Maambukizi ya Streptococcal

(Maambukizi ya Strep)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Je, maambukizi ya streptococcal (strep) ni nini?

Streptokokali (kwa urahisi huitwa strep) ni kikundi cha kawaida cha bakteria. Aina tofauti za maambukizi husababisha magonjwa tofauti. Mara nyingi husababisha vidonda vya koo (koo lenye strep) au maambukizi ya ngozi. Lakini wanaweza kusababisha maambukizi yenye kutishia maisha kwenye sehemu nyingine ya mwili wako.

  • Bakteria wa streptokokali wanaweza kuishi ndani na juu ya mwili wako bila kusababisha dalili zozote.

  • Maambukizi yanaweza kutokea kwenye koo, sikio la kati, sanasi, mapafu, ngozi au tishu zako zilizo chini ya ngozi yako, vali za moyo na damu

  • Maambukizi yanaweza kusababisha tishu zilizovimba zenye kuuma na nyekundu, vidonda vyenye magamba, koo kuuma, na upele

  • Madaktari hutibu maambukizi ya streptococcal kwa kutumia dawa za kuua bakteria

Je, nini husababisha maambukizi ya strep?

Bakteria wa streptokokali wanaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa:

  • Kuvuta ndani matone yenye maambukizi kutoka kwa chafya au kikohozi cha mtu.

  • Kugusa kidonda kilichoambukizwa

  • Kujifungua, ambapo inaweza kusambaa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto

Je, zipi ni dalili za maambukizi ya strep?

Kuna dalili mbalimbali kulingana na sehemu yalipo maambukizi:

  • Maambukizi kwenye koo (koo lenye strep): Koo lenye vidonda, mabonge yaliyovimba kwenye shingo yako, homa, usaha kwenye findo zako

  • Maambukizi ya ngozi: Sehemu nyekundu yenye uchungu kwenye ngozi yako (selulitisi) au vidonda vyenye magamba ya njano (upele ambukizi wa malengelenge)

  • Maambukizi chini ya ngozi yako (kufa kwa tisho za utando): Mzizimo, homa na maumivu makali na kulainika katika sehemu ya mwili yenye maambukizi

Kufa kwa tishu za utando ni hali ya hatari sana. Unaweza kupata gangrini na kupoteza mkono au mguu au hata kufa.

Je, ni matatizo gani husababishwa na maambukizi ya strep?

Homa itokanayo na baridi yabisi husababisha upate maumivu makali, kuvimba kwa vifundo Watoto wenye homa itokanayo na baridi yabisi wanaweza kupata mishtuko ya kusogeza mikono na miguu yao ambayo hawawezi kuidhibiti Wakati mwingine homa itokanayo na baridi yabisi huharibu vali za moyo. Lakini kwa kawaida uharibifu wa vali za moyo huwa hauonekani kwa miaka mingi.

Homa ya vipele vyekundu hukufanya upate upele usoni, na kisha sehemu zingine za mwili wako. Upele huwa na hisia kama ya msasa. Unapopotea, ngozi yako hubanduka. Ulimi wako hupata viuvimbe vyekundu hivyo kufanana na stroberi (huitwa ulimi wa stroberi).

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina maambukizi ya strep?

Daktari atapima sampuli kutoka kwenye koo lako au tishu nyingine iliyoambukizwa.

Je, madaktari hutibu vipi maambukizi ya strep?

Madaktari hutibu maambukizi ya strep kwa kutumia dawa za kuua bakteria.

Kwa kufa kwa tishu za utando, utalazwa hospitaini na kufanyiwa upasuaji ili kuoadoa tishu zilizokufa, zenye maambukizi.