua kwenye mfuko wa uzazi, viungo vyao havijakua kamili

  • Watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao wana matatizo katika kupumua na kula na wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi

  • Watoto wengi waliozaliwa kabla ya wakati wao wana matatizo ya muda mrefu

  • Watoto waliozaliwa mapema sana wana nafasi kubwa zaidi ya kukumbwa na matatizo ya afya ya muda mrefu kama vile ugonjwa wa kupooza kwa ubongo, matatizo ya kusikia, au matatizo ya kujifunza

  • Watoto waliozaliwa mapema sana wanaweza kuhitaji kuwekwa kwenye kitamizi ili kumpea joto, kuwa kwenye kipumuaji ili kuwasaidia kupumua na kulishwa kupitia kwenye mfereji kwenye pua yao

  • Watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao hubaki hospitalini hadi waweze kula kwa njia ya kawaida, waongeze uzani na wasihitaji tena kuwa kwenye kitamizi

  • Kuona daktari wako mara kwa mara wakati wa ujauzito hupunguza nafasi yako ya kupata mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati wao

Ni nini husababisha mtoto kuzaliwa mapema sana?

Wakati mwingi, hakuna sababu dhahiri ya kwa nini mtoto anazaliwa mapema zaidi.

Nafasi za kupata mtoto kabla ya wakati wake ziko juu zaidi ikiwa mama:

  • Alikuwa amepata mtoto kabla ya wakati wake hapo awali

  • Amekuwa na kuharibika mimba au utoaji mimba kadhaa

  • Ana matatizo mengine ya afya, kama vile shinikizo la damu la juu wakati wa ujauzito au ugonjwa wa moyo au figo

  • Ana mambukizi ambayo hayajatibiwa (kama vile Maambukizi ya njia ya mkojo)

  • Anapata mapacha au watoto watatu

  • Alitumiwa kwenye utungisho wa vitro (IVF) ili kuwa mjamzito

  • Anavuta sigara

  • Hapati huduma nzuri za kabla ya kujifungua

Dalili za mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake ni zipi?

Watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao wanaonekana tofauti na watoto wa kipindi kamili. Kwa kawaida:

  • Ana uzito wa kati ya pauni 1 na 5.5 (gramu 500 hadi 2500)

  • Ana kichwa ambacho kinaonekana kuwa kikubwa ikilinganishwa na mwili mwingine

  • Hawana mafuta chini ya ngozi yao

  • Wana ngozi nyembamba, inayong'aa, yenye rangi ya waridi

  • Wana mishipa inayoonekana kupitia kwenye ngozi yao

Mara nyingi watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao:

  • Hupumua haraka na wanaweza kusita kwa sekunde kwa wakati (kukoma kupumua)

  • Wana tatizo katika kudhibiti halijoto ya mwili wao

  • Wana tatizo kunyonya na kumeza

Ni matatizo gani ambayo watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao wanayo?

Watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao hupata matatizo kwa sababu viungo vyao havijakua kikamilifu. Vile wamezaliwa mapema kabla ya wakati wao, ndivyo wanapata matatizo zaidi.

  • Matatizo ya ubongo: Upumuaji hafifu, tatizo katika kunyonya na kumeza, kuvuja damu kwenye ubongo

  • Matatizo ya Njia ya Mmeng'enyo wa Chakula: Kucheua sana, utumbo unaovuja damu, ngozi ya manjano (homa ya nyongo ya manjano)

  • Matatizo ya mfumo wa kingamwili: Maambukizi kwenye mtiririko wao wa damu (sepsisi) au kuzunguka ubongo wao (homa ya uti wa mgongo)

  • Maambukizi ya mapafu: Mapafu kuzibika kwa kiowevu (ugonjwa wa shida ya kupumua)

  • Matatizo ya jicho: Kuvuja damu na kupata alama kwenye retina (kuona sehemu ya macho), tatizo linaloitwa retinopathi ya kabla ya wakati

Matatizo mengi yanaisha baada ya muda. Lakini watoto ambao wana matatizo makali wanaweza kuendelea kupata matatizo kwa upumuaji au uoni wao.

Madaktari wanatibu aje watoto waliozaliwa kabla ya wakati wao?

Madaktari watatunza mtoto wako hospitalini kwenye kitengo maalum cha watoto wagonjwa waliozaliwa karibuni. Inaitwa NICU, ambayo inasimamia kitengo cha wagonjwa mahututi cha watoto wachanga. Pia:

  • Wataweka mtoto wako kwenye kitamizi ili kukusaidia kupea mtoto joto

  • Wataweka dawa kwenye mapafu ya mtoto wako ili kusaidia mtoto wako kupumua na wakati mwingine kuweka mfereji kwenye mapua au mdomo wa mtoto wako ulioambatishwa kwenye mashine ya kupumua (kipumuaji)

  • Watalisha mtoto wako kupitia mshipa au mfereji wa kulisha hadi mtoto wako anyonye na ameze

  • Wataweka mtoto kwenye mwanga wa ultraviolet (UV) ili kutibu homa ya nyongo ya manjano

Ninawezaje kuzuia mtoto wangu asizaliwe mapema sana?

Unaweza kupunguza uwezekano wa mtoto wako kuzaliwa mapema zaidi kwa:

  • Kuhudhuria ziara zako zote za daktari wa kabla ya kujifungua

  • Kufuata lishe yenye afya

  • Kutokunywa pombe

  • Kutotumia tumbaku au dawa

Ukipata uchungu wa uzazi mapema, daktari wako anaweza kukupatia dawa ya:

  • kupunguza uchungu wako wa uzazi

  • Kusaidia mapafu ya mtoto wako yakue haraka zaidi