Ugonjwa wa Selulitisi

Imepitiwa/Imerekebishwa Nov 2023

Selulitisi ni nini?

Selulitisi ni maambukizi ya bakteria kwenye ngozi yako.

  • Selulitisi ni maambukizi ya ngozi yaliyoenea sana ambayo yanaweza kusambaa haraka na kuwa mabaya sana

  • Sehemu iliyoambukizwa inauma na ni nyekundu, ya moto na imevimba

  • Selulitisi inakaa sana kwenye miguu yako lakini inaweza kutokea sehemu yoyote

  • Ikiwa maambukizi yanafi kwenye mtiririko wa damu wa damu yako, yanaweza kuhatarisha maisha

Nini kinasababisha selulitisi?

Selulitisi inasababishwa na vijidudu (bakteria) wanaoingia kwenye ngozi yako. Bakteria wana uwezekano wa kuingia kupitia mipasuko midogo kwenye ngozi yako kupitia kwenye mikwaruzo, vitobo vya kudungwa sindano, majeraha ya kuungua, maambukizi ya kuvu, alama za kuumwa na mnyama na matatizo ya ngozi. Hata hivyo, selulitisi inaweza pia kutokea kwenye ngozi ambayo haina majeraha dhahiri.

Selulitisi mara nyingi unasababishwa na bakteria aina ya Stafailokokasi (maambukizi ya staph). Aina moja ya Stafailokokasi inayoweza kusababisha selulitisi inajulikana kama MRSA (Stafailokokasi Aureus isiyotibika kwa Methicillin). MRSA haitibiki kwa dawa nyingi za kuua bakteria na inaweza kuwa vigumu kuitibu.

Watu wenye mfumo wa kingamaradhi ambao ni dhaifu wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi yanayosababisha selulitisi.

Watu wana hatari kubwa ya kupata selulitisi kwa kujirudia ikiwa wana:

Zipi ni dalili za selulitisi?

  • Wekundu kwenye ngozi, kuvimba, joto na maumivu

  • Wakati mwingine malengelenge yenye kiowevu cha manjano

  • Wakati mwingine homa na vinundu vya limfu vilivyovimba (matezi yaliyovimba)

Selulitisi kwa kawaida huanza kama baka dogo jekundu ambalo linaonekana kidogo kama kidonda. Sehemu iliyoathiriwa inaweza kuwa kubwa haraka. Kwa siku chache, inaweza kubadilika kutoka kuwa doa na kusambaa kwenye sehemu yote ya chini ya mguu wako.

Ikiwa maambukizi yataingia kwenye mtiririko wa damu, unaweza kuwa na homa kali, shinikizo la chini la damu na baadhi ya ogani zako kuacha kufanya kazi (sepsisi).

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina selulitisi?

Madaktari hutambua ugonjwa wa selulitisi kulingana na mwonekano wa ngozi yako. Hakuna vipimo vya kuthibitisha kwa usahihi kabisa. Hata hivyo, madaktari wanaweza kufanya vipimo kama vile kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti ili kuhakikisha wekundu na uvimbe kwenye miguu yako si kwa sababu ya kuganda kwa damu.

Mwone daktari haraka ikiwa eneo la ngozi yako ni jekundu, limevimba na lina maumivu.

Je, madaktari wanatibu vipi selulitisi?

  • Dawa za kuua bakteria ili kuwaondoa bakteria

  • Kwa kawaida unatumia dawa za kumeza za kuua bakteria lakini wakati mwingine, panapokuwa na maambukizi makali, kwa njia ya mshipa (IV) hospitalini

  • Ikiwa una selulitisi kwenye mguu wako, madaktari watakuomba uunyanyue

Ninawezaje kuzuia selulitisi?

  • Safisha vidonda vya ngozi, vifunike kwa bandeji na upake dawa ya kuua bakteria kwa ajili ya ulinzi.

  • Tibu maambukizi ya kuvu za mguuni (kama vile kanyagio la mwanariadha) na matatizo mengine ya ngozi ili kusaidia mipasuko yoyote kwenye ngozi ipone.

  • Ikiwa una kisukari au mzunguko duni, chunguza miguu yako kila siku, tumia kilainisha ngozi na uepuke majeraha kwa kuvaa viatu vizuri