Maambukizi ya Stafailokokasi aureasi

(Maambukizi ya staph)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2023

Je, stafailokoki aureasi ni nini?

Stafailokokasi aureasi ("Staph") ni kikundi cha kawaida cha bakteria Kwa kawaida baadhi ya aina za staph huishi katika ngozi za watu na kwenye mazingira na hazisababishi ugonjwa. Aina zingine za staph, hasa Stafailokokasi aureasi, zinaweza kusababisha maambukizi makali. Mara nyingi huitwa maambukizi ya staph.

  • Unaweza kupata maambukizi ya staph kutoka kwa mtu mwingine kwa kugusa vitu ambavyo vina bakteria

  • Maambukizi ya staph yanaweza kuwa kiasi au ya hatari

  • Bakteria wa Staph wanaoingia kwenye mtiririko wa damu wanaweza kusababisha matatizo kwenye ogani zako

  • Madaktari hutibu maambukizi ya staph kwa kutumia dawa za kuua bakteria

  • Maambukizi mengi ya staph hustahimili dawa za kawaida za kuua bakteria

  • Unaweza kusaidia kuzuia maambukizi ya staph kwa kunawa mikono yako vizuri

Stafailokoki aureasi inayostahimili Methisilini (MRSA)

Maambukizi ya staph hapo awali yalikuwa yakiponywa na dawa nyingi za kuua bakteria. Sasa aina nyingi za staph zimekuwa stahimilivu kwa dawa zote kali za kuua bakteria. Staph ambayo haiwezi kuponywa kwa kikundi kimoja cha dawa za kawaida za kuua bakteria huitwa MRSA (Stafailokokasi aureasi inayostahimili Methisilini). MRSA na aina zingine sugu zaidi za staph zinazidi kuenea, haswa katika hospitali. Maambukizi haya hayatibiki kirahisi.

Je, nini husababisha maambukizi ya staph?

Maambukizi ya staph yanaweza kusambaa kwa urahisi kwa:

  • Kumgusa mtu mwingine mwenye maambukizi

  • Kugusa vitu vyenye bakteria (kama vile vifaa vya mazoezi, simu, vitasa vya milango, kidhibiti cha mbali, au vitufe vya lifti)

Kwa kawaida staph huambukiza:

  • Ngozi

Hata hivyo, staph inaweza kuhama kupitia mtiririko wa damu yako na kuambukiza karibu kila sehemu ya mwili wako kama vile mifupa na vali za moyo wako. Pia staph inaweza kujibandika kwenye vifaa vya matibabu kwenye mwili wako, kama vile kifaa cha kudhibiti mapigo ya moyo, na kifundo bandia, au vali ya moyo.

Je, waenezaji wa staph ni nini?

Baadhi ya watu wana bakteria wa staph kwenye ngozi au pua zao lakini hawana dalili. Watu hawa huitwa waenezaji. Waenezaji wanaweza kusambaza bakteria kwa watu wengine na kuwapatia maambukizi. Watu wanaofanya kazi hospitalini au ni wangonjwa walio hospitalini wana uwezekano mkubwa wa kuwa waenezaji.

Je, zipi ni dalili za maambukizi ya staph?

Ikiwa una maambukizi ya staph kwenye ngozi yako, unaweza kuwa:

  • Maumivu na wekundu wa ngozi yako (Selulitisi)

  • Malengelenge yenye kuwasha au yenye kuuma ambayo yamejaa majimaji meupe au njano ambayo hupasuka na kuacha gaga (upele ambukizi wa malengelenge)

  • Uvimbe uchungu, uliojaa usaha chini ya ngozi yako (majipu)

Iwapo una maambukizi ya staph kwenye sehemu nyingine ya mwili wako, unaweza kupata dalili zingine:

  • Maambukizi ya matiti (uvimbe wa titi): Majipu uchungu na mekundu (vifuko vya usaha) kwenye titi, ambayo huwapata sana akina mama wanaonyonyesha mara nyingi wiki 1 hadi 4 baada ya kuanza kuonyonyesha

  • Maambukizi ya mapafu (nimonia): Mara nyingi homa kali, kushindwa kupumua, na kukohoa makohozi yenye damu

  • Maambukizi ya damu (sepsisi): Homa kali na wakati mwingine hali ya hatari ya kupungua sana kwa shinikizo la damu (mshtuko wa maambukizi)

  • Maambukizi ya vali ya moyo (endokardaitisi): Homa na kukosa pumzi —hali hii inaweza kuwa hatarishi

  • Maambukizi ya mifupa (ostiyomayelaitisi): Mzizimo, homa, maumivu ya mifupa, na wekundu na kuvimba kwa ngozi iliyo juu ya mfupa

Baadhi ya Maambukizi ya Mifupa Yanayosababishwa na
Kisiba (Jipu)
Kisiba (Jipu)

Kisiba (jipu) kwenye picha hii ni sehemu laini, iliyovimba na imejaa usaha.

Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.

Jipu Chini ya Nyusi za Jicho
Jipu Chini ya Nyusi za Jicho

Mwanamke huyu ana uvimbe wa jipu, jekundu chini ya nyusi za jicho lake.

DermPics/MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI

Upele ambukizi wa malengelenge
Upele ambukizi wa malengelenge

Kwa upele ambukizi wa malengelenge, vishada vya vidonda huchanika na kutengeneza mpasuko wenye rangi ya asali.

Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.

Upele Ambukizi wa Malengelenge kwa Mtoto
Upele Ambukizi wa Malengelenge kwa Mtoto

Mtoto huyu mweye upele ambukizi wa malengelenge ana vishada vya ukurutu/upele, vidonda vyenye magamba ya njano.

DKT P. MARAZZI/MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina maambukizi ya staph?

Kwa kawaida madaktari wanaweza kutambua ngozi yenye maambukizi ya staph kwa kuichunguza. Ili kujua kama una maambukizi ya staph katika sehemu zingine, madaktari hufanya vipimo kama vile:

  • Kipimo cha damu

  • Kipimo cha majimaji ya mwili yenye maambukizi

Je, madaktari hutibu vipi maambukizi ya staph?

Madaktari hutibu maambukizi ya staph kwa kutumia dawa za kuua bakteria. Kama ulipata maambukizi hospitalini, watakupatia dawa za kuua bakteria ambayo inafanya kazi dhidi ya MRSA.

  • Wakati mwingine maambukizi ya ngozi yanaweza kutibiwa kwa mafuta yenye dawa ambayo unayapaka kwenye ngozi yako

  • Kama maambukizi ya ngozi yako ni makali sana, utapatiwa dawa za kuua bakteria ili uzimeze au wakati mwingine kupitia mshipa

  • Kwa kawaida maambukizi ya mifupa yanahitaji upasuaji ili kuondoa tishu ya mfupa yenye maambukizi

  • Ikiwa una jipu, madaktari watalikata ili kulifungua na kuondoa usaha

Je, ninawezaje kuzuia maambukizi ya staph?

  • Nawa mikono yako vizuri kwa sabuni na maji au tumia kitakatisha mikono

  • Usipike au kuandaa chakula kwa ajli ya watu wengine ikiwa una maambukizi ya staph kwenye ngozi yako