Kuota meno ni nini?
Kuota meno ni kipindi ambacho meno ya watoto huanza kutokea kupitia fizi zao.
Watoto wengi hupata jino lao la kwanza wanapokuwa na umri wa miezi 6
Kufikia umri wa miaka 3, watoto wengi wana meno yao yote 20
Watoto wanaoota meno mara nyingi huwa na fujo, lakini licha ya kile watu wengi hufikiri, kuota meno hakusababishi homa
Mpigie simu daktari wako ikiwa mtoto wako ana fujo sana au ana homa ya juu zaidi ya 100° F (37.8° C)—mtoto wako labda ni mgonjwa, si tu kuota meno.
Dalili za kuota meno ni zipi?
Mtoto anayeota meno:
Hulia na kuwa na fujo kuliko kawaida
Halali vizuri
Anakula kidogo kuliko kawaida
Hudondokwa na mate
Ana fizi nyekundu
Hutafuna vitu
Ninawezaje kutibu dalili za kuota meno?
Ili kumsaidia mtoto wako kujisikia vizuri zaidi:
Mpe mtoto wako kitu salama cha kutafuna, kama vile kifaa imara cha kuchanua meno au pete ya kuchanua yenye jeli baridi
Sugua fizi za mtoto wako kwa kidole chako au kwa kutumia barafu
Mpe mtoto wako dawa ya maumivu, kama vile acetaminophen au ibuprofen, ikiwa mtoto wako hana raha
Usitumie jeli za kuotesha meno—hazisaidii sana, na zinaweza kuwa na benzocaine, ambayo husababisha matatizo makubwa kwa baadhi ya watoto