Muhtasari wa Bakteria

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Je, bakteria ni nini?

Bakteria ni viumbe hai wadogo. Ni wadogo sana na hawaonekani bila kutumia hadubini. Nywele ya binadamu ni pana mara 100 kuliko bakteria nyingi wa kawaida. Bakteria hawafanani na viumbe wengine wadogo sana kama vile virusi au kuvu.

Kuna maelfu ya aina mbalimbali za bakteria. Bakteria wana maumbo mbalimbali, ambayo huwasaidia madaktari kuwatambua.

Bakteria huishi kila mahali, ikujumuisha:

  • Ardhini

  • Kwenye maji

  • Kwenye ngozi yako

  • Mdomoni, kwenye utumbo na uke wako

Bakteria huzaa kwa haraka wanapokuwa katika mazingira sahihi. Bakteria wachache wanaweza kuongezeka hadi kuwa bilioni ndani ya siku moja.

Je, maambukizi ya bakteria ni nini?

Maambukizi ya bakteria ni pale bakteria wanapovamia sehemu ya mwili wako na kukufanya uumwe. Maambukizi ya kawaida ya bakteria ni pamoja na:

Baadhi ya bakteria huachia sumu za kemikali zinazoitwa toksini. Sumu husambaa kupitia damu na kuathiri maeneo ambayo hayajavamiwa na bakteria. Magonjwa yanayosababishwa na toksini za bakteria ni pamoja na:

Je, bakteria wote hukufanya uumwe?

Hapana, bakteria wengi hawasababishi maambukizi. Hata baadhi yao hutoa msaada mkubwa. Bakteria wengi wanaoishi kwenye ngozi yako au kwenye mwili wako ni wa kawaida na hawakudhuru. Hawa huitwa vijidudu wako wakaaji. Hata hivyo, bakteria wengine ambao hupanda au kuingia kwenye mwili wako wanaweza kuzishambulia.

Je, unapataje maambukizi ya bakteria?

Bakteria hatari wanaweza kuingia kwenye mwili wako kwa njia mbalimbali. Unaweza:

  • Kula au kunywa kitu chenye bakteria ndani yake

  • Vuta hewa ambayo imebeba bakteria

  • Kugusa kitu kilichochafuliwa kwa bakteria kisha ukagusa mdomo, pua au macho

  • Kupata mkwaruzo, mchubuko au kuungua ambapo huruhusu bakteria kuingia mwilini mwako

Baadhi ya bakteria wenye madhara, kama vile wale wanaosababisha pepopunda, hutoka kwenye mazingira. Hata hivyo, bakteria wengi wenye madhara hutoka kwa watu au wakati mwingine kwa wanyama wenye maambukizi.

Wakati mwingine bakteria wa kawaida mwilini mwako huingia mahali ambapo si sahihi. Kwa mfano, bakteria wa kawaida kwenye utumbo wako wanaweza kusababisha maambukizi iwapo wataingia kwenye kibofu cha mkojo au kwenye mtiririko wako wa damu.

Je, mwili wako unajikingaje dhidi ya bakteria?

Mwili wako una njia za kujikinga dhidi ya bakteria:

  • Ngozi na utando wa utumbo wako huzuia bakteria wengi wasiingie ndani

  • Mfumo wako wa kingamwili hushambulia bakteria wanaoingia kwenye mwili wako

Mfumo wako wa kingamwili unatumia seli nyeupe za damu kutambua bakteria hatarishi. Baadhi ya seli nyeupe za damu zinaua bakteria moja kwa moja. Zingine hutengeneza dutu zinazoitwa kingamwili ambazo huua bakteria.

Je, madaktari wanajuaje kuwa una maambukizi ya bakteria?

Madaktari hushuku kuwa una maambukizi ya bakteria kutokana na dalili zako. Kwa kawaida watatuma sampuli kwenye maabara kwa ajili ya kupima bakteria. Kulingana na mahali ambapo maambukizi yanaonekana, huenda daktari akatuma sampuli ya:

  • Damu

  • Mkojo

  • Kikohozi (kamasi unayokohoa)

  • Sampuli kutoka kwenye koo, uume, au uke

Maabara inaweza kumjulisha daktari kama bakteria wapo, aina yake, na aina ya dawa za kuua bakteria zinazoweza kuwaua.

Je, madaktari hutibu vipi maambukizi ya bakteria?

Mwili wako unaweza kupambana na baadhi ya maambukizi ya bakteria peke yake. Lakini kwa maambukizi mengi ya bakteria, madaktari watakupatia:

dawa za kuua bakteria, kama vile Penisilini, ni dawa zinazoua bakteria. Kuna aina nyingi tofauti za dawa za kuua bakteria. Kila dawa ya kuua bakteria hufanya kazi dhidi ya aina fulani ya bakteria.

Ikiwa una maambukizi makali ya bakteria, unaweza kuhitaji kufika hospitali na kuingizwa moja kwa moja dawa za kuua bakteria kupitia mshipa (IV).

Je, usugu wa dawa za kuua bakteria ni nini?

Usugu wa dawa za kuua bakteria unamaanisha kuwa bakteria hawezi kuawa na dawa fulani za kuua bakteria.

Bakteria wana usugu wa asili kwa baadhi ya dawa za kuua bakteria. Hata hivyo, bakteria mara nyingi huwa sugu kwa dawa za kuua bakteria ambazo zilifanya kazi hapo awali. Zinakuwa kinzani kwa sababu jeni zao hubadilika au kupata jeni kutoka kwa bakteria zingine ambazo zimekuwa kinzani. Hurithisha hizi jeni za ukinzani kwa vizazi vyao.

Usugu kwa dawa za kuua bakteria ni tatizo kubwa Maambukizi sugu yanahitaji dawa kali zaidi za kuua bakteria ambazo mara nyingi huwa na athari za kando. Hata kwa dawa kali za kuua bakteria, maelfu ya watu hufa kila mwaka kutokana na maambukizi sugu dhidi ya dawa za kuua bakteria.

Jinsi dawa za kuua bakteria zinapotumika kila mara, ndivyo uwezekano wa bakteria sugu unavyoongezeka. Hii inaamanisha kwamba usugu kwa dawa za kuua bakteria mara nyingi hutokea hospitali na pia katika baadhi ya mashamba ya wanyama ambao hupewa dawa za kuua bakteria kila mara. Bakteria sugu wanaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kusambaa huku ni hatari hasa hospitalini, ambapo watu wengi wana mfumo dhaifu wa kingamwili au tayari wanaumwa sana.

Je, unawezaje kuzuia maambukizi ya bakteria?

Ili kuzuia maambukizi ya bakteria:

  • Nawa mikono yako mara kwa mara, haswa ikiwa unashika chakula au unaingiliana sana na watu

  • Andaa na upike chakula vizuri

  • Shiriki ngono kwa njia salama

  • Pata chanjo ambazo daktari wako anasema unazihitaji