Maambukizi ya Koo

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Maambukizi ya koo ni nini?

Maambukizi ya koo yanaweza kujumuisha upande wa nyuma wote wa koo lako au findo zako tu. Findo ni uvimbe mdogo wa tishu nyuma ya koo lako. Findo husaidia kupambana na maambukizi lakini wakati mwingine hupata maambukizi. Maambukizi kwenye findo huitwa mafindofindo.

  • Kila mtu anapata maambukizi ya koo, lakini mafindofindo hutokea sana kwa watoto

  • Maambukizi ya koo kwa kawaida yanasababishwa na virusi lakini yanaweza kusababishwa na bakteria

  • Dalili zake ni pamoja na maumivu makali unapomeza na findo kuvimba na kuwa nyekundu

  • Ikiwa hautatibiwa, mafindofindo yanayotokana na bakteria yanaweza kubadilika kuwa jipu la findo (mkusanyiko wa usaha nyuma ya findo zako), lakini hali hii ni nadra

  • Ikiwa unapata mafindofindo mara nyingi sana, daktari wako anaweza kufanya upasuaji ili kuondoa findo zako (upasuaji wa kuondoa findo)

Nini kinachosababisha maambukizi ya koo?

Maambukizi ya koo yanasababishwa na:

Dalili za maambukizi ya koo ni zipi?

Dalili za kawaida ni:

  • Koo lenye vidonda ambalo hali inakuwa mbaya unapomeza au kuzungumza

  • Koo jekundu na findo

  • Vinundu vya limfu vilivyovimba na laini kwenye shingo

Vinundu vya limfu na tishu ndogo zinye umbo la harage zinazosaidia mwili wako kupambana na maambukizi. Watu wengine kwa kukosea wanaziita "tezi" na wanazungumza kuhusu "tezi zilizovimba" wakati koo lao lina vidonda.

Wakati mwingine unaweza pia kupata:

  • Maumivu kwenye masikio yako

  • Homa

  • Madoa meupe kwenye findo zako

  • Harufu mbaya mdomoni

Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina maambukizi kwenye koo?

Madaktari wanaweza kujua endapo koo lako lina maambukizi kwa kuangalia kwenye koo lako na kuona kwamba ni jekundu. Wakati mwingine watachukua ute kwenye koo lako na kufanya kipimo cha strep, ili kuona kama koo lenye strep linasababisha maambukizi.

Findo kubwa, nyekundu zilizovimba zenye madoa meupe zinaweza kusababishwa au zisisababishwe na koo lenye strep. Aina zote za maambukizi ya koo zinaweza kuonekana hivyo, si strep tu.

Je, madaktari wanatibu vipi maambukizi kwenye koo?

Madaktari wanatibu maambukizi ya koo kwa kutumia:

  • Dawa za maumivu za kununua dukani, kama vile acetaminopheni au ibuprofeni

  • Wakati mwingine, kotikosteroidi ili kusaidia dalili ziondoke haraka

  • Dawa za kuua bakteria, lakini ikiwa tu una maambukizi ya bakteria, kama vile koo lenye strep

Ikiwa unapata mafindofindo makali kutokana na koo lenye strep mara nyingi sana, daktari wako anaweza kupendekeza kufanya upasuaji ili kuondoa findo zako (upasuaji wa kuondoa findo)