Ostiyomayelaitisi ni nini?
Ostiyomayelaitisi ni maambukizi ya mfupa.
Mfupa ni tishu hai na unaweza kuambukizwa kama sehemu nyingine yoyote ya mwili wako
Maambukizi huingia kwenye mfupa kupitia damu yako au kutoka kwenye tishu ya karibu yenye maambukizi au kidonda kilicho wazi
Unaweza kuwa na maumivu katika mfupa wako, homa, na kupoteza uzani
Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta), au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku)
Utahitaji kutumia dawa za kuua bakteria kwa wiki kadhaa au uwezekano wa kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kutibu ostiyomayelaitisi
Maambukizi yakiwa mabaya, baadhi ya sehemu za mfupa zinaweza kufa, hivyo kufanya maambukizi kuwa magumu kutibu.
Wakati mwingine maambukizi huenea kutoka kwa mfupa wako hadi kwenye ngozi na misuli iliyo karibu.
Je, nini husababisha ostiyomayelaitisi?
Kwa kawaida maambukizi ya mifupa husababishwa na bakteria wanao:
Enea kutoka kwa ngozi iliyo karibu iliyoambukizwa
Ingia kupitia kidonda kilichochimba juu ya mfupa
Ni mara chache bakteria:
Husafiri kupitia mtiririko wa damu kutokana na maambukizi katika sehemu nyingine ya mwili wako
Huingia wakati mfupa uliovunjika umetoboa ngozi
Ni matatizo ya upasuaji wa mfupa au kiungo
Una uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya mifupa ostiyomayelaitisi kama:
Una matatizo mengine ya kiafya, kama vile saratani, ugonjwa wa selimundu, au mfumo wa kingamwili ambao ni dhaifu
Unajidunga dawa za mtaani
Uko kwenye huduma ya kusafisha damu
Zipi ni dalili za ostiyomayelaitisi?
Dalili za maambukizi ya mifupa ostiyomayelaitisi ni pamoja na:
Homa
Maumivu kwenye mifupa iliyoambukizwa
Sehemu nyekundu, ya vuguvugu, iliyovimba juu ya mfupa wenye maambukizi
Kupungua uzani na uchovu
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina maambukizi ya mifupa ostiyomayelaitisi?
Madaktari hufanya:
Vipimo vya damu
Eksirei, uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta), MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku)
Ikiwa vipimo hivi vinaonyesha uwepo wa ostiyomayelaitisi, basi madaktari wanaweza:
Kuchukua sampuli ya sehemu iliyoambukizwa kwa kutumia sindano au kwa upasuaji
Je, madaktari wanatibu vipi maambukizi ya mifupa ostiyomayelaitisi?
Madaktari hutibu maambukizi ya mifupa ostiyomayelaitisi kwa kutumia:
Dawa za kuua bakteria zinazoingizwa kwa njia ya mshipa
Unaweza kutakiwa kutumia dawa za kuua bakteria kwa wiki 4 hadi 8, hasa ikiwa umekuwa na maambukizi kwa muda mrefu.
Ikiwa wewe ni mgonjwa au kuna mifupa mingi iliyokufa, madaktari wanaweza:
Kufanya upasuaji ili kuondoa mfupa ulioambukizwa na kufa