Kuchelewa Kubalehe

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023

Je, kuchelewa kubalehe ni nini?

Ubaleghe ni sehemu ya mwisho ya utoto ambapo wavulana na wasichana wanakomaa viungo vya uzazi. Wanaanza kuonekana zaidi kama watu wazima na kuwa na uwezo wa kupata watoto. Wavulana hupata nywele usoni na mwilini, sauti nzito, na korodani kubwa. Wasichana hukua matiti na nywele za sehemu za siri. Kubaleghe kwa kawaida huanza kati ya umri wa miaka 8 hadi 13 kwa wasichana na miaka 10 hadi 14 kwa wavulana.

Kuchelewa kubaleghe ni wakati kubalehe huanza baadaye kuliko inavyotarajiwa. Kubalehe huchelewa inapoanza baada ya umri wa miaka 13 kwa wasichana na baada ya miaka 14 kwa wavulana.

  • Kuchelewa kubaleghe kunaweza kuwa jambo la kawaida ikiwa watu wengi katika familia yako walichelewa kubalehe pia

  • Wakati fulani kuchelewa kubalehe husababishwa na matatizo ya kiafya au kwa sababu mtoto alipata matibabu ya mionzi au tibakemikali (kwa mfano, matibabu ya saratani)

  • Ishara ya kuchelewa kubalehe kwa wavulana ni kutokuwa na kuongezeka kwa ukubwa wa korodani kufikia umri wa miaka 14

  • Dalili za kuchelewa kubalehe kwa wasichana ni pamoja na kutokua kwa matiti kufikia umri wa miaka 13 au kutopata hedhi ifikapo miaka 16

  • Matibabu hutegemea kile kinachosababisha kuchelewa kubalehe—madaktari wanaweza kuagiza mtoto wako atumie homoni

Hatua katika Ukuaji wa Viungo vya Uzazi kwa Wasichana na Wavulana

Wakati wa kubaleghe, ukuaji wa kijinsia hutokea kwa utaratibu fulani. Hata hivyo, mabadiliko hutokea na kuendelea kwa wakati tofauti kwa kila mtu.

Kwa wasichana, kubaleghe huanza karibu na umri wa miaka 8 hadi 13 na hudumu kama miaka 4.

Kwa wavulana, kubaleghe huanza karibu na umri wa miaka 9 hadi 14 na hudumu kama miaka 4 hadi 6.

Chati hii inaonyesha utaratibu wa kawaida na kipindi cha kawaida cha ukuaji wa kijinsia.

Je, nini huchelewesha kubalehe?

Kuchelewa kubalehe kunaweza kuwa tofauti ya kawaida ambayo iko katika familia. Mara nyingi, watoto wenye afya nzuri waliochelewa kubalehe watakuwa na kasi ya ukuaji kwa kuchelewa na hatimaye kuwafikia watoto wengine wa umri wao.

Wakati mwingine kuchelewa kubalehe husababishwa na tatizo jingine la kiafya kama vile:

Wasichana wanaokula chakula kidogo na kufanya mazoezi kupita kiasi mara nyingi huchelewa kubaleghe.

Je, dalili za kuchelewa kubalehe ni zipi?

Kuchelewa kubalehe ni kawaida zaidi kwa wavulana. Wavulana waliochelewa kubalehe kwa kawaida:

  • Huwa bado korodani hazijakua kubwa wafikapo umri wa miaka 14

  • Ni wafupi

Wasichana waliochelewa kubalehe huwa:

  • Hawajamea matiti kufikia umri wa miaka 13

  • Hawajaanza kupata hedhi kufikia umri wa miaka 16

Watoto wanaweza kudhihakiwa au kuonewa ikiwa wamechelewa kubalehe.

Je, mtoto wangu anapaswa kumwona daktari lini kwa kuchelewa kubalehe?

  • Wavulana ambao hawana dalili za kubaleghe wanapaswa kumuona daktari kufikia umri wa miaka 14

  • Wasichana ambao hawana dalili za kubaleghe wanapaswa kumuona daktari kufikia umri wa miaka 12 hadi 13—wasichana ambao hawajapata hedhi kufikia umri wa miaka 16 wanapaswa pia kuona daktari

Daktari wa mtoto wako anaweza kutaka kumwona mtoto wako kila baada ya miezi 6 ili kuona ameanza kubaleghe.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu amechelewa kubalehe?

Madaktari hutambua ugonjwa wa kuchelewa kubalehe kulingana na ukuaji wa viungo vya uzazi vya mtoto wako.

Ili kutathmini sababu ya kuchelewa kubalehe, madaktari huuliza kuhusu tabia za kula za mtoto wako. Pia watafanya vipimo:

  • Eksirei ya mifupa ya mtoto wako

  • Vipimo vya damu

  • Vipimo vya viwango vya homoni

  • Wakati mwingine, kupima jeni

  • Wakati mwingine, MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ili kuhakikisha kuwa hakuna tatizo la ubongo au tezi ya pituitari

Je, madaktari hutibu vipi hali ya kuchelewa kubalehe?

Madaktari watatibu matatizo yoyote ya kiafya ambayo yanazuia kubaleghe kuanza.

Watoto ambao kawaida huchelewa kukua kwa kawaida hawahitaji matibabu yoyote. Ikiwa kuchelewa kubalehe kunasababisha msongo mwingi wa mawazo au kuendelea kwa muda mrefu, madaktari wanaweza kuagiza matumizi ya homoni za ngono. Homoni za ngono zitaanzisha kubaleghe na kumsaidia mtoto wako kukua kimwili na kingono.

Matatizo ya jeni hayawezi kutibiwa, lakini kutumia homoni za ngono kunaweza kusaidia ukuaji wa mwili.