Mvilio wa damu kwenye mshipa wa ndani ni nini?
Mvilio wa damu kwenye mshipa wa ndani (DVT) ni wakati damu iliyoganda inajiunda ndani ya mshipa mkubwa zaidi. Kwa kawaida mshipa uko ndani sana kwenye mguu wako, lakini damu iliyoganda inaweza kujiunda kwenye mshipa kwenye sehemu yako ya fupanyonga au mkono wako.
Damu iliyoganda ni nzuri wakati inakusaidia kusitisha kuvuja damu baada ya jeraha. Lakini damu iliyoganda ambayo hutokea wakati hauvuji damu inaweza kuwa hatari.
Damu iliyoganda inaweza kujiunda kwenye mishipa ya ndani sana wakati haifai kujiunda
Damu iliyoganda inaweza kukosa dalili au inaweza kusababisha mguu au mkono wako kuvimba na kuuma
Damu iliyoganda inaweza kulegea na kuelekea hadi kwenye mapafu yako (kuziba kwa mishipa ya mapafu), hivyo husababisha matatizo ya kupumua na hata kifo
Ili kuona kama una DVT, madaktari wanaweza kufanya kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti
Madaktari wanaweza kukupatia dawa ili kusaidia kuzuia damu iliyoganda isijiunde na kuizuia kwenda kwenye mapafu yako
Ikiwa dawa haifanyi kazi au hauwezi kuitumia, daktari wako anaweza kuweka kichujio kidogo kwenye mshipa ili kuzuia damu iliyoganda iiliyoachana isiende kwenye mapafu yako
Damu iliyoganda iliyo kwenye mishipa ya ndani zaidi ni hatari zaidi kuliko damu iliyoganda kwenye mishipa iliyo juu karibu na ngozi yako. Damu iliyoganda kwenye mishipa iliyo juu inaitwa mvilio wa damu kwenye mshipa wa juu.
Ni nini husababisha DVT?
Visababishaji kuu vya DVT vinajumuisha:
Jeraha la mshipa: Mshipa wako umejeruhiwa, kama vile kwenye ajali
Tatizo la damu: Una tatizo ambali linasababisha kuganda kwa damu kulioongezeka
Kupumzika kitandani: Mtiririko wa damu kwenye mishipa yako ni wa kasi ya polepole sana kwa sababu uko kwa mapumziko ya kitandani (kwa mfano, baada ya jeraha au kiharusi)
Kitambaa au kombea: Kitambaa au kombea hukuzuia usisongeshe mguu wako
Upasuaji wa mguu: Ulifanyia upasuaji kwenye mguu wako, kama vile mbadala wa magoti au kiuno
Una uwezekano mkubwa wa kupata damu iliyoganda ikiwa:
Una saratani
Una tatizo la damu iliyoganda ambalo lilipitishwa kwenye familia
Utatumia dawa fulani, kama vile dawa za kuzuia mimba
Uvutaji sigara
Ulijifungua hivi karibuni au ulifanyiwa upasuaji
Umekosa maji mwilini (maji kidogo zaidi au viowevu kwenye mwili wako), haswa ikiwa wewe ni mtu mzima mzee
Unaketi kwa muda mrefu, kama vile ndege
Je, dalili za DVT ni zipi?
Nusu ya watu walio na DVT hawana dalili.
Ikiwa damu iliyoganda iko kwenye mshipa wa mguu wa ndani zaidi, ambayo ni sehemu ya kawaida zaidi, hivyo shavu au mguu wako unaweza:
Kuvimba
yenye uchungu
Nyekundu
Ni nyororo ukigusa
Joto
Damu iliyoganda inaweza kuachana na kusafiri kwenye mapafu yako. Hii ni hali ya kutishia maisha inayoitwa kuziba kwa mishipa ya mapafu. Ikiwa una hii, unaweza:
Kuishiwa na pumzi
Maumivu ya kifua
Kuhisi kizunguzungu na udhaifu (kutokana na shinikizo la damu la chini)
Matatizo ya DVT ni gani?
Kuna matatizo 2 makuu ya mvilio wa damu kwenye mshipa wa ndani:
kuziba kwa mishipa ya mapafu: Sehemu ya damu iliyoganda inaachana na kusafiri kwenye mapafu yako
Upungufu wa vena wa muda mrefu: Damu iliyoganda huharibu daima mshipa wako
Kuziba kwa mishipa ya mapafu kunaweza kusababisha:
Kuishiwa na pumzi
Maumivu ya kifua
Udhaifu na kizunguzungu
Kifo
Upungufu wa vena wa muda mrefu kuzuia damu kutiririka vizuri kupitia kwneye mshipa ulioharibika. Inaweza kusababisha kuvimba kwa daima na kuhisi vibaya kwenye mguu au mkono wako.
Madaktari wanawezaje kujua kama nina DVT?
Madaktari huangalia uwepo wa damu iliyoganda kwa kutumia vipimo kama vile:
Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti
Kipimo cha damu ili kupima kitu kinachoachiliwa kutoka kwenye damu iliyoganda
Madaktari hutibu DVT vipi?
Kawaida, matibabu yanahusisha:
Dawa za kuyeyua damu ili kuzuia kuganda zaidi
Ikiwa dawa za kuyeyua damu hazifanyi kazi au hauwezi kuzitumia kwa sababu fulani, madaktari kwa nadra wanaweza:
Kuweka kichujio cha kuzuia damu kuganda kwenye mshipa mkuu ambao unaelekea kwenye moyo wako—hii inaweza kusaidia kuzuia kuziba kwa mishipa ya mapafu
Kwa nadra, ikiwa una damu iliyoganda kubwa sana, madaktari wanaweza kukupea dawa za kuyeyusha damu iliyoganda kwenye mshipa wako. Hata hivyo, madaktari hawafanyi hivi mara nyingi kwa sababu dawa ya kuyeyusha damu iliyoganda inaweza kusababisha kuvuja damu kunaotishia maisha.
Kuwa amilifu kimwili hakuongezei hatari ya kuziba kwa mishipa ya mapafu na haitafanya uwezekano wa damu iliyoganda kuachana uongezeke.
Ninawezaje kuzuia DVT?
Unaweza kupunguza uwezekano wa kupata DVT:
Ukiinua miguu yako unapokuwa umeketi, kuinamisha na kulainisha kifundo cha mguu wako mara 10 kila nusu saa na kutembea au kulainisha baada ya kila saa 2—hii husaidia mtiririko wa damu na kutuliza kuvimba kwa miguu yako
Ukitumia dawa yoyote ya kuyeyusha damu ambayo daktari wako anakuandikia
Ikiwa uko kwa hatari kubwa zaidi, valia mavazi ya ndani yanayobana (mavazi ya ndani yanayobana) katika mchana au utumie vifungaji mguu vilivyojawa na hewa vilivyounganishwa kwenye mashine ambayo inabana miguu yako mara kwa mara (kubana kwa nyumatiki ya vipindi).