Maambukizi ya Virusi vya Hanta

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Virusi vya hanta ni nini?

Virusi vya hanta ni maambukizi ya virusi yaliyoenezwa kwa mkojo na kinyesi cha panya. Virusi vya hanta kinaweza musababisha maambukizi ya kutishia maisha ya mapafu na figo.

  • Unaweza kupata virusi vya hanta kwa kupumua hewa ambayo imechafuliwa na mkojo au kinyesi cha mnyama mgugunaji (panya) iliyeambukizwa

  • Virusi vya hanta husababisha homa, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli na matatizo kwa mapafu au mafigo yako

  • Maambukizi makali ya hanta yanaweza kufisha

Je, nini husababisha maambukizi ya virusi vya hanta?

Virusi vya hanta huambukiza wanyama wagugunaji wa mwituni ulimwengu mzima. Kuna aina tofauti za virusi vya hanta katika sehemu tofauti za ulimwengu.

Kulingana na aina ambayo uko nayo, virusi huathiri viungo tofauti.

Mapafu: Aina ya virusi vya hanta katika Marekani magharibi na Amerika Kusini na Kati kwa kawaida husababisha maambukizi ya mapafu ambayo husababisha kukohoa, tatizo katika kupumua na kiowevu kwenye mapafu yako.

Figo: Aina ya virusi vya hanta katika Korea na Ulaya husababisha upele na maumivu ya tumbo na vinaweza kusitisha mafigo yako yasifanye kazi.

Je, dalili za virusi vya hanta ni zipi?

Dalili za mapema za hanta ni?

  • Homa

  • Maumivu ya kichwa na maumivu ya misuli

  • Wakati mwingine, maumivu ya tumbo, kutapika au kuhara

Dalili hizi za mapema zinaendelea kwa takriban siku 4, wakati mwingine zaidi. Kisha, unaweza kuwa na dalili zingine kulingana na aina ya virusi vya hanta.

Wