Kisukari Wakati wa Ujauzito

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024

Kisukari ni ugonjwa ambao viwango vyako vya sukari kwenye damu (glukosi) kuwa juu sana. Sukari ya damu ni chanzo kikuu cha mwili wako cha kutoa nguvu. Mwili wako unavunja aina zote za vyakula, ikiwa ni pamoja na mkate, matunda, soda na tambi kuwa sukari ya damu.

Homoni insulini hudhibiti sukari yako ya damu. Ikiwa mwili wako hauna insulini ya kutosha au hauitikii ipasavyo kwa insulini, sukari yako ya damu itakuwa juu sana. Sukari ya juu ya damu inaeza kusababisha matatizo mengi kwako wewe pamoja na mtoto wako.

Takriban 4% ya wanawake wajawazito hupata kisukari wakati wa ujauzito. Kupata kisukari wakati wa ujauzito kunaitwa kisukari cha ujauzito.

  • Ikiwa tayari una ugonjwa wa kisukari, ujauzito wako utakuwa katika hali mbaya zaidi wakati wa ujauzito

  • Unaweza pia kuwa na kisukari kwa mara ya kwanza wakati ni mjamzito, kisukari hiki mara nyingi kinaondoka baada ya kuzaa mtoto

  • Kuwa na kisukari wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha matatizo makubwa kwako na kwa mtoto wako

  • Madaktari wanawapima wanawake wajawazito wote ili kuona kama wana kisukari wakati wa ujauzito

  • Madaktari watakufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kwamba kiwango cha sukari yako ya damu inabaki kuwa karibu na hali ya kawaida

Nini kinachosababisha kisukari wakati wa ujauzito?

Una uwezekano mkubwa wa kupata kisukari cha ujauzito ikiwa:

  • Umekuwa nao hapo awali

  • Una unene kupita kiasi

  • Una wanafamilia wa karibu wenye kisukari

  • Wewe ni wa jamii fulani, hasa Mmarekani Asilia, Wa Asia ya Kusini au Mashariki, Mzaliwa wa Visiwa vya Pasifiki, au Mhispania/Latino.

Ni matatizo gani yanaweza kuletwa na kisukari wakati wa ujauzito?

Ikiwa hakitatibiwa, kisukari wakati wa ujauzito kinaweza kuleta uwezekano wa:

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kisukari wakati wa ujauzito?

Madaktari wanawapima wanawake wote wajawazito kuona ikiwa wana kisukari kwa kutumia kipimo cha damu. Madaktari wengi wanapendekeza kipimo cha kuonyesha kustahimili glukosi. Katika kipimo hiki:

  • Unakunywa kinywaji chenye sukari ambacho kina glukosi nyingi sana

  • Saa moja baadaye, madaktari watachukua sampuli ya damu na kupima kiwango cha sukari kwenye damu

  • Ikiwa sukari kwenye damu ipo juu sana, una kisukari cha ujauzito

  • Ikiwa sukari kwenye damu iko juu tu kidogo, madaktari wanarudia kipimo kwa kutumia glukosi nyingi zaidi kwenye kinywaji na kupima sukari kwenye damu yako baada ya saa 3

Wakati mwingine, madaktari wanapima tu sukari kwenye damu yako bila kukupa kinywaji chenye sukari. Hatua hii ni ya haraka na rahisi lakini si sahihi

Je, madaktari wanatibu vipi kisukari wakati wa ujauzito?

Kabla ya ujauzito

Ikiwa una kisukari na unapanga kupata ujauzito, madaktari watakuelekeza udhibiti kiwango cha sukari kwenye damu yako kwa:

  • Kufuata mpango wa mlo (kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi, usiongezeke uzani)

  • Kufanya mazoezi mara kwa mara

  • Kutumia insulini

Ukiwa mjamzito

Daktari wako anaweza kufanya kazi kama sehemu ya timu ya huduma ya afya akiwa na wauguzi na wataalamu wa lishe ili kupunguza uwezekano wa kupata matatizo. Atafanya yafuatayo:

  • Watajaribu kufanya kiwango cha sukari yako ya damu inabaki kuwa karibu na hali ya kawaida

  • Watakuambia upime kiwango cha sukari kwenye damu yako ukiwa nyumbani mara kadhaa kwa siku kwa kutumia kipimo cha sukari kwenye damu

  • Kukupa insulini au dawa nyingine ya kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu

  • Kumwangalia mtoto wako kwa kuhesabu kipimo cha mapigo ya moyo ya mtoto wako na kufanya kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti

Wakati wa uchungu wa uzazi na kujifungua

  • Ikwia hupati uchungu wa uzazi kufikia wiki ya 39, madaktari wanaweza kuanzisha uchungu wa uzazi kwa kutumia dawa

  • Madaktari wanaweza kukupatia insulini kupitia mshipa wakati wa leba

Baada ya ujauzito

  • Timu yako ya huduma ya afya itamwagalia mtoto wako kwa karibu na kufanya vipimo vya damu mara kwa mara

  • Ikiwa ulikuwa na kisukari kabla ya ujauzito, kwa kawaida utaweza kurejea kwa kiasi cha insulini au dawa uliyokuwa ukinywa ndani ya wiki moja baada ya kupata mtoto wako.

  • Kisukari cha ujauzito kwa kawaida kinaondoka baada ya kuzaa mtoto wako, lakini unaweza kukipata tena ukiwa na ujauzito mwingine na una uwezekano mkubwa wa kupata kisukari cha kudumu umri unapokuwa mkubwa