Je, kuvimba tumbo na utumbo ni nini?
Gastroenteraitisi ni maambukizi ya njia ya mmeng'enyo wa chakula (pia inaitwa njia ya mfumo wa utumbo au njia ya GI) ambayo husababisha kutapika, kuhara au vyote. Tumbo na utumbo ni viungo vikuu vya njia ya mmeng'enyo wa chakula. Wakati mwingine watu hufanya makosa ya kuita gastroenteraitisi "homa ya tumbo." Lakini si "homa" na haihusishwi kwa vyovyote na mafua (homaya mafua).
Gastroenteraitisi ni tatizo la GI la kawaida zaidi kwa watoto
Watoto wenye gastroenteraitisi hutapika na kuhara, kuvimba tumbo na homa
Kutapika na kuendesha, haswa zinapotokea pamoja, zinaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini (kutokuwa na maji ya kutosha au viowevu vingine kwenye mwili), ambayo inaweza kusababisha matatizo makubwa
Unaweza kusaidia kuzuia gastroenteraitisi kwa kumpeleka mtoto apewe chanjo na kwa kufanya watoto wanawe mikono yao mara nyingi
Gastroenteraitisi inatibiwa kwa kubadilisha maji na elektroliti, kwa kawaida kwa kunywa kiowevu maalum kilichotengenezewa kwa ajli ya watoto walio na gastroenteraitisi
Watoto ambao hawawezi kuweka viowevu wanapaswa kuona daktari—wanaweza kuhitaji kupata viowevu moja kwa moja kwenye mshipa (IV)
Je, nini husababisha kuvimba tumbo na utumbo?
Gastroenteraitisi mara nyingi inasababishwa na virusi (kama vile virusi vya rota). Inaweza pia kusababishwa na bakteria au vimelea.
Watoto wanaweza kupata gastroenteraitisi kutokana na:
Kugusa watoto walioathiriwa au wanasesere na kisha kuweka vidole vyao kwenye mdomo wao
Kuwa karibu na mtoto mgonjwa ambaye anapiga chafya au kutema mate
Kukula vyakula au kunywa kiowevu ambacho kina bakteria ndani yake (ni inaitwa sumu ya chakula)
Kunywa mazima au juisi isiyopashwa moto (isiyopashwa moto inamaanisha kuwa haikupashwa moto ili kuua vijidudu)
Kugusa vitambaazi, nyuni, vyura au salamander ambazo zinabeba bakteria
Kula mimea au dawa fulani
Kumeza maji yenye maambukizi kutoka kwenye madimbwi ya kuogelea, bustani za maji au mito
Je, dalili za kuvimba tumbo na utumbo ni zipi?
Dalili zinajumuisha:
Kutapika
Kuharisha
Kukakamaa kwa tumbo
Kutohisi njaa
Wakati mwingine, aina fulani za gastroenteraitisi zinasababisha kuhara damu. Hii ni mbaya zaidi na unapaswa kupeleka mtoto wako kwa daktari mara moja.
Matatizo ya gastroenteraitisi ni yapi?
Tatizo kuu ni:
Upungufu wa maji mwilini
Upungufu wa viowevu ni maji au viowevu vingine kidogo zaidi mwilini. Hii inaweza kuwa hatari. Watoto wachanga wana uwezekano mkubwa wa kukosa maji mwilini kwa sababu ni wadogo sana.
Mtoto wako anakosa maji mwilini na anahitaji kuona daktari mara moja ikiwa mtoto wako:
Ana sehemu nyororo iliyoingia ndani kwenye sehemu ya juu ya kichwa (watoto wote wana sehemu nyororo, lakini haipaswi kuwa imeingia ndani)
Ana macho yaliyoingia ndani
Kuwa na mdomo mkavu
Hana machozi anapolia
Hakojoi sana
Hana umakini sana na ana nguvu kiasi
Mtoto wako anakosa maji mwilini na anahitaji kumwona daktari mara moja ikiwa mtoto wako:
Hakojoi sana na hajakojoa kwa saa 6 au zaidi
Ni mwepesi na mvivu
Kuwa na mdomo mkavu
Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana gastroenteraitisi?
Dalili za mtoto wako na uchunguzi wa kimwili husaidia madaktari kujua kama mtoto wako ana gastroenteraitisi. Kwa kawaida hakuna vipimo vya damu au vipimo vya kinyesi vinahitajika. Wakati mwingine daktari wako anahitaji kujua ni maambukizi ya aina gani yalisababisha gastroenteraitisi na atapitisha pamba kwenye uharo ili kufanya kipimo.
Je, madaktari hutibu vipi kuvimba tumbo na utumbo?
Kwa watoto wachanga, madaktari hutibu gastroenteraitisi kwa kuwafanya:
Waendelee kunyonyesha au kunywa maziwa ya fomula
Wakunywe majimaji maalum ya kurejesha maji mwilini (majimaji ya elektroliti ya kunywa kwa mdomo—poda au viowevu zinauzwa kwenye famasia na maduka ya kuuza mboga na matunda)
Kwa watoto wakubwa, ushauri wa daktari ni:
Kufanya mtoto wako akunywe kiowevu, kama vile majimaji ya elektroliti ya kunywa kwa mdomo kwenye siku ya kwanza ya ugonjwa—vijana wanapaswa kunywa kinywaji cha spoti badala ya soda au juisi, lakini majimaji ya elektroliti ya kunywa kwa mdomo yanapendelewa.
Ikiwa mtoto wako anatapika, mpatie mafundo kidogo ya kiowevu kila dakika 10 au 15—ikiwa mtoto wako hatapiki, mpatie kiowevu kingi kiasi hatua kwa hatua
Katika kipindi cha saa 24, mtoto wako anapaswa kunywa angalau aunsi 1½ ya kiowevu kwa kila pauni ya uzani wa mwili
Ikiwa mtoto wako anaharisha, mpatie kiowevu zaidi kuliko kawaida
Mfanye mtoto wako akule lishe bora ukiwezekana—vyakula maalum havihitajiki
Ikiwa mtoto wako anaharisha, mpatie bidhaa chache za maziwa (kama vile maziwa au siagi)
Daktari wa mtoto wako anaweza kukupea:
Viowevu kwenye mshipa (IV) ikiwa mtoto wako anakosa maji mwilini
Dawa ili kuzuia kutapika au ili kusaidia kupunguza kasi ya kuharisha
Dawa za kuua bakteria ikiwa kisababishaji ni aina fulani ya bakteria
Dawa za kuua vimelea ikiwa kisababishaji ni kimelea
Je, ninaweza kuzuia vipikuvimba tumbo na utumbo?
Ili kusaidia kuzuia gastroenteraitisi:
Hakikisha kuwa mtoto wako anapata chanjo ya rotavirus, ambayo ni mojawapo ya chanjo msingi
Kufanya watoto waoshe mikono yao mara kwa mara
Hifadhi vyakula vizuri (kuweka vyakula baridi vikiwa baridi na vyakula moto vikiwa moto), na usiwache mtoto wako ale vyakula ambavyo ambacho hakijafunikiwa kwa zaidi ya saa moja
Kuweka maeneo ya kubadilishia nepi yakiwa safi (na kuweka dawa ya kuua vimelea mara kwa mara kwa majimaji ya kitoa rangi kikombe ¼ katika galoni 1 ya maji)
Kunyonyesha
Usiwaruhusu watoto au watoto wachanga walio na mifumo hafifu ya kingamwili waguse watambaazi, nyuni au amfibia
Mfunze mtoto wako kuepuka kumeza maji anapoogelea
Ili kusaidia kuzuia kuenea kwa gastroenteraitisi:
Mtoto aliye na kinyesi chepesi (kuharisha) anapaswa kukaa nyumbani kutoka shuleni au utunzaji wa mchana na hapaswi kuogelea kwenye madimbwi ya kuogelea ya umma au maeneo mengine ya kuogelea ya umma
Angalia nepi ya mtoto wako mara nyingi na uibadilishe mbali na madimbwi ya kuogelea ya umma na maeneo ya kuogelea