Angioedema ya Kurithi na Isiyo ya Kurithi ni nini?
Angioedema ni kuvimba kwa uso, midomo, ulimi, na koo ambako kwa kawaida husababishwa na mmenyuko wa mzio. Lakini angioedema inaweza pia kusababishwa na tatizo fulani la mfumo wako wa kingamwili.
Angioedema ya kurithi ni tatizo la mfumo wa kingamwili ambalo unazaliwa nalo
Angioedema inayokushika kiasili ni tatizo la mfumo wa kingamwili linalosababishwa na ugonjwa au hali nyingine
Angioedema ya kurithi na isiyo ya kurithi ni kama angioedema inayosababishwa na mmenyuko wa mzio, lakini haiwashi na hupatwi na mabaka (mabaka mekundu, yanayowasha, yaliyoinuka kwenye ngozi).
Midomo, ulimi, na koo lako linaweza kuvimba, na huku kunaweza kusababisha matatizo ya kupumua
Unaweza kuugua tumbo lako na kutapika
Madaktari wanaweza kutumia dawa kutibu na kuzuia uvimbe
DKT P. MARAZZI/MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI
Angioedema ya Kurithi na Isiyo ya Kurithi husababishwa na nini?
Angioedema ya Kurithi ipo kwenye jeni (hurithiwa kutoka kwa mzazi). Hali hiyo huwepo tayari wakati wa kuzaliwa, lakini dalili huanza unapokuwa mtoto au kijana.
Angioedema isiyo ya Kurithi inaweza kutokea baada ya kupata baadhi ya saratani au mfumo wa kingamwili kwenda kinyume na mwili (ugonjwa unaosababisha mfumo wa kinga ya mwili wako kushambulia tishu zake). Dalili huanza baadaye katika maisha.
Je, kitu gani kinaweza kuchochea shambulio la angioedema?
Katika angioedema ya kurithi na isiyo ya kurithi, uvimbe unaweza kuchochewa na:
Jeraha ndogo
Maambukizi
Vyakula fulani
Ujauzito
Baridi
Msongo wa mawazo
Dalili za angioedema ya kurithi na isiyo ya kurithi ni zipi?
Dalili zinaweza kujumuisha uvimbe wenye uchungu kwenye:
Uso
Midomo
Ulimi
Mikono
Miguu
Sehemu za siri
Utando wa mdomo, koo, njia za hewa, na njia ya mmeng'enyo wa chakula
Dalili zingine ni pamoja na:
Kuhisi mgonjwa tumboni
Kutapika
Kukakamaa
Kuvimba kwa kisanduku cha sauti, koo, au ulimi kunaweza kusababisha matatizo ya kupumua.
Picha hii inaonyesha uvimbe midomoni mwa mtu aliye na angioedema ya kurithi.
Kwa idhini ya mchapishaji. Kutoka kwa Joe E, Soter N. In Current Dermatologic Diagnosis and Treatment, ilihaririwa na I Freedberg, IM Freedberg, na MR Sanchez. Philadelphia, Current Medicine, 2001.
Mtu huyu ana ulimi uliovimba kutokana na angioedema.
MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI
Mtu huyu amevimba midomo kutokana na angioedema.
DKT P. MARAZZI/MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI
Madaktari wanawezaje kujua kama nina angioedema ya urithi au isiyo ya kurithi?
Madaktari watashuku angioedema ya kurithi au isiyo ya kurithi ikiwa unapata uvimbe lakini hakuna mabaka. Ili kuthibitisha, daktari atafanya:
Vipimo vya damu
Madaktari hutibu vipi angioedema ya kurithi na isiyo ya kurithi?
Madaktari hukutibu kwa:
Dawa ambazo husaidia mfumo wako wa kingamwili
Madaktari pia wanaweza kukupa dawa za kuzuia uvimbe, haswa kabla ya vichochezi vinavyojulikana.
Matibabu ya njia ya hewa iliyozuiwa
Iwapo njia yako ya hewa imevimba na una matatizo ya kupumua, madaktari watahitaji kufungua njia yako ya hewa. Ili kufanya hivyo, wanaweza:
Kukupa dawa ya sindano ya kupunguza uvimbe
Kuweka bomba la kupumua kupitia pua au mdomo wako
Iwapo kuna uvimbe mwingi kwenye eneo la pua na mdomo, wanaweza kuweka bomba la kupumulia kwa kukata kwenye ngozi ili kufikia boma la pumzi