Je, kichefuchefu na kutapika kupindukia wakati wa ujauzito ni nini?
Kichefuchefu na kutapika kupindukia wakati wa ujauzito (Hyperemesis gravidarum) ni hali ya kutapika sana unapokuwa mjamzito
Unatapika sana hadi unapoteza uzani na kukosa maji mwilini (huna maji ya kutosha au majimaji mwingine mwilini)
Kutapika kwingine katika ujauzito ni jambo la kawaida. Mara nyingi huitwa "ugonjwa wa asubuhi." Ikiwa una ugonjwa wa asubuhi, unajihisi vibaya lakini unaendelea kuongeza uzani na kunywa maji ya kutosha. Madaktari hawana uhakika kwa nini baadhi ya wanawake wanatapika sana.
Kichefuchefu na kutapika kupindukia wakati wa ujauzito ni tofauti na ugonjwa wa asubuhi kwa sababu ni kali sana
Utahitaji majimaji ya IV (yanayowekwa moja kwa moja kwenye mshipa wako wa damu) na kwa kawaida dawa za kukomesha kutapika
Kwa kawaida, kichefuchefu na kutapika kupindukia wakati wa ujauzito huisha kufikia wiki 16 hadi 18 za ujauzito
Ikiwa itahudumu kwa muda mrefu au ni kali sana, inaweza kusababisha matatizo kwa ini yako
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina kichefuchefu na kutapika kupindukia wakati wa ujauzito?
Madaktari watafanya vipimo vya damu na mkojo ili kujua kama una upungufu wa maji mwilini
Vilevile watafanya kipimo cha picha cha kutumia mawimbi ya sauti (kuchukua picha zinazosonga za sehemu za ndani ya uterasi yako)
Kipimo cha picha kinachotumia kutumia mawimbi ya sauti kinaweza kuwasaidia madaktari kujua ikiwa unatapika kwa sababu nyinginezo, kama vile kwa sababu una ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja
Je, madaktari hutibu kichefuchefu na kutapika kupindukia wakati wa ujauzito aje?
Utaenda hospitalini
Madaktari watakuwekea maji ya IV moja kwa moja kwenye mshipa wako wa damu
Kwa kawaida, utakaa hospitalini ili uweze kuongezewa maji zaidi ya IV na dawa za kusaidia kukomesha kutapika
Baada ya kuacha kutapika, utapata maji ya kukunywa na kiasi kidogo cha vyakula visivyo na mafuta ili ule
Ikiwa utaanza kutapika tena, mchakato huu unaanza tena
Kwa nadra, ikiwa unaendelea kutapika na kupoteza uzani, unaweza kulishwa kupitia mrija. Mrija hupitia pua yako na kushuka kooni hadi kwenye tumbo lako.
Ikiwa utaendelea kutapika na kupoteza uzani na kuwa na matatizo ya ini, unaweza kufikiria kusitisha ujauzito wako. Unaweza kuzungumza na daktari wako kuhusu chaguo hili.