Kuoza kwa Tishu za Magamba ya Figo

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023

Figo zako ni viungo 2 vyenye umbo la maharagwe ambavyo hutengeneza mkojo (haja ndogo), husawazisha viwango vya maji na madini mwilini, na huchuja uchafu kwenye damu yako.

The Urinary Tract

Je, kuoza kwa tishu za magamba ya figo ni nini?

Kuoza kwa tishu za magamba ya figo ni kufa kwa tishu kwenye tabaka la juu (ganda) la figo moja au yote.

Kuoza kwa tishu za magamba ya figo kunasababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu ambayo huleta damu kwenye figo.

  • Kuoza kwa tishu za magamba hutokea pale kitu kinapoingilia mtiririko wa damu kwenye figo zako

  • Mara nyingi husababishwa na matatizo makubwa ya kiafya ambayo husababisha kupungua kwa shinikizo la damu

  • Kuoza kwa tishu za magamba hufanya figo zako ziache kufanya kazi yake (figo kushindwa kufanya kazi)

  • Unakojoa mara chache, una mkojo mweusi, homa, na maumivu kwenye sehemu ya chini ya mgongo

  • Madaktari wanapaswa kutibu tatizo linalosababisha kuoza kwa tishu za magamba ya figo na wanaweza kutumia majimaji na dawa za kuua bakteria

Je, nini husababisha kuoza kwa tishu za magamba ya figo?

Sababu hutegemea umri.

Kwa watoto waliozaliwa karibuni, sababu ni pamoja na:

kwa watoto, husababishwa na:

Kwa watu wazima, sababu ni pamoja na:

Je, dalili za kuoza kwa tishu za magamba ya figo ni zipi?

Kwa kawaida unakuwa huna dalili isipokuwa kama ukipata hali ya kushindwa kwa figo kufanya kazi. Dalili za figo kushindwa kufanya kazi ni pamoja na:

  • Kuhisi udhaifu na uchovu

  • Kuhisi mgonjwa tumboni

  • Kutohisi njaa kama kawaida

  • Kuwasha

  • Kuhisi usingizi au kuchanganyikiwa

Je, madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa kuoza kwa tishu za magamba ya figo?

Madaktari hushuku uwepo wa ugonjwa wa kuoza kwa tishu za magamba ya figo ikiwa una mojawapo ya magonjwa yanayoweza kuusababisha na vipimo vya kila mara vinaonyesha figo zako hazifanyi kazi vizuri. Ili kuwa na uhakika, wanaweza kufanya:

  • Angiografia ya upimaji kwa kompyuta (CTA)—aina ya uchanganuzi wa CT unaozingatia mishipa ya damu

Je, madaktari hutibu vipi kuoza kwa tishu za magamba ya figo?

Madaktari hutibu chanzo kilichosababisha kuoza kwa tishu za magamba.

Ikiwa una tatizo la figo kushindwa kufanya kazi, unaweza kuhitaji: