Upungufu wa Maji Mwilini kwa Watoto

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2023

Kila mtu anahitaji maji na kemikali fulani (elektroliti) ili kuwa mwenye afya. Kwa kawaida, unakunywa viowevu ili kukidhi mahitaji na kuwa mwenye kiu hukwambia kuwa unahitaji viowevu vingi. Lakini watoto na watoto wachanga zaidi hawawezi kukwambia kila wakati wanahitaji kiowevu, haswa wakati ni wagonjwa.

Upungufu wa maji mwilini mwa watoto ni nini?

Upungufu wa maji mwilini ni kutokuwa na maji ya kutosha mwilini mwako. Mara nyingi watoto huwa wenye kukosa maji mwilini ikiwa wanatapika au kuendesha (mara nyingi, kinyesi majimaji chepesi) na hawanywi maji ya kutosha ili kuisawazisha. Homa hufanya kokosa maji mwilini kuwe kubaya zaidi.

  • Kutapika na kuhara kunaweza kusababisha kukosa maji mwilini

  • Kupata maziwa kidogo sana wakati wa kunyonya inaweza kusababisha kukosa maji mwilini kwa watoto

  • Kukosa maji mwilini sana kunaweza kufanya watoto wahisi wakiwa wagonjwa na wakati mwingine wafariki

  • Mtoto anayekosa maji mwilini anahitaji viowevu na madini yanayoitwa elektroliti

  • Maziwa ya matiti na michanganyiko ya kuongeza maji mwilini kupitia kinywani (inauzwa kwenye maduka ya chakula na dawa) ina msawazisho mzuri wa maji na elektroliti

Soda, juisi na vinywaji vya spoti havina msawazisho mzuri wa maji na elektroliti.

Je, dalili za upungufu wa maji mwilini ni zipi?

Watoto watakuwa na dalili ya kile ambacho kinawafanya wakose maji mwilini, kama vile kutapika sana, kuhara au zote mbili. Kukosa maji mwilini husababisha dalili kama vile:

  • Kucheza na kuongea kidogo

  • Kuwa na hasira na kuudhika

  • Kulia bila kutoa machozi

  • Mdomo mkavu

  • Mashavu na macho yaliyoingia ndani

  • Kupunguza uzani ndani ya siku chache tu

  • Kukojoa chini ya mara 2 au 3 kwa siku

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa mtoto wako ana mojawapo ya ishara hizi za onyo:

  • Hawezi kukaa na viowevu mwilini

  • Hapitishi kiwango sawa cha mkojo au anatumia nepi chache zaidi

  • Analala tu hapo akionekana dhaifu na mchovu

Kukosa maji mwilini sana kunaweza kutishia maisha kusipotibiwa.

Je, madaktari wanatibu vipi kukosa maji mwilini kwa watoto?

Watoto ambao wanatapika au kuhara kidogo lakini hawakosi maji mwilini wanaweza kuendelea kunywa kile ambacho huwa wanakunywa. Unaweza kuwapea kiowevu kidogo cha ziada, kama vile mafundo kidogo ya supu wazi, soda wazi au mchanganyiko wa juisi nusu na maji nusu. Watoto wenye umri wa zaidi ya mwaka 1 wanaweza pia kupewa pepsiko.

Watoto wanaokosa maji mwilini wanahitaji kiowevu cha ziada kwa mchanganyiko mzuri wa maji na elektroliti. Maji tupu, maziwa, soda, juisi na vinywaji vya spoti havina msawazisho mzuri wa maji na elektroliti.

Viowevu vya kupatiana:

  • Maziwa ya matiti, ikiwa tayari unanyonyesha (maziwa ya matitit ina elektroliti na ndiyo kiowevu kizuri zaidi cha kunyonyesha watoto)

  • Mchanganyiko wa kuongeza maji mwilini kupitia kinywani (mchanganyiko wa maji na elektroliti) ambao unaweza kununua kama poda au kiowevu kwenye duka ya dawa au duka ya mboga na matunda—baada ya mtoto wako kupitisha saa 12 bila kutapika, kisha unaweza kumpatia fomula

Jinsi ya kumpea viowevu:

  • IIkiwa mtoto wako anakosa maji mwilini kutokana na kutapika, mpatie mafundo kidogo ya viowevu kila dakika 10, kisha viwango vingi mara nyingi ikiwa mtoto wako ana uwezo wa kunywa bila kutapika

  • Ikiwa mtoto wako anakosa maji mwilini kutokana na kuhara, mpatie kiowevu zaidi, mara chache—unaweza pia kumpatia maziwa ya kopo au vyakula vya kawaida ikiwa mtoto wako hatapiki

Ikiwa mtoto wako ana upungufu mkubwa wa maji mwilini au ni mgonjwa sana na hawezi kunywa kiasi cha kutosha, madaktari:

  • Watampea viowevu kupitia kwenye mshipa (kwa IV)

  • Watampea viowevu kupitia kwenye mfereji mwembamba wa plastiki ambao unaingia kwenye pua la mtoto, kuelekea kwenye koo na kwenye tumbo