Choa ni maambukizi ya kawaida ya kuvu kwenye ngozi au kucha. Choa haina uhusiano wowote na minyoo. Lakini upele unaweza kuwa na umbo la pete. Kwa hiyo, maambukizi kwa sasa yanajulikana kama choa. Madaktari huita maambukizi haya "tinea."
Choa wa mwili ni nini?
Choa wa mwili ni maambukizi ya kuvu ambao huunda upele wenye umbo la pete kwenye uso, mikono, miguu, kifua au tumbo lako.
Choa wa mwili wanaweza kusambaa kwenye maeneo mengine ya mwili wako au kwa watu wengine ikiwa ngozi yako itagusana na ngozi zao
Madaktari huitibu kwa kutumia malai ya dawa ya kuvu au mara chache kwa kutumia vidonge
Zipi ni dalili za choa wa mwili?
© Springer Science+Business Media
© Springer Science+Business Media
Dalili zinajumuisha:
Madoa ya mviringo yenye rangi ya waridi au nyekundu kwenye ngozi yako yenye kingo za magamba, zilizoinuliwa
Mara nyingine, mwasho
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina choa wa mwili?
Mara nyingi madaktari wanaweza kufahamu kuwa ni choa wa mwili kwa kuitazama tu. Ili kufahamu kwa hakika, madaktari wanaweza kukwangua kipande kidogo cha ngozi yako ili kukichunguza kwenye hadubini.
Je, madaktari wanatibu vipi choa wa mwili?
Madaktari hutibu choa wa mwili kwa kutumia:
Malai ya dawa ya kuvu au losheni
Wakati mwingine, dawa za kumeza
Ikiwa utasitisha matumiza ya dawa mapema sana, maambukizi yanaweza kurejea.