Choa ni maambukizi ya kawaida ya kuvu kwenye ngozi au kucha. Choa haina uhusiano wowote na minyoo. Lakini upele unaweza kuwa na umbo la pete. Kwa hiyo, maambukizi kwa sasa yanajulikana kama choa. Madaktari huita maambukizi haya "tinea."
Choa wa ngozi ya kichwa ni nini?
Choa wa ngozi ya kichwa ni maambukizi ya kuvu ambayo husababisha upele wenye magamba au kidoa cha kunyonyoka kwa nywele kwenye ngozi ya kichwa.
Choa wa ngozi ya kichwa huwapata sana watoto
Husambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine
Inaweza kusababisha upele wa ngozi ya kichwa, mabaka ya upara, na mara chache uvimbe unaouma wenye kutoa usaha
Matibabu hujumuisha dawa ya kuvu ya kumeza na ile inayotumika kwenye malai ya ngozi ya kichwa na shampuu maalumu
Inaweza kuchukua muda mrefu kuondoa choa wa ngozi ya kichwa
Zipi ni dalili za choa wa ngozi ya kichwa?
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Dalili zinajumuisha:
Upele mkavu na wenye gamba kichwani kwako ambao unaweza kuwasha
Kiunga cha upotevu wa nywele (alopesha)
Wakati mwingine, ngozi ya kichwa chako kubanduka na kutoa vitu kama mba
Wakati mwingine, doa lililovimba lenye uchungu kwenye ngozi ya kichwa ambalo linaweza kugeuka na kuwa lengelenge au kutoa usaha (kerioni)
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina choa wa ngozi ya kichwa?
Mara nyingi madaktari wanaweza kufahamu kuwa ni choa wa ngozi ya kichwa kwa kutazama tu. Wakati mwignine, wanaweza kunyofoa nywele kutoka kwenye kichwa chako na kukwangua kipande kidogo cha ngozi yako ili kuchunguza kwenye hadubini. Wanaweza kuangalia ngozi ya kichwa chako kwa kutumia mwanga usioonekana kwa jicho la binadamu (UV), kwa sababu choa hung'aa chini ya mwanga wa UV na upele mwingine haufanyi hivyo.
Je, mdaktari wanatibu vipi choa wa ngozi ya kichwa?
Madaktari hutibu choa wa ngozi ya kichwa katika watoto kwa kutumia:
Dawa ya kuvu ya kumeza kwa wiki 4 hadi 6
Malai ya dawa ya kuvu yanayopakwa kwenye ngozi ya kichwa cha mtoto hadi maambukizi yaishe
Agizo-shampuu ya salfaidi ya saliniamu yenye nguvu kwa ajili ya kuosha nywele za mtoto, angalau mara mbili kwa wiki
Kwa kerioni, kwa kumeza kotikosteroidi
Watoto wanaweza kuenda shuleni wakati wa matibabu.
Madaktari hutibu choa wa ngozi ya kichwa katika watu wazima kwa kutumia:
Dawa ya kuvu ya kumeza kwa wiki 3 hadi 4