Mzunguko wa Hedhi

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2024

Je, mzunguko wa hedhi ni nini?

Mzunguko wa hedhi ni mchakato ambao mfumo wa uzazi wa mwanamke hupitia kila mwezi ili kuachia yai kutoka kwenye ovari na kuweka uwezekano wa yeye kupata mimba.

Mzunguko wa hedhi (kuingia mwezini) ni kuvuja damu kila mwezi kutoka kwenye uke ambapo hutokea mwanzoni mwa kila mzunguko wa hedhi. Wakati wa hedhi, utando wa uterasi hutoka na kuachiwa kama damu ya hedhi.

Katika mzunguko wa hedhi wa kila mwezi:

  • Yai hukomaa na kutolewa (mchakato unaoitwa udondoshaji)

  • Utando wa uterasi huvimba pamoja na mishipa ya damu hivyo kuwa tayari kupokea yai ambalo limerutubishwa na shahawa za mwanaume

  • Yai lililotungishwa hujipachika kwenye utando wa uterasi na kuanza kukua AU

  • Yai lisipotungishwa, halijipachiki, nao utando wa uterasi hubambuka na kutolewa kama damu ya hedhi.

Siku za mzunguko wa hedhi huhesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya mzunguko mmoja wa hedhi. Kwa kawaida mzunguko wa hedhi hudumu kati ya siku 25 na 35 lakini zinaweza kubadilika kati ya mwezi na mwezi. Kwa kawaida, kipindi cha hedhi hudumu kwa siku 3 hadi 7.

  • Wasichana huanza kupata mzunguko wa hedhi wakati wa kubalehe, wakiwa na kiasi cha miaka 13, na hukoma kupata hedhi katika wakati wa ukomo wa hedhi, kiasi cha umri wa miaka 52

  • Ovari huachia yai (kutaga yai) takribani siku 14 kabla ya kuanza kwa mzunguko wa hedhi

  • Mwanamke ana uwezekano mkubwa wa kupata mimba ikiwa atafanya mapenzi bila kinga wakati wa siku 3 kabla ya kutaga yai (takribani siku 17 kabla ya kuanza kwa mzunguko wa hedhi)

Je, ni matatizo gani yanayoweza kutokea kwa mzunguko wa hedhi?

Kwa kawaida matatizo makubwa ya mzunguko wa hedhi ni pamoja na:

Sababu za kawaida zaidi za kukoma kwa mzunguko wa hedhi ni: