Matatizo ya kula

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2023

Matatizo ya kula ni nini?

Matatizo ya kula kwa watoto wachanga yanajumuisha matatizo kula chakula au kuiweka tumboni bila kutapika au kupata kiwango kisichostahili cha chakula (aidha kidogo sana au kingi sana).

Matatizo ya kula ya kawaida yanajumuisha:

  • Kucheua

  • Kutapika

  • Kulisha kupita kiasi

  • Kula kidogo kupita kiasi

Matatizo ya kula yanatokea sana na ni ya kawaida kwa watoto wadogo, lakini wakati mwingine mtoto wako mchanga au mtoto mdogo anaweza kuhitaji kuonekana na daktari au kutibiwa hospitalini.

Je, kucheua ni nini?

Kucheua ni wakati maziwa ya kopo au maziwa ya mama ambayo mtoto wako amemeza hivi punde yanaporudi na kutiririka nje ya mdomo au pua ya mtoto. Mtiririko huwa wa polepole, si wa kulazimishwa kama kutapika.

Kucheua ni hali ya kawaida kwa watoto wachanga.

  • Karibu watoto wote wachanga hutema na karibu kila wakati huacha wakifika umri wa miezi 12

  • Kucheua hutokea kwa sababu watoto wachanga hawawezi kuketi baada ya kula na kwa sababu vali ambazo huzuia chakula tumboni ni dhaifu

  • Kucheua ambako kunasababisha maumivu kwa mtoto wako, hakukomi, au kuzuia mtoto wako kula au kuongezeka uzani kunajulikana kama kupwa kwa asidi (refluksi gastroesofajia)—mtoto wako anaweza kuhitaji dawa ili kuitibu

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa mtoto wako anatema kitu chenye rangi ya kijani au damu au kinafanya mtoto wako mchanga akohoe au anyongwe.

Ninawezaje kuzuia kucheua?

Ili kuzuia mtoto wako mchanga kucheua:

  • Walishe watoto wachanga kabla wakuwe njaa zaidi

  • Wapige mbweu baada ya kila dakika 4 hadi 5 huku ukiwalisha

  • Washikilie kama wamesimama wakati wa kula na baada ya kula

  • Hakikisha kuwa chuchu la chupa linaachilia tu matone machache kwa shinikizo au wakati imeinamishwa

Kutapika ni nini?

Kutapika ni chakula kilicho tumboni kulamishwa kirudi juu kwenye koo ya mtoto mchanga au mtoto. Kutapika kwingi kwa watoto wachanga na watoto kunasababishwa na virusi vya tumbo.

  • Kutapika ni ishara ya ugonjwa au tatizo—watoto wachanga kati ya wiki 2 na miezi 4 hutapika kwa nadra bila sababu

  • Kutapika kwingi huisha kwenyewe bila matibabu

  • Ikiwa mtoto wako anatapika, mpatie viwango kidogo vya viowevu mara kwa mara

Kutapika sana kunaweza kusababisha kukosa maji mwilini, ambayo si kuwa na maji ya kutosha kwenye mwili wako.

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa mtoto wako anatapika na ana yoyote ya ishara hizi za onyo:

  • Maumivu makali ya tumbo

  • Hawezi kunywa viowevu bila kutapika

  • Homa kali

  • Anahisi mdhaifu na mchovu mwili wao wote

  • Hutapika kwa zaidi ya saa 12

  • Anatapika vitu vyenye rangi ya kijani au damu

  • Hakojoi kwa saa 8

Kukula kupita kiasi ni nini?

Kukula kupita kiasi ni kupatiana chakula kingi kuliko chenye mtoto anahitaji ili kuwa mwenye afya na akue. Hii inaweza kusababisha watoto kutapika, kuhara (kinyesi chenye majimaji, chepesi mara nyingi), au anakuwa na uzani mkubwa kupita kiasi au mnene sana.

Ili kuzuia kula zaidi kupita kiasi:

  • Usimlishe mtoto wako kwa sababu tu mtoto wako analia-angalia ikiwa kuna sababu nyingine ya kulia

  • Usimpe mtoto wako chupa kama shughuli au kumruhusu mtoto awe na chupa muda wote

  • Usimpe mtoto zawadi ya chakula kwa sababu ya tabia njema

  • Usimfanye mwanao amalize chakula akiwa hahisi njaa

Kutokula chakula cha kutosha ni nini?

Kutokula chakula cha kutosha ni kutowapa watoto wako chakula cha kutosha ili wawe na afya na kuendelea kukua. Kunatokea kawaida ikiwa mtoto ni mkaidi sana kula au ana matatizo ya kunyonya au kumeza.

Mtoto ambaye hajalishwa vya kutosha anaweza kuwa na tatizo la kushindwa kukua.

  • Ili kuhakikisha mtoto wako anapata kiasi sahihi cha lishe, siku zote changanya mchanganyiko wa maziwa ya fomula kulingana na maelekezo

  • Mashirika ya kijamii, kama vile mpango wa Wanawake, Vichanga na Watoto (WIC), yanaweza kukusaidia kulipia chakula na maziwa ya fomyula na kujifunza njia bora zaidi za kuchanganya maziwa na kumlisha mtoto wako

  • Ikiwa mtoto wako ana uzani wa chini sana, madaktari wanaweza kumtunza mtoto wako hospitalini ili kuhakikisha kwamba mtoto wako anaongezeka uzito