Mzio wa Chakula

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2022

Mzio wa chakula ni nini?

Mzio hutokea pale ambapo mfumo wa kingamwili humenyuka kutokana na kitu kisicho na madhara, kama vile chakula, mimea, au dawa. Mzio wa chakula ni mmenyuko wa mzio unaosababishwa na chakula fulani.

  • Karibu chakula vyote vinaweza kusababisha mmenyuko wa mzio

  • Dalili za mzio wa chakula ni pamoja na upele unaowasha, makamasi puani, na wakati mwingine kuforota.

  • Ingawa ni nadra, mmenyuko mkali wa mzio wa chakula kuhatarisha maisha (mmenyuko kama huo huitwa mmenyuko wa anafailaktiki)

  • Watoto wanaweza kuacha kuwa na mizio ya chakula wanapokua

  • Mtu mzima akipata mzio wa chakula, kwa kawaida hauishi tena

  • Madaktari wanaweza kufanya vipimo vya ngozi na damu na kujaribu kuondoa vyakula kutoka kwa lishe yako ili kujua ni chakula gani kinachosababisha mzio.

Ni vyakula gani vinavyosababisha mmenyuko wa mzio?

Karibu chakula chochote kinaweza kusababisha mmenyuko wa mzio. Sababu zinazoonekana sana hutegemea umri wa mtu.

Kwa watoto wachanga na watoto wadogo vichochezi vinavyojulikana zaidi ni:

  • Mayai

  • Maziwa

  • Ngano

  • Karanga

  • Soya

Kwa watoto wakubwa na watu wazima vichochezi vinavyojulikana zaidi ni:

  • Njugu

  • Vyakula vya baharini

Dalili za mzio wa chakula ni zipi?

Kwa watoto, dalili za mzio wa chakula zinaweza kubadilika kadiri mtoto anavyokua.

Watoto wachanga wanaweza kuonyesha dalili kama vile:

  • Upele

  • Kutapika

  • Kuharisha

Watoto wenye umri wa mwaka 1 na zaidi wanaweza:

  • Upele

  • Kuforota (sauti ya mluzi unapopumua)

  • Pua zinazotoa kamasi

Kufikia umri wa miaka 10, mizio ya chakula mara nyingi huisha (kama vile mzio wa maziwa).

Kwa watu wazima na watoto wakubwa, dalili za mzio wa chakula zinaweza kuwa mbaya zaidi na zinaweza kujumuisha:

  • Mdomo kuwasha

  • Mabaka (mekundu, yanayowasha, yaliyoinuka kwenye ngozi)

  • Eksema (vipele vyekundu vya ngozi, vilivyokauka, kama vile magamba, hutokea kwenye sehemu ambapo mikono na miguu hujikunja)

  • Pua zinazotoa makamasi na pumu

  • Maumivu ya tumbo

  • Kuumwa na tumbo

  • Kusokota na kuhara

Mzio wa chakula ukiwa mkali sana, unaweza kusababisha mmenyuko wa anafailaktiki, ambao unaweza kusababisha upele mwili mzima, uvimbe wa koo, na matatizo ya kupumua. Isipotibiwa, unaweza kufariki.

Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nina mzio wa chakula?

Daktari wako anaweza kupima mzio wa chakula kupitia njia moja au zaidi kati ya hizi:

  • Kipimo cha kuchoma ngozi, ambacho kinahusisha kuweka kiasi kidogo cha chakula juu ya ngozi yako na kisha kuichoma kwa sindano ili kuangalia kinachofuata.

  • Kipimo cha damu

  • Kuondoa vyakula, ambako kunajumuisha kutokula vyakula ambavyo vinashukiwa kusababisha mzio, na kisha kuviongeza moja baada ya nyingine ili kujua ni chakula gani kinachosababisha tatizo.

Madaktari hutibu vipi mzio wa chakula?

Matibabu ni kuepuka vyakula ambavyo husababisha upate dalili za mzio. Ili kupunguza dalili zako, daktari wako anaweza kukuagiza:

  • Umeze dawa za antihistamini ili kutuliza mabaka na uvimbe

  • Ubebe sindano ya epinefrini ili uitumie ukipata dalili kali na kuzuia mmenyuko wa anafailaktiki