Upungufu wa Vena wa Muda Mrefu na Ugonjwa wa Baada ya Thrombotic

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2023 | Imebadilishwa Dec 2023

Upungufu wa vena wa muda mrefu na ugonjwa wa baada ya thrombotic ni nini?

Upungufu wa vena wa muda mrefu ni kuharibika kwa mishipa ya mguu wako ambayo huzuia damu yako kutiririka kwa njia ya kawaida.

Uvimbe wa vena ni kuvimba kwa mojawapo ya mishipa yako. Mara nyingi unasababishwa na damu iliyoganda kwenye mshipa wako. Ugongwa wa baada ya thrombotic ni tatizo ambalo hutokea baada ya kuwa na uvimbe wa vena.

  • Upungufu wa vena wa muda mrefu unaweza kusababisha maumivu au uchungu, kuvimba, upele wa ngozi na mabadiliko kuhusu jinsi mguu wako unakaa

  • Madaktari hufanya kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti ili kuangalia mtiririko wa damu kwenye mishipa ya mguu wako ili kujua kama una upungufu wa vena wa muda mrefu

  • Ili kutibu upungufu wa vena wa muda mrefu, kuweka mguu wako ukiwa umeinuka, kuvalia mavazi ya ndani yasiyobana na kwa umakinifu kutibu vidonda vyovyote vya ngozi

Je, nini husababisha upungufu wa vena wa muda mrefu?

Kisababishi kikuu cha upungufu wa vena wa muda mrefu ni:

Damu iliyoganda kwenye mshipa wako inaweza kusababisha kupata madoa na matatizo kwa vali kwenye mshipa. Vali ni vifuniko 2 vya tishu ambavyo vinafa nya kazi kama lango la mwelekeo mmoja. Huruhusu damu kutiririka kwenye mwelekeo mmoja pekee, damu hukusanyika kwenye miguu yako. Ikiwa vali imeharibika, damu hukusanyika kwenye miguu yako. Kuharibika kwa vali baada ya kupata damu iliyoganda kwenye mshipa kunaweza kusababisha matatizo ya mguu inayoitwa ugonjwa wa baada ya thrombotic.

One-Way Valves in the Veins

One-way valves consist of two flaps (cusps or leaflets) with edges that meet. These valves help veins return blood to the heart. As blood moves toward the heart, it pushes the flaps open like a pair of one-way swinging doors (shown on the left). If gravity or muscle contractions momentarily pull the blood backward or if blood begins to back up in a vein, the flaps are immediately pushed closed, preventing backward flow (shown on the right).

Una uwezekano mkubwa wa kupata upungufu wa vena wa muda mrefu ikiwa:

  • Una jeraha la mguu

  • Wewe ni mtu mzee

  • Una uzani mkubwa sana kupita kiasi

Je, dalili za upungufu wa vena wa muda mrefu ni zipi?

Dalili zinaweza kujumuisha:

  • Kuvimba mguu ambako kwa kawaida kunapona baada ya kulala chini kwa saa kadhaa

  • Mishipa ya Iliyovimba daima (mishipa iliyovimba kwenye miguu yako ambayo mara nyingi unaweza kuona kama uvimbe chini ya ngozi yako)

  • Ngozi yenye magamba, inayowasha kwenye sehemu ya ndani ya kifundo cha mguu—ngozi inaweza kubadilika iwe ya rangi ya wekundu-kahawia

Ikiwa una upungufu wa vena kali:

  • Mguu wako wa chini unaweza kuongezeka kwa ukubwa kuliko kawaida

  • Unaweza kupata vidonda vya ngozi (vidonda vilivyopasuka) ambazo haziponi vizuri

Madaktari wanawezaje kujua kuwa nina upungufu wa vena wa muda mrefu?

Kwa kawaida madaktari wanaweza kujua kama una upungufu wa vena wa muda mrefu kutokana na dalili zako na uchunguzi wa kimwili.

Wakati mwingine madaktari watafanya kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti cha miguu yako.

Madaktari wanatibu aje upungufu wa vena wa muda mrefu?

Matibabu yanajumuisha:

  • Kupumzisha mguu wako na kuuinua juu ya moyo wako—utafanya hivi kwa nusu saa au zaidi, angalau mara 3 kwa kila siku

  • Kufinyiza (kubana) mguu wako kwa kutumia bedeji nyumbufu, mavazi maalum ya ndani, au kanga zilizojaa hewa vilivyounganishwa kwenye mashine ambayo inabana miguu yako mara kwa mara

  • Kutunza vizuri vidonda vyovyote vya ngozi

Daktari wako anaweza kutumia bedeji ambazo zina dawa ndani yake ili kusaidia vidonda vya ngozi kupona.

Ninawezaje kuzuia upungufu wa vena wa muda mrefu?

Kufanya mabadiliko kwenye maisha yako kunaweza kusaidia, kama vile:

  • Kupunguza uzani

  • Kuwa amilifu kila siku

  • Kula chumvi kidogo (sodiamu)

Ikiwa umekuwa na mvilio wa damu kwenye mishipa ya ndani, daktari wako anaweza kuandikia dawa za kufanya damu iwe nyepesi ili kuzuia ugonjwa wa baada ya mvilio.