Maambukizi ni nini?
Maambukizi ni pale ambapo vijidudu (viini vya maradhi) vinapovamia sehemu ya mwili wako na kukufanya uugue.
Vijidudu ni nini?
Vijidudu ni viumbe vidogo ambavyo ni vidogo sana haviwezi kuonekana bila kutumia hadubini. Kuna aina nyingi tofauti za vijidudu, ikiwa ni pamoja na:
Bakteria, kama vile E. coli
Virusi kama vile rhinovirus, ambavyo vinasababisha mafua ya kawaida
Fungi, kama vile fangasi, ambayo husababisha maambukizi ya fangasi
Vimelea, kama vile chawa
Istilahi 'kiini' hurejelea aina mbalimbali za vijidudu ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa.
Vijidudu vinatoka wapi?
Vijidudu vipo karibu kila mahali. Kuna maelfu ya aina mbalimbali. Wengine wanaishi kwenye ngozi yako au ndani ya kinywa chako, kwenye utumbo na sehemu za siri (hasa uke). Vijidudu wengine wanaishi kwenye ardhi au kwenye maji na wanaweza kuingia kwenye mwili wako.
Je, vijidudu wote wanafanya watu waumwe?
Vijidudu wengi hawasababishi maambukizi. Wengine hata wanasaidia. Vijidudu wengi wanaoishi kwenye ngozi yako au ndani ya mwili wako ni wa kawaida na hawakudhuru. Hawa huitwa vijidudu wako wakaaji.
Vijidudu wengine kwa kawaida hawaishi ndani au juu ya mwili wako na wanaweza kukufanya uugue. Mifano hujumuisha virusi vya hepatitis au virusi vya ukimwi (VVU).
Watu wanapataje maambukizi?
Maambukizi yanasababishwa na vijidudu wenye madhara wanaoingia kwenye mwili wako. Wanaweza kuingia kwenye mwili wako kupitia:
Kwenye pua au kinywa chako
Ngozi yako kutokana na kukatwa, mikwaruzo au kung'atwa
Kufanya ngono na mwenzi aliyeambukizwa
Vijidudu vinaweza kuingia kwenye kinywa chako ikiwa unakula au kunywa kitu kilicho na vijidudu ndani yake. Wanaweza pia kuingia kwenye pua au kinywa chako ikiwa utagusa kitu chenye maambukizi kisha uguse pua au kinywa chako. Baadhi ya vijidudu (kwa kawaida virusi) huvutwa na matone ya kupumua ambayo hutolewa wakati mtu aliye karibu naye anapokohoa, kupiga chafya, kuimba, kufanya mazoezi, au kuzungumza.
Wanapoingia kwenye mwili wako, vijidudu wenye madhara wanazaliana na kukufanya uumwe.
Wakati mwingine vijidudu wa kawaida kwenye mwili wako wanaingia katika sehemu isiyo sahihi. Kwa mfano, bakteria wa kawaida kwenye utumbo wako wanaweza kusababisha maambukizi ikiwa wataingia kwenye kibofu cha mkojo au kwenye mtiririko wa damu.
Je, mwili wangu hujikinga vipi dhidi ya maambukizi?
Mwili wako una njia nyingi za kujikinga dhidi ya maambukizi:
Ngozi yako inawazuia vijidudu wasiingie ndani
Ute kwenye pua lako, koo, macho na uke na utumbo unasafisha vijidudu na una dutu ambazo zinaweza kuviua
Mfumo wako wa kingamwili unashambulia vijidudu ndani ya mwili wako
Homa (joto la mwili la juu) husaidia kuua vijidudu
Mfumo wako wa kingamwilini unatumia seli nyeupe za damu kutambua viini hatari vya maradhi. Baadhi ya seli nyeupe za damu zinaua vijidudu moja kwa moja. Wengine wanatengeneza dutu zinzoitwa kingamwili zinazoua vijidudu.
Ni nani aliye katika hatari ya juu ya maambukizi?
Watoto wachanga na watu wazee sana wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi kwa sababu ulinzi wa mwili wao si thabiti sana.
Vitu vingine vinavyoongeza hatari yako ya maambukizi hujumuisha:
Magonjwa yanayodhoofisha mfumo wako wa kingamaradhi, kama vile UKIMWI, saratani au kisukari
Dawa zinazoingilia mfumo wako wa kingamwili, kama vile tibakemikali kwa ajili ya saratani au kotikosteroidi
Vifaa vya matibabu kwenye mwili wako, kama vile IV, bomba za kutoa mkojo (katheta), bomba za kupumulia kwenye koo la hewa au maungio bandia
Tiba ya Mionzi ya Saratani
Dalili za maambukizi ni zipi?
Dalili zinategemea:
Ambapo maambukizi iko kwenye mwili wako
Aina gani ya kijidudu iliyosababisha maambukizi yako
Iwe ni sehemu moja tu au sehemu kubwa ya mwili wako imeathiriwa
Kuambukizwa katika sehemu moja tu ya mwili wako husababisha maumivu na dalili za kawaida. Kwa mfano, maambukizi ya mapafu (Nimonia) yanaweza kusababisha maumivu ya kifua na kikohozi. Maambukizi kwenye ubongo husababisha kichwa kuuma. Maambukizi chini ya ngozi yako (majipu) yanaweza kuvimba, kubadilika kuwa mekundu na yenye maumivu.
Maambukizi yanayoathiri sehemu kubwa ya mwili wako yanaweza kusababisha dalili nyingi tofauti. Baadhi ya dalili kuu za jumla hujumuisha:
Kuhisi udhaifu na uchovu
Kukosa hamu ya kula
Maumivu kila upande
Ikiwa una maambukizi ambayo hayajatibiwa kwa muda mrefu, unaweza kupungua uzani.
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina maambukizi?
Madaktari wanashuku kuwa una maambukizi kulingana na dalili ulizo nazo. Kwa kawaida hawafanyi vipimo kwa ajili ya maambukizi ya kawaida, kama vile mafua na maambukizi ya ngozi. Kwa maambukizi mengine, madaktari mara nyingi wanatuma sampuli kwenye maabara ili kupima kuona kama kuna vijidudu. Kulingana na mahali ambapo maambukizi yanaonekana, huenda daktari akatuma sampuli ya:
Damu
Mkojo
Kikohozi (kamasi unayokohoa)
Sampuli kutoka kwenye koo, uume, au uke
Madaktari wanatibu vipi maambukizi?
Mwili wako unaweza kupambana na maambukizi wenyewe.
Kwa maambukizi mengine, madaktari watakutibu kwa dawa ya kuua vijidudu. dawa za kuua bakteria, kama vile Penisilini, ni dawa zinazoua bakteria.
Ikiwa una maambukizi makali, unapaswa kwenda hospitalini.
Ninawezaje kuzuia maambukizi?
Ili kuzuia maambukizi:
Nawa mikono yako mara kwa mara, haswa ikiwa unashika chakula au unaingiliana sana na watu
Pata chanjo ambazo daktari wako anasema unazihitaji