Ukinzani wa Arginine Vasopressini

(Kisukari cha maji mwilini cha Neffrogeniki)

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2024

Ukinzani wa arginine vasopressini ni nini?

Ukinzani wa arginine vasopressini (hapo awali ulijulikana kama kisukari cha maji mwilini cha neffrogeniki) ni tatizo la figo ambalo hukufanya kukojoa sana na kisha kukufanya uwe na kiu.

Kwa kawaida, figo zako huweka viwango sawa vya maji kwenye mwili wako ili uwe na kiasi sahihi cha maji (usawa wa maji). Lakini kwa ukinzani wa arginine vasopressini, mwili wako hupoteza maji mengi kupitia kukojoa.

  • Ukinzani wa Arginine vasopressini unaweza kuanza punde tu baada ya kuzaliwa, au unaweza kuupata baadaye

  • Unakojoa sana—galoni 1 hadi 6 (takribani lita 4 hadi 24) za mkojo kwa siku

  • Kuhisi kiu sana na kunywa maji kwa wingi kwa sababu unakojoa sana, unapata kiu na kunywa maji sana

  • Kukojoa na kunywa maji mengi huondoa usawa wa chumvi na madini (elektroliti) katika mwili wako.

  • Unaweza kuishiwa maji (kukosa maji mwilini)

  • Madaktari uhakikisha unakunywa maji ya kutosha na huli chumvi nyingi au protini

  • Wakati mwingine, dawa inaweza kusaidia

Ni nini husababisha ukinzani wa Arginine vasopressini?

Ukinzani wa arginine vasopressini hutokea pale figo zinapoacha kuitikia homoni inayoitwa vasopressini. Vasopressini hutoa ishara kwa figo ili zihifadhi maji na usikojoe sana. Iwapo figo zako zikiacha kuitikia vasopressini, utakojoa sana.

Visababishaji vya ukinzani wa Arginine Vasopressini vinajumuisha:

Dalili za ukinzani wa Arginine Vasopressini ni zipi?

Dalili za ukinzani wa Arginine Vasopressini vinajumuisha:

  • Kuhisi kiu sana

  • Kukojoa sana (kama galoni 6 [lita 24] kwa siku)

Katika aina moja ya ukinzani wa Arginine Vasopressini, dalili zinaweza kuanza punde tu baada ya kuzaliwa. Watoto wachanga hupoteza maji mengi mwilini na huwa na dalili kama vile:

  • Homa

  • Kutapika

  • Vifafa

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ukinzani wa arginine vasopressini?

Madaktari wanashuku ukinzani wa arginine vasopressini ikiwa unakunywa na kukojoa sana. Ili kuwa na uhakika, watafanya:

  • Vipimo vya damu

  • Vipimo vya mkojo

Wakati mwingine, madaktari hufanya kipimo cha kutokunywa maji.

Madaktari hutibu vipi ukinzani wa arginine vasopressini?

Ili kutibu ukinzani wa arginine vasopressini, madaktari watakuagiza:

  • Unywe maji mara tu unapohisi kiu—watoto wachanga, watoto, na watu wazima wenye ukinzani wa arginine vasopressini wanapaswa kupewa maji kila mara

  • Ule chakula ambacho kina kiasi kidogo cha chumvi na protini

  • Wakati mwignine, utumie dawa ambazo husaidia figo kufyonza tena sodiamu na maji ili usikojoe mara kwa mara