Ugonjwa wa Refluksi Gastroesofajia kwa Watoto

(Ugonjwa wa Refluksi Gastroesofajia [GERD])

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023

Je, ugonjwa wa Refluksi Gastroesofajia (GERD) ni nini?

GERD (asidi kurudi nyuma) ni ugonjwa unaosababishwa na matumbo na asidi ya tumbo kurudi nyuma kwenye umio lako. Umio ni mrija unaounganisha koo na tumbo lako. GERD ni ya kawaida pia kwa watu wazima.

  • Asidi ya tumbo inaweza kuwasha na wakati mwingine kuharibu umio

  • Wakati mwingine asidi ya tumbo inaingia kwenye koo ya mtoto wako na kuelekea chini ya bomba la upepo

  • Karibu watoto wote wachanga hupata hali ya kupwa na hucheua wakati mwingine

  • Watoto wachanga walio na GERD wanaweza kutapika, wawe na matatizo ya kula au kupumua au kuwa mwepesi

  • Watoto wana maumivu ya kifua au tumbo au kiungulia

  • Madaktari hufanya mabadiliko kwa lishe ya mtoto wako na jinsi unavyowalisha na kukuandikia dawa ya kuzuia asidi

  • Watoto wachanga wengi wanakuza zaidi refluksi kwa takriban miezi 18

Ni nini husababisha refluksi kwa watoto?

Mzunguko wa misuli huweka mwisho wa umio ukiwa umefungwa. GERD hufanyika wakati misuli hio haifungi kabisa umio na huacha vitu vilivyo kwenye tumbo vitiririke kwenye umio.

Husababishwa na:

  • Misuli hafifu au isiyokua vizuri kwenye sehemu ya chini ya umio

  • Shinikioz la juu zaidi kwenye tumbo ya mtoto wako, kama vile kutokana na kula kupita kiasi au magonjwa ya mapafu ya muda mrefu

Refluksi ina uwezekano mkubwa wakati watoto:

  • Wanalala kwa tumbo wakati au baada ya kula

  • Wana mzio wa chakula au maziwa

  • Wako karibu na moshi wa sigara

  • Wanapata kafeini au nikotini kutoka kwenye maziwa ya matiti ya wazazi wao

Je, dalili za refluksi kwa watoto ni zipi?

Kwa kawaida dalili za refluksi zinaanzia punde tu baada ya kuzaliwa na ni kali zana katika umri wa miezi 6 au 7. Kisha dalili huisha polepole na kwa kawaida zinaisha kwa takriban miezi 18.

Kwa watoto wachanga, dalili za kawaida zaidi ni:

  • Kutapika

  • Kucheua sana

Waototo wachanga wakitapika sana, huenda wasiongeze uzani kama inavyotakiwa. Asidi ikiingia kwenye koo au bomba lao la upepo, watoto wachanga wanaweza kukohoa na kuforota.

Kwa watoto, dalili za kawaida zaidi ni:

  • Maumivu ya kifua

  • Maumivu ya tumbo

  • Wakati mwingine kiungulia (maumivu yenye mwasho kwenye kifua)

Kwa balehe, dalili ya kawaida zaidi ni:

  • Kiungulia

Madaktari wanawezaje kujua kama mtoto wangu ana refluksi?

Mara nyingi madaktari hutegemea utambuzi wa ugonjwa wa refluksi kwenye dalili za mtoto wako. Ikiwa mtoto wako ana dalili kali, madaktari wanaweza pia kufanya vipimo kama vile:

  • Uchunguzi wa kutumia bari (eksirei ambayo hutumia bari inayomezwa ili kusaidia madaktari kuona kila kitu katika njia ya mmeng'enyo wa chakula)

Madaktari wanatibu GERD aje kwa watoto?

Matibabu ya GERD yanategemea umri na dalili za mtoto wako.

Kwa mtoto, madaktari wanaweza kukwambia:

  • Uongeze uzito wa fomula ya mtoto kwa kutumia nafaka ya mchele

  • Umshikilie mtoto kama ameinuka kiasi ili kula

  • Umpige mbweu mtoto mara nyingi

  • Utumie fomula maalum ya mtoto ambayo haisababishi mizio (fomula ya hypoallergenic)

  • Wakati mwingine umpatie mtoto wako dawa ya kutoa asidi ambayo inatuliza asidi ya tumbo au dawa ya kukomesha asidi

  • Wakati mwingine uinue kichwa cha hori takriban inchi 6 (sentimita 15)

Kwa mtoto mkubwa, daktari atasema mtoto wako:

  • Asile saa 2 au 3 kabla ya wakati wa kulala

  • Asinywe vinywaji visivyo na viputo (vyenye kaboni) kama vile vinywaji visivyo vya pombe au vinywaji vya kafeini kama vile kahawa

  • Asitumie dawa fulani

  • Asile vyakula fulani kama vile chokoleti au vyakula vyenye mafuta au kula kupita kiasi

Watoto wote wanapaswa kuwekwa mbali na kafeini na moshi wa sigara kwa vile hizi zinaweza kufanya GERD iwe mbaya zaidi.