Ugonjwa wa Folikulaitisi
Folikulaitisi ni nini?
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Folikulaitisi ni mwako au maambukizi kwenye vishina vya nywele (mahali ambapo nywele zinaota kutoka kwenye ngozi yako). Inapokuwa kwa sababu ya maambukizi, ni aina ya usaha wa ngozi mdogo sana.
Folikulaitisi kwa kawaida unasababishwa na maambukizi ya bakteria
"Beseni la majimoto la folikulaitisi" ni aina ya folikulaitisi ambayo inasababishwa na bakteria fulani ambao wanaweza kukua kwenye beseni la majimoto au kizingia cha maji
Folikulaitisi inaonekana kama chunisi ndogo ya rangi nyeupe au nyekundu kwenye kitako cha nywele
Mashina ya nywele yaliyoambukizwa yanawasha na yanauma kidogo
Losheni yenye dawa za kuua bakteria au jeli kwa kawaida inatibu folikulaitisi
Nini husababisha folikulaitisi?
Aina nyingi za folikulaitisi zinasababishwa na bakteria, kwa kawaida bakteria aina ya Stafailokokasi (maambukizi ya staph). Aina nyingine za bakteria na kuvu zinaweza kusababisha folikulaitisi.
Kwa kawaida unapata folikulaitisi pale ambapo ngozi yako ina unyevu au imekwangulika kwa sababu ya kukuna, kama vile ngozi ambayo ipo chini ya vifaa vya michezo au kwenya matako yako. Una uwezekano mkubwa wa kupata folikulaitisi ikiwa wewe ni mtu mzima au una:
Majeraha kwenye ngozi yako
Unene kupita kiasi
Kisukari
Mfumo dhaifu wa kingamaradhi
Wakati mwingine, nywele ngumu zinaweza kuingia tena kwenye ngozi (nywele zilizooteana) baada ya kunyoa na kusababisha folikulaitisi isiyo na maambukizi
Dalili za folikulaitisi ni zipi?
Chunisi ndogo ya rangi nyeupe au nyekundu kwenye shina la nywele
Chunusi zinaweza kuwa zinawasha au zinauma kidogo
Unaweza kuwa na moja au mashina mengi ya nywele yaliyoambukizwa
Mashina ya nywele yaliyoambukizwa yanakuwa makubwa na kina kirefu zaidi, yanaweza kuwa usaha wa ngozi (majipu)
Madaktari hutibuje folikulaitisi?
Huenda madaktari wakakufanya:
Oga kwa kutumia sabuni ya kuua bakteria
Lowanisha kitambaa cha kuogea kwa maji ya vuguvugu yenye chumvi kitumie kwenye folikulaitisi mara kadhaa kwa siku
Weka krimu ya dawa za kuua bakteria kwenye ngozi yako
Tumia dawa za kuua bakteria kwa kinywa, ikiwa una sehemu kubwa ya mashina ya nywele yaliyoambukizwa
Ikiwa kila mara unapata nywele zinazooteana, madaktari wanaweza:
Kukuambia uache kunyoa kwa muda
Kukuambia utumie dawa za kuua bakteria, ikiwa mashina ya nywele yameambukizwa
Folikulaitisi wa kwenye beseni la maji moto wataondoka wenyewe. Kagua na urekebishe kiwango cha klorini cha beseni la maji moto ili kuzuia watu wengine wasipate folikulaitisi.
Usaha wa kwenye ngozi
Usaha wa kwenye ngozi ni nini?
Usaha wa kwenye ngozi ni vifuko vya usaha kwenye ngozi yako. Usaha ni majimaji mazito ambayo mwili wako huyatengeneza unapopambana na maambukizi. Unaweza pia kuwa na usaha ndani ya mwili wako.
Usaha wa kwenye ngozi unasababishwa na maambukizi ya bakteria, kwa kawaida kwa sababu ya bakteria aina ya Stafailokokasi (maambukizi ya staph)
Wakati mwingine unapata bakteria kwa sababu ya mpasuko kwenye ngozi au shina la nywele (sehemu ambapo nywele inaotea)
Usaha ni vidonda vinavyouma sana vilivyojaa usaha
Daktari atapasua jipu ili kuondoa usaha na wakati mwingine pia atakupa dawa za kuua bakteria
Aina mahususi za usaha wa kwenye ngozi ni:
Visiba (majipu): usaha wa kwenye ngozi ambao unajitengeneza kuzunguka mashina ya nywele
Vijipu vikubwa: zaidi ya kisiba kimoja vikiwa vimeunganika pamoja kwenye ngozi
Bakteria anaweza kuenea kutoka kwenye usaha wa kwenye ngozi na kuambukiza tishu nyingine na ogani kwenye mwili wako.
Ikiwa maambukizi yataingia kwenye mtiririko wa damu, unaweza kuwa na homa kali, shinikizo la chini la damu na ogani zako kushindwa kufanya kazi (sepsisi).
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Unaweza kupata usaha wa kwenye ngozi tena na tena kwa sababu zisizojulikana.
Nini husababisha usaha wa kwenye ngozi?
Usaha wa kwenye ngozi unasababishwa na maambukizi ya bakteria, kwa kawaida kwa sababu ya bakteria aina ya Stafailokokasi (maambukizi ya staph). Aina moja ya Stafailokokasi inayoweza kusababisha selulitisi inajulikana kama MRSA (Stafailokokasi Aureus isiyotibika kwa Methicillin). MRSA haitibiki kwa dawa nyingi za kuua bakteria na inaweza kuwa vigumu kuitibu.
Una uwezekano mkubwa wa kupata usaha wa kwenye ngozi ikiwa wewe ni mtu mzima mwenye umri mkubwa au una:
Majeraha kwenye ngozi yako
Unene kupita kiasi
Kisukari
Mfumo dhaifu wa kingamaradhi
Dalili za usaha wa kwenye ngozi ni nini?
Usaha wa kwenye ngozi unaweza kuwa popote kwenye mwili wako.
Ni uvimbe mwekundu unaoumiza sana ni laini sana kuushika
Visiba ni vyekundu, vinang'aa na kwa kawaida havizidi urefu wa inchi moja (sentimita 2.5) kwa upana.
Usaha wa kwenye ngozi ambao si visiba unaweza kukuwa kufikia hadi inchi 2 au 3 (sentimita 5 hadi 7)
Ikiwa hautatibiwa, usaha wa kwenye ngozi unaongezeka kuwa mkubwa, unapasuka na kutoa usaha.
Unaweza kuwa na homa na kuhisi kuumwa
Madaktari wanatibu vipi usaha wa kwenye ngozi?
Ikiwa usaha wa kwenye ngozi ni mdogo, madaktari watakuambia uweke juu yake joto kidogo, kama vile nguo ya moto au chupa ya maji moto. Ikiwa hiyo haitafanya kazi, madaktari:
Watapasua uvimbe na kutoa usaha
Watasafisha kifuko cha usaha kwa mchanganyiko wa chumvi
Madaktari wanaweza pia kuweka shashi kwenye kifuko kwa siku 1 hadi 2 ili kuacha paendelee kuwa wazi ili usaha uendelee kutoka.
Hali nyingi za usaha wa kwenye ngozi hazihitaji kutumia dawa za kuua bakteria. Hata hivyo, madaktari wanaweza kukupa dawa za kuua bakteria ikiwa:
Una uvimbe mwingi wenye usaha
Maambukizi yameenea kwenye ngozi ya karibu (selulitisi)
Una mfumo wa kingamaradhi ulio dhaifu
Ikiwa utapata tena usaha wa kwenye ngozi, madaktari:
Watakwambia usafishe ngozi yako kwa kutumia sabuni ya maji ya dawa za kuua viini
Atakupa dawa za kuua bakteria kwa mwezi 1 hadi 2