Kushindwa kustawi ni nini?
Kushindwa kustawi ni wakati mtoto mchanga au mtoto hakui au kuongezeka uzani kama inavyotarajiwa. Watoto wachanga na watoto wanaoshindwa kustawi wana uzani wa chini kupita kiasi, wanapunguza uzani au kuacha kukua kwa kiwango chao kinachotarajiwa.
Kushindwa kustawi kunaweza kusababisha matatizo ya muda mrefu kwa masomo, tabia na ukuaji, haswa ikifanyika wakati wa mwaka wa kwanza wa maisha ya mtoto.
Ni nini husababisha kushindwa kustawi?
Kushindwa kustawi kwa kawaida hufanyika kwa sababu watoto hawapati chakula cha kutosha. Au chakula wanachopata hakina protini, mafuta, vitamini na madini (virutubishi) vya kutosha wanavyohitaji kwa ajili ya kukua wakiwa na afya. Hii inaweza kufanyika kwa sababu ya matatizo kwenye familia au tatizo la kiafya ambalo mtoto ako nalo.
Matatizo ya familia:
Kuzembea au dhuluma
Umaskini
Wazazi ambao wako na msongo wa mawazo, wasiwasi au wana matatizo ya akili
Wazazi kutoelewa jinsi ya kuchanganya fomula au kulisha watoto wachanga
Hali tatanishi za familia, kama vile kuwa katika hatari ya kupoteza makazi
Matatizo ya kiafya:
Matatizo katika kumeza au kukula vyakula bila kutapika
Matatizo katika kufyonza virutubishi kutoka kwenye vyakula (hali ya kushindwa kunyonya virutubishi)
Ugonjwa wa ini, figo au moyo
Je, dalili za kushindwa kustawi ni zipi?
Watoto walioshindwa kustawi wanaweza:
Kukua polepole kuliko wanavyopaswa
Punguza uzani
Kunyamaza na kutokuwa makini
Mwaka wa kwanza wa maisha ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa ubongo. Ikiwa kushindwa kustawi wakati huu hakutatibiwa, wataoto baadaye wanaweza kupata:
Matatizo ya masomo shuleni
Matatizo ya hisia na tabia
Je, madaktari wanawezaje kujua kama mtoto wangu hastawi?
Daktari wa mtoto wako ataweka kumbukumbu ya urefu na uani katika kila ziara ya kumwona daktari. Watalinganisha uzani na urefu wa mtoto wako kwa:
Urefu na uzani uliorekodiwa kwenye ziara za daktari za awali
Urefu na uzani wa kawaida kwa watoto wa umri huo
Wanashuku kushindwa kustawi ikiwa mtoto wako hakui kama inavyotarajiwa. Madaktari wanachunguza mtoto wako na kuuliza kuhusu tabia za kula na dalili za mtoto wako.
Ikiwa mtoto wako anapata chakula cha kutosha, madaktari wanafanya vipimo ili kujua kama tatizo la kiafya linasababisha kushindwa kustawi. Kwa kawaida, madaktari hufanya yafuatayo:
Vipimo vya mkojo na kinyesi
Vipimo vya damu
Eksirei
Je, madaktari hutibu vipi kushindwa kustawi?
Ili kutibu kushindwa kustawi, madaktari:
Watatibu tatizo lolote la kiafya ambalo linalisababisha
Watakwambia umpatie mtoto wako vyakula venye kuchochea afya vya kutosha vilivyo na kalori za kutosha ili akue na kuongeza uzani
Watatengeneza ratiba ya malisho kwa ajili yako kufuata na kukusaidia kupata rasilimali ili uweze kununua vyakula vya kutosha
Kwa kushindwa kustawi kali, watatunza mtoto wako hospitalini
Watoto ambao kushindwa kustawi kwao ni kwa sababu ya kuzembea au dhuluma wanaweza kuhitaji kuwekwa kwenye makazi ya utunzaji.