Kifo cha Ghafla cha Mshtuko wa Moyo kwa Wanariadha

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024

Kifo cha ghafla cha mshtuko wa moyo kwa wanariadha ni wati mtu anafariki kwa ghafla kutokana na matatizo ya moyo yaliyoletwa na mazoezi.

  • Kifo cha ghafla cha mshtuko wa moyo kwa wanariadha ni cha nadra (takriban 1 kati ya wanariadha 200,000)

  • Inaweza kutokea kwa watu wazee ambao wanajua kuwa wana matatizo ya moyo

  • Pia inaweza kutokea kwa watu ambao ni wachanga na wanaonekana kuwa wenye afya lakini wana tatizo la moyo ambalo hawajui kuhusu

  • Ongea na daktari wako kabla ya kuanzia spoti au mazoea mapya ya mazoezi

Pia watu wanaweza kufariki wakati wa mazoezi kwa sababu ya vitu kama shambulio la pumu, kiharusi cha joto, au jeraha. Kwa kawaida hizi hazitambuliwi kuwa vifo vya ghafla vya moyo kwa sababu tatizo la moyo si kisababishaji kuu.

Ni nini husababisha kifo cha ghafla cha mshtuko wa moyo kwa wanariadha?

Wazee wanaokufa kutokana na tatizo la moyo linaloletwa na mazoezi kwa kawaida huwa na ugonjwa wa ateri ya moyo. Ateri ambazo zinapeleka oksijeni kwenye moyo zimefungika. Wanaweza au kutoweza kujua wana tatizo la moyo.

Watu wachanga kwa kawaida wana tatizo la nadra la moyo ambalo walizaliwa nalo. Kwa kawaida hawajui wana tatizo la moyo.

Tatizo la kawaida zaidi la moyo kwa watu wachanga ni:

Tatizo la kawaida zaidi la moyo kwa watu wenye umri mdogo ni:

  • Hali za moyo ambazo hufanya mdundo wa moyo wako usiwe wa kawaida unapofanya mazoezi au kuhisi shinikizo, kama vile ugonjwa wa QT ndefu

  • Valvu ya moyo iliyo na kasoro (stenosis ya aota)

  • Sehemu dhaifu au uvimbe katika sehemu ya aota yako (ateri kuu ambayo hubeba damu kutoka kwenye moyo wako hadi kwenye mwili mwingine—sehemu au uvimbe dhaifu unaitwa aneurysm ya aota)

  • Kasoro za kuzaliwa kwenye ateri zako za moyo (mishipa ya damu ambayo huletea moyo wako oksijeni)

  • Moyo uliotanuka

Katika umri wowote, una uwezekano mkubwa wa kupatwa na kifo cha ghafla cha mshtuko wa moyo wakati wa mazoezi ikiwa unatumia dawa za mtaani ambazo zinasisimua moyo. Dawa kama hizo zinajumuisha kokeini na amfetamini.

Je, dalili za kifo cha ghafla cha mshtuko wa moyo ni zipi?

Wanariadha wengi vijana wana afya na hawajui wana tatizo la moyo. Baadhi ya wanariadha wana ishara za onyo kama vile kuzirai au kukosa pumzi. Wanariadha wanaweza kosa kutambua kuwa hizi ni dalili za tatizo hatari na huenda wasimwambie yeyote.

Hata hivyo, ishara ya kwanza kwa kawaida huwa kuwa mtu anazirai kwa ghafla. Moyo wao haudundi na hawapumui. Kwa kawaida watu hufariki isipokuwa wakipewa CPR (ufufuaji wa moyo na mapafu).

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa niko kwa hatari ya kufariki kwa ghafla kutokana na mshtuko wa moyo?

Ona daktari wako kabla uanze mpango wa mazoezi au spoti. Daktari wako atakuuliza kuhusu historia yako ya afya na kufanya uchunguzi wa kimwili ili kutambua matatizo ambayo yanaweza kufanya mazoezi yawe hatari kwako.

