Matabaka mawili ya utando mwembamba, unaoitwa pleura, hufunika mapafu yako. Tando hizi mbili kwa kawaida hugusana. Lakini wakati mwingine nafasi kati ya utando, iitwayo pleura, hujaa hewa au majimaji.
Majimaji yaliyopo kwenye nafasi ya pleura huitwa kuvimba kwa pleura. Hewa iliyo kwenye nafasi ya pleura huitwa nimothoraksi.
Kuvimba kwa pleura ni nini?
Kuvimba kwa pleura ni mkusanyiko wa majimaji kwenye nafasi ya pleura.
Kuvimba kwa pleura kunaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali kama vile maambukizi, uvimbe au jeraha
Majimaji yanaweza kuwa chepechepe au yenye damu au usaha
Unaweza kupata shida ya kupumua na maumivu ya kifua, hasa unapovuta hewa nyingi kwenye mapafu au kukohoa
Madaktari wanaweza kuona kuvimba kwa pleura kwa eksirei au kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa kifua
Madaktari watatibu tatizo ambalo linasababisha kuvimba kwa pleura na wanaweza kutoa majimaji kwa kutumia sindano
Je, nini husababisha kuvimba kwa pleura?
Matatizo mbalimbali yanaweza kusababisha kuvimba kwa pleura:
Jeraha kwenye kifua chako, kama vile ubavu kuvunjika
Zipi ni dalili za kuvimba kwa pleura?
Ikiwa una tatizo la kuvimba kwa pleura, unaweza usiwe na dalili zozote, au unaweza kuwa:
Kuishiwa na pumzi
Maumivu ya kifua, hasa unapovuta hewa nyingi kwenye mapafu au kukohoa
Wakati mwingine, maumivu kwenye sehemu ya juu ya tumbo, shingo au bega lako
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina tatizo la kuvimba kwa pleura?
Ili kufahamu kama nina tatizo la kuvimba kwa pleura, madaktari watafanya:
Mara baada ya kugundua uwepo wa tatizo la kuvimba kwa pleura, madaktari wanaweza kufanya vipimo na taratibu zingine:
Kuchukua sampuli ya majimaji kwa kutumia sindano
Wakati mwingine, uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta)
Wakati mwingine, kuingiza bomba la kutazama kwenye kifua chako
Je, madaktari wanatibu vipi tatizo la kuvimba kwa pleura?
Madaktari watatibu tatizo ambalo linasababisha kuvimba kwa pleura. Kwa mfano, ikiwa una maambukizi ya mapafu, unaweza kupatiwa dawa za kuua bakteria.
Ikiwa kuna kiasi kidogo cha majimaji, madaktari wanaweza:
Kusubiri ili kuona kama majimaji yatajiondoa yenyewe.
Kama kuna kiasi kikubwa cha majimaji, au kama majimaji yanasababisha kupumua kwa shida, madaktari wanaweza:
Kutoa majimaji kwa kutumia sindano
Wanaweka sindano au bomba ndani kupitia upande wa kifua chako, katikati ya mbavu mbili. Iwapo majimaji yatajikusanya tena baada ya kuyaondoa, wakati mwingine wataacha bomba dogo kwenye kifua chako ili majimaji yaendelee kutoka.
Ikiwa majimaji hayo yalisababishwa na saratani, madaktari wanaweza kuweka dawa au kitu kingine ndani kupitia bomba (pleurodesis). Dawa husumbua pleura na kuzifanya zijikusanye pamoja na kutengeneza kovu hivyo majimaji hayawezi kukusanyika.