Homa kwa watu wazima

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2024

Je, homa ni nini?

Homa ni hali joto ya mwili iliyo juu zaidi ya 100 ° F (37.8 ° C). Homa si tu kujihisi joto au kutoka jasho. Ili iwe homa, hali joto ya mwili wako lazima iwe juu, kama inavyopimwa na themomita.

Halijoto ya kawaida ya mwili haifanani kwa kila mtu, lakini kwa kawaida inakuwa kati ya 98.6° F (37° C). Hali joto ya mwili ya kawaida inaweza kuwa hadi digrii 1 juu au chini ya hii kwa baadhi ya watu.

  • Homa nyingi kwa watu wenye afya husababishwa na maambukizi yatokanayo na virusi na kwa kawaida huondoka yenyewe ndani ya siku kadhaa

  • Unapokuwa na homa, dalili zako mara nyingi huwa zinatokana na kile kinachosababisha homa, na si homa yenyewe.

  • Homa yenyewe haiwezi ikakudhuru isipokuwa kama itapanda juu zaidi ya 106° F (41.1° C)

  • Madaktari wanajaribu kutafuta kujua nini kinachosababisha homa kwa kufanya uchunguzi wa kimwili na wakati mwingine kuchukua vipimo

  • Dawa kama vile ibuprofen au acetaminophen zinaweza kusaidia kushusha homa yako ikiwa inakufanya usijisikie vizuri

Nini kinasababisha homa kwa watu wazima?

Matatizo mengi yanaweza kusababisha homa.

Sababu zinazojulikana ni pamoja na:

Mara chache zaidi, homa inaweza kusababishwa na:

Kukiwa na magonjwa ya mwako na saratani, wa kawaida homa inadumu kwa muda mrefu. Homa huenda ikaendelea kuwepo muda wote au ikaja na kuondoka.

Kwa watu wenye umri mkubwa, sababu ya homa kwa kawaida ni maambukizi ya bakteria, mara nyingi kwenye mapafu, njia ya mkojo au tishu nyinginezo laini. Hata hivyo, maambukizi hayasababishi homa kila wakati kwa watu wenye umri mkubwa.

Homa ya chanzo kisichojulikana

Homa ya chanzo kisichojulikana (FUO) ni homa ambayo:

  • Ina hali joto la 101 ° F (38,3 ° C).

  • Inadumu kwa wiki kadhaa

  • Haina sababu dhahiri ambayo inaweza kugunduliwa na madaktari

Madaktari kwa kawaida wanachukua vipimo vingi, ikiwa ni pamoja na vipimo vya damu na mkojo na vipimo vya picha ili kuangalia maambukizi yasiyo ya kawaida au saratani. Ikiwa matokeo ya vipimo hivi hayaonyeshi kitu, madakatri huenda wakahitaji kupima sampuli ya tishu (uchukuaji wa kipande cha tishu kwa ajili ya uchunguzi) kutoka kwenye ini lako, uboho au eneo jingine ambalo linaweza kuwa na maambukizi.

Je, zipi ni dalili za homa kwa watu wazima?

Homa ni dalili ya ugonjwa. Kwa kawaida homa yenyewe haisababishi dalili nyingi isipokuwa:

  • Homa inapoanza unaweza kutetemeka mwili wote na meno kugongana kama upo nje kwenye baridi kali (huitwa "mzizimo")

  • Ikiwa una homa kali, ngozi yako itakuwa ya moto ikiguswa

  • Homa inapoondoka ("inapovunjika") unaweza kutokwa jasho jingi.

Huenda pia ukawa na dalili za kitu kilichosababisha homa yako. Kwa mfano, ikiwa homa yako ilisababishwa na maambukizi ya kifua, unaweza kukohoa.

Ni wakati gani ninapaswa kumwonda daktari kuhusu homa?

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa una homa na yoyote kati ya ishara hizi za onyo:

  • Kubadilika katika uwezo wa kufikiri, kama vile mkanganyiko

  • Maumivu ya kichwa, shingo iliyokaza, au vyote

  • Kipele

  • Kuhisi kuzimia au kizunguzungu

  • Mapigo ya moyo ya haraka

  • Kuishiwa pumzi au kupumua kwa haraka

  • Hali joto la juu zaidi ya 104° F (40° C) au chini ya 95° F (35° C)

  • Safari ya hivi karibuni kwenda kwenye maeneo ambapo ugonjwa mbaya wa kuambukiza, kama vile malaria unapatikana kwa wingi

  • Matumizi ya dawa ya hivi karibuni ambayo yanadhoofisha mfumo wa kingamaradhi (dawa za kukandamiza kingamwili)

Ikiwa huna yoyote kati ya dalili hizi za onyo lakini una homa kwa zaidi ya siku 1 au 2, mpigie simu daktari wako. Kulingana na umri wako, dalili na historia ya afya, daktari wako anaweza kukuomba uende akuangalie na anaweza kufanya vipimo ili kujua kinachosababisha homa yako. Anaweza kuagiza:

  • Vipimo vya damu

  • Vipimo vya mkojo

  • Eksirei ya kifua

  • Vipimo vingine, kulingana na dalili zako

Ikiwa homa yako inadumu kwa zaidi ya siku 3 hadi 4 kukiwa na dalili nyinginezo au la, nenda kwa daktari wako.

Madaktari wanatibu vipi homa kwa watu wazima?

Kulingana na vile unavyo hisi na hali joto uliyo nayo, daktari wako huenda asilazimike kutibu homa yako, homa maana yake ni kwamba mwili wako unapambana na maambukizi. Daktari wako atakupatia matibabu ya kile kinachosababisha homa.

Ikiwa homa yenyewe inakufanya usijisike vizuri, daktari wako huenda akakupa dawa, kama vile acetaminophen au ibuprofen, ambayo itashusha homa yako. Kunywa zaidi viowevu na kuvaa nguo nyepesi kunaweza kukufanya pia ujisikie vizuri.

Ikiwa homa yako iko juu zaidi ya 105.8° F (41.0° C), huenda ukahitaji kulazwa hospitalini. Hospitalini utapewa viowevu kupitia kwenye mishipa (IV) na mablanketi ya kushusha joto.