Nchini Marekani, wanariadha wa shule ya upili wanapaswa kufanyiwa uchunguzi kila baada ya miaka 2. Watu wazima wanapaswa kufanyiwa mmoja baada ya kila miaka 4. Huko Uropa, uchunguzi hurudiwa kila baada ya miaka 2 bila kujali umri wa mwanariadha. Madaktari wakijua kuwa una matatizo fulani ya kimatibabu, kwa kawaida watakufanyia uchunguzi mara nyingi.

Hali za hatari ambazo madaktari watakuuliza kuhusu yanajumuisha:

  • Kuwa na dalili kama vile maumivu ya kifua au kujihisi vibaya, moyo unaodunda haraka au mapigo ya moyo yasiyokuwa sawa, kuzirai au kukaribia kuzirai, uchovu na ugumu katika kupumua, hasa pale dalili hizi zinapotokea wakati wa mazoezi makali

  • Kuwa na wanafamilia waliofariki au waliofariki wakati wa mazoezi au ambao walifariki kwa ghafla kabla ya takriban miaka 50

  • Kutumia dawa

Kulingana na umri wako, historia ya afya, dalili na spoti mahususi unazofanya, madaktari wanaweza kufanya vipimo kama vile:

  • Elektrokadiogramu (ECG—kipimo cha haraka, kisicho na maumivu, bila madhara ambacho kinapima mikondo ya umeme ya moyo wako na huirekodi kwenye kijikaratasi)

  • Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti (kipimo ambacho hutumia mawimbi ya sauti ili kuunda picha ya moyo wako na jinsi unavyofanya kazi)

  • Kipimo cha shinikizo (kipimo cha kuangalia jinsi moyo wako unavyofanya kazi wakati unadunda kwa kasi ya juu, kama wakati unapofanya mazoezi)

Katika baadhi ya nchi nje ya Marekani, madaktari wanapendekeza kuwa kila mtu apate ECG kabla ya kuanzia mpango wa mazoezi.

Je, madaktari wanatibu vipi kufariki kwa ghafla kutokana na mshtuko wa moyo?

Mtu anayeacha kupumua na kuzimia anahitaji matibabu ya mara moja:

  • CPR (mbinu ya kuokoa maisha ya kusukuma kwenye kifua na kupatiana upumuaji wa uokoaji)

  • Tumia defaibrileta ya nje (kifaa ambacho huleta mshtuko wa umeme kwenye kifua ili kurejesha mdundo wa moyo wa kawaida)

Ikiwa mtu anaishi, madaktari hutibu hali ambayo ilisababisha tatizo hilo. Wanaweza kukupatia dawa au kuweka defaibrileta ya kupandikiza kwenye moyo. Defaibrileta ya kupandikiza kwenye moyo ni kifaa ambacho madaktari huweka kwenye moyo ili kufuatilia mdundo wake na kuanzisha moyo upya ukiacha kufanya kazi.

Defaibrileta ya Nje ya Kiotomatiki: Kuanzisha Moyo Upya

Defaibrileta ya nje ya kiotomatiki (AED) ni kifaa ambacho kinaweza kutambua na kusahihisha aina ya mdundo wa moyo usio wa kawaida unaoitwa fibrilesheni ya ventrikali. Fibrilesheni ya ventrikali husababisha mshtuko wa moyo.

Ni rahisi kutumia AED. Shirika la Msalaba Mwekundu na mashirika mengine hutoa kipindi vya mafunzo kuhusu matumizi ya AED. Vipindi vingi vya mazoezi vinachukua tu saa chache; lakini kunawezekana kutumia AED hata kama haujawai shiriki katika kozi ya mafunzo. AED tofauti zina maelekezo tofauti ya matumizi. Maelekezo yameandikwa kwenye AED na AED nyingi za kisasa pia hutumia makumbusho ya sauti ili kuelekeza mtumiaji kwa kila hatua. AED zinapatikana katika sehemu nyingi za kukusanyika, kama vile stadia, viwanja vya ndege na kumbi za tamasha. Watu ambao wanaambiwa na daktari wao kuwa wana uwezekano mkubwa wa kupata fibrilesheni ya ventrikali lakini ambao hawana defaibrileta iliyopandikizwa wanaweza kutaka kununua AED ya matumizi ya nyumbani ya wanafamilia, ambao wanapaswa kufunzwa kwa matumizi yake.