Uvimbe wa Polimofiki wa Ujauzito

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2023

Je, uvimbe wa polimofiki wa ujauzito ni nini?

Uvimbe wa polimofiki wa ujauzito ni vipele vinavyowasha sana ambavyo hutokea tu wakati wewe ni mjamzito. Vipele:

  • Kwa kawaida huonekana katika wiki 2 hadi 3 za mwisho za ujauzito

  • Ina mabaka mekundu, yenye umbo lisilo la kawaida na yaliyofura kidogo, wakati mwingine ina malengelenge madogo katika sehemu ya katikati

  • Hutokea kwenye tumbo lako na kisha kuenea kwa mapaja yako, makalio, na wakati mwingine mikono

  • Kwa kawaida huisha muda mfupi baada ya kujifungua

  • Ni vya kawaida katika ujauzito wa kwanza—vipele hivyo kwa kawaida havitokei tena katika ujauzito wa siku za usoni

Unaweza kuwa na mamia ya mabaka yanayowasha. Mara nyingi ngozi iliyo karibu na mabaka huwa imepauka.

Je, vipele hivi vinasababishwa na nini?

Hakuna anayejua chanzo cha vipele hivi. Madaktari wanaweza hata kupata changamoto wakati wa kufanya utambuzi wa ugonjwa wa uhakika.

Je, madaktari hutibu vipi vipele hivi?

Madaktari watakuelekeza kupaka malai ya kotikosteroidi kwenye vipele vyako. Kwa nadra sana, ikiwa vipele vyako ni sugu, unaweza kumeza tembe ya kotikosteroidi, kama vile predinisone.