Muhtasari wa Uvimbe wa Ubongo kwa Watoto

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2024

Je, uvimbe wa ubongo kwa watoto ni nini?

Uvimbe wa ubongo kwa watoto ni kuota kwa kinyama kwenye ubongo. Uvimbe wa ubongo unaweza kuwa wa saratani (wenye madhara) au usio na saratani. Lakini hata uvimbe usio na kansa unaweza kusababisha matatizo makubwa.

  • Uvimbe wa ubongo ni miongoni mwa saratani zinazowapata sana watoto

  • Uvimbe wa ubongo unaowapata sana watoto ni astrosaitomasi, medulablastomasi, na apendimomasi—kila mojawapo huanza katika sehemu tofauti ya ubongo

  • Mtoto mwenye uvimbe wa ubongo anaweza kupata maumivu ya kichwa, kutapika na matatizo ya kuona au ya kutembea pasipo kuyumba

  • Madaktari hutibu uvimbe wa ubongo kwa kuchanganya upasuaji, tiba ya mionzi au tibakemikali

Je, nini husababisha uvimbe wa ubongo kwa watoto?

Mara nyingi, madaktari hawajui kwanini watoto hupata uvimbe wa ubongo. Hata hivyo, hatari ya uvimbe wa ubongo ni kubwa ikiwa watoto watapokea kiasi kikubwa cha mionzi kwenye kichwa au wakiwa na magonjwa fulani ya kurithi, kama vile nyurofibromatosisi.

Je, dalili za uvimbe wa ubongo kwa watoto ni zipi?

Dalili za uvimbe wa ubongo hutokea kwa sababu uvimbe unaoongezeka hukandamiza ubongo.

Watoto wachanga wanaweza:

  • Kuonekana wameudhika

  • Kulala kila mara au vigumu kuamka wakati ambapo kwa kawaida wangekuwa macho

  • Tapika

Ikiwa uvimbe utaanza mapema kipindi cha uchanga, kichwa cha mtoto wako kinaweza kuonekana kikubwa sana

Watoto wakubwa wana dalili sawa na hizo, lakini pia wanaweza kuwa:

  • Maumivu ya kichwa

  • Matatizo ya kuona, kama vile kuona vitu mara mbili (kuona picha 2 za kitu kile kile)

  • Shida ya kupandisha macho juu

  • Mabadiliko ya kihisia, kama vile kukasirika kirahisi

  • Mabadiliko ya hali ya uchangamfu, kama vile kuchanganyikiwa au kushikwa na usingizi

Dalili zingine hutegemea mahali ambapo uvimbe umeota kwenye ubongo.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana uvimbe wa ubongo?

Madaktari hushuku uwepo wa uvimbe wa ubongo kutokana na dalili za mtoto wako. Ili kujua kama mtoto wako ana uvimbe wa ubongo, madaktari watafanya:

Ikiwa matokeo ya MRI yanaonyesha uwepo wa uvimbe wa ubongo, madaktari wanaweza:

  • Kufanya upasuaji wa kuondoa kipande kidogo cha tishu au uvimbe wote na kuuchunguza kwenye hadubini (huitwa uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi)

Ili kuona kama saratani yoyote imesambaa, madaktari wanaweza pia kukinga majimaji ya uti wa mgongo (kuchukua majimaji ya sampuli kutoka kwenye uti wa mgongo).

Je, madaktari hutibu vipi uvimbe wa ubongo katika watoto?

Timu ya madaktari waliobobea katika kutibu uvimbe wa ubongo kwa watoto hupanga matibabu ya mtoto wako. Ili kutibu uvimbe wa ubongo, madaktari watatumia mchanganyiko wa:

Kama uvimbe huu unazuia mtiririko wa majimaji ya uti wa mgongo, madaktari wanaweza kuweka bomba dongo kwenye ubongo wa mtoto wako ili kutoa majimaji hayo kabla ya upasuaji.