Kubalehe kwa Wasichana

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2024

Je, kubalehe ni nini?

Balehe ni kipindi cha ukuaji na maendeleo ambapo watoto na vijana hupata sifa za kimwili za watu wazima, kama vile matiti au kuota nywele sehemu za siri, na kuwa na uwezo wa kuzaa (kupata watoto). Kwa wasichana, kubalehe/kupevuka mara nyingi huanza kipindi cha miaka 8½ hadi 10 na kuendelea kwa kiasi cha miaka 4.

Wakati wa kuanza kwa balehe/kupevuka kwa wasichana hutegemea mambo yafuatayo:

  • Uzani: Wasichana wenye uzani mkuwa kupita kiasi mara nyingi huanza kubalehe mapema

  • Lishe: Wasichana ambao hawana au hawawezi kunyonya lishe sahihi huchelewa kuanza balehe

  • Jenetiki: Wasichana waliozaliwa na akina mama ambao walibalehe mapema nao wana uwezekano mkubwa wa kuanza kubalehe mapema

Je, nini husababisha kubalehe?

Mfumo wote wa uzazi, ikijumuisha kubalehe, hudhibitiwa na homoni. Homoni ni visafirishaji vya kemikali ambavyo hutengenezwa katika sehemu fulani za mwili na husafiri kupitia damu kuelekeza sehemu nyingine za mwili kuhusu cha kufanya.

Kubalehe kwa wasichana huanza pale homoni zinazotolewa na ubongo zinaposababisha ovari kukua. Kisha ovari huachia homoni ya estrojeni. Estrojeni husababisha kukua kwa mfumo wa uzazi wa msichana, pamoja na:

  • Matiti

  • Uke

  • Ovari (jozi za ogani ambapo mayai hutengenezwa na kuhifadhiwa)

  • Uterasi (ogani ambapo kijusi hukua kabla ya kuzaliwa)

Vipindi vya hedhi kwa kawaida huanza miaka michache baada ya balehe kuanza.

Je, ni mabadiliko gani hutokea wakati wa kubalehe?

Mabadiliko ya kimwili yafuatayo hutokea, mara nyingi kwa mpangilio huu:

  • Kwanza, matiti hukua—mara nyingi hili hutokea katika umri wa miaka 8 hadi 13

  • Muda mfupi baadaye, nywele huanza kuota kwenye makwapa na sehemu za siri

  • Kasi ya kuongeza urefu hutokea—mara nyingi ukuaji hupungua pale hedhi zinapoanza

  • Hedhi (kuingia mwezini) huanza takribani miaka 2 hadi 3 baada ya kuanza kwa ukuaji wa matiti

  • Mara nyingi wasichana huacha kuongezeka kimo wakiwa na umri wa kati ya miaka 14 na 16

Mara nyingi hedhi ya kwanza huanza takribani umri wa miaka 13 japokuwa inaweza kutokea wakati wowote kati ya umri wa miaka 10 na 16. Kwa mara ya kwanza, hedhi inaweza isitokee kila mara. Inaweza kuchukua hadi miaka 5 kwa mzunguko wa hedhi kutokea kila wakati. Jinsi wasichana wanavyokua, umbo la miili yao hubadilika. Nyonga na mapaja yao huongezeka, na wanapata mafuta zaidi mwilini. Hii ni hatua ya kawaida katika kubalehe kwa wasichana.

Hatua Muhimu katika Maendeleo ya Kijinsia

Wakati wa kubaleghe, ukuaji wa kijinsia hutokea kwa utaratibu fulani. Hata hivyo, mabadiliko hutokea na kuendelea kwa wakati tofauti kwa kila mtu. Kwa wasichana, kubalehe/kupevuka mara nyingi huanza katika umri wa miaka 8 1/2 hadi 10 na kudumu kwa takribani miaka 4. Chati hii inaonyesha utaratibu wa kawaida na kipindi cha kawaida cha ukuaji wa kijinsia.

Je, matatizo yepi yanaweza kutokea wakati wa kubalehe?

Matatizo ya kubalehe kawaida huhusisha homoni. Kuna matatizo mengi ya homoni ambayo husababisha homoni chache sana hivyo:

Mara chache, kuna homoni nyingi na msichana ana: