Tinea ya mguu ni nini?
Tinea ya mguu ni maambukizi ya kuvu ambayo husababisha upele kwenye maeneo yenye unyevunyevu katika mguu wako
Tinea ya mguu hutokea kila mara kwa sababu maji hunasa kwenye nafasi zenye hali ya uvuguvugu katikati ya vidole vya miguu yako
Inaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine katika mabafu, mabafu ya manyunyu, na sehemu zilizolowa zenye hali ya uvuguvugu zinazotumiwa na watu wengi
Kuweka miguu yako katika hali ya ukavu hupunguza uwezekano wa kupata tinea ya mguu
Madaktari hutibu tinea ya mguu kwa kutumia malai ya dawa ya kuvu
Zipi ni dalili za tinea ya mguu?
Dalili zinajumuisha:
Kuwasha
Ukurutu kwenye mguu
Kuna aina mbalimbali za ukurutu wa tinea ya mguu:
Ngozi iliyopasuka inayobanduka katikati ya vidole vya miguu yako
Ngozi nene yenye magamba kwenye nyayo za miguu yako
Malengelenge yaliyojaa majimaji, ambayo si ya kawaida
Mipasuko katika ngozi yako inaweza kuruhusu vijidudu kuingia na kusababisha maambukizi ya bakteria kwenye ngozi ya mguu wako (seluliti).
Ngozi iliyo katikati ya vidole vya miguu imepasukapasuka, ina magamba, na mara nyingi ina rangi nyekundu. Ugunduzi huu unafanana hasa na kanyagio la mwanariadha (tinea ya mguu) Wakati mwingine hali isiyo ya kawaida huonekana zaidi katikati ya vidole vya miguu, kama ilivyo kwenye picha iliyo upande wa kulia.
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Image provided by Thomas Habif, MD.
This photo shows cracked, scaly skin on the sole of the foot.
© Springer Science+Business Media
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina tinea ya mguu?
Mara nyingi madaktari wanaweza kufahamu kuwa ni tinea ya mguu kwa kuitazama tu. Ili kufahamu kwa hakika, madaktari wanaweza kukwangua kipande kidogo sana cha ngozi kwa ajili ya kukichunguza kwenye hadubini.
Je, madaktari wanatibu vipi tinea ya mguu?
Madaktari hutibu tinea ya mguu kwa kutumia:
Malai ya dawa ya kuvu ya kupaka kwenye mguu wako
Mara chache, kwa dawa za kuua bakteria za kumeza
Tinea ya mguu mara nyingi hurejea baada ya matibabu. Unaweza kuhitaji kutumia dawa kwa muda mrefu.
Ninawezaje kuzuia tinea ya mguu?
Ili kuzuia tinea ya mguu:
Hakikisha miguu yako ni mikavu wakati wote
Vaa viatu vya kuogea au ndara ukiwa kwenye mabafu ya ukumbi wa michezo ya mazoezi ya viungo au mabafu mengine ya umma
Njia za kuweka miguu yako katika hali ya ukavu:
Kwa kuvaa viatu vinavyoacha vidole vya miguu wazi au viatu vinavyoruhusu mzunguko wa hewa
Kwa kubadilisha soksi zako kila mara, hasa wakati ambapo hali ya hewa inakuwa yenye uvuguvugu
Kwa kukausha nafasi zilizo katikati ya vidole vyako vya miguu ukitumia taulo mara baada ya kumaliza kuoga
Kwa kupaka poda za dawa ya kuvu (kama vile miconazole), jivii, au myeyusho wa kloridi ya alumini au kuloweka miguu yako kwenye myeyusho wa Burow