Maumivu ya Kiungo: Kiungo Kimoja

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2023

Viungo ni sehemu katika mwili wako ambapo mifupa miwili huungana, kama vile vifundo vya mikono, viwiko, mabega, nyonga, magoti na vifundo vya miguu.

Viungo pia vipo mahali ambapo hudhanii. Kwa mfano, kuna viungo kati ya mifupa mingi kwenye miguu, mikono, nyonga na uti wa mgongo.

Ni vitu gani husababisha maumivu kwenye kiungo kimoja?

Kwa kawaida, maumivu kwenye kiungo kimoja tu huwa na sababu tofauti na zile za maumivu kwenye viungo vingi.

Kwa watu wenye umri wowote, sababu inayotokea zaidi ya maumivu ya ghalfa ya kiungo kimoja ni:

  • Jeraha

Ikiwa hujajeruhiwa, sababu za kawaida hutegemea umri wako.

Miongoni mwa watu wazima wenye umri wa makamo:

Maambukizi ya viungo mara nyingi husababishwa na kisonono ambacho kimesambaa mwilini kote. Viini vingine vya maradhi, kama vile vilivyo kwenye sehemu ya karibu iliyo na maambukizi ya ngozi au jipu (usaha) pia vinaweza kusababisha maambukizi ya viungo.

Miongoni mwa watu wazima wenye umri wa juu:

Sababu zisizotokea sana za maumivu ya kiungo kimoja ni pamoja na:

Osteonekrosisi wakati mfupa unaharibika na kufa. Mfupa unaweza kufa kutokana na majeraha makubwa (kama vile mfupa wa nyonga uliovunjika) au kama athari ya dawa fulani (kama vile kotikosteroidi).

Je, napaswa kumwona daktari lini?

Mwone daktari mara moja ikiwa una maumivu kwenye kiungo kimoja na dalili yoyote ya tahadhari kati ya zifuatazo:

  • Maumivu makali au ya ghafla

  • Wekundu, joto, kuvimba au kukakamaa kwenye kiungo

  • Homa

  • Ngozi iliyo karibu na kiungo kuwa na kidonda, nyekundu, yenye joto, au maumivu unapoigusa

  • Una tatizo la kutokwa na damu, unatumia viyeyushaji vya damu, au una ugonjwa wa selimundu

  • Dalili za ugonjwa wa ghafla kando na maumivu ya viungo

  • Uwezekano wa maambukizi ya zinaa

Mpigie daktari baada ya siku kadhaa ikiwa una maumivu kiasi ya viungo yasiyoisha yenyewe.

Je, nitarajie nini ninapokwenda kumwona daktari wangu?

Kabla ya kukupima, daktari wako atakuuliza kuhusu dalili zako na historia ya afya yako.

Daktari anaweza kufanya vipimo kama vile:

  • Vipimo vya majimaji ya kiungo—madaktari huchukua majimaji kutoka kwenye kiungo chako kwa kutumia sindano kisha wanapima majimaji hayo ili kutafuta dalili za maambukizi au jongo

  • Upimaji wa picha, kwa kawaida huwa eksirei, lakini wakati mwingine MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) au uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta)

  • Vipimo vya damu, kwa nadra

Madaktari wanatibu vipi maumivu ya viungo?

Madaktari watatibu kisababishaji cha maumivu yako. Kwa mfano, ikiwa umevunjika mfupa, madaktari wanaweza kuweka kiungo chako kwenye plasta. Ikiwa una maambukizi ya kiungo, watakupatia dawa za kuua bakteria na mara nyigi watafanya upasuaji ili kuondoa maambukizi.

Madaktari wanaweza pia kukutibu maumivu ya viungo kwa:

  • Dawa za kupunguza uvimbe zisizo za steroidi (NSAID) au asetaminofeni

  • Kitambaa au kombeo

  • Kuwekelea kitu chenye joto au baridi—wakati mwingine madaktari watakushauri ubadilishe kati ya kitu chenye joto na baridi

Baada ya maumivu yako ya kiungo kupungua, madaktari wakati mwingine hupendekeza tiba ya mazoezi. Tiba ya mazoezi huzuia na kutibu ukakamavu wa kiungo na kuimarisha nguvu za misuli iliyo karibu na kiungo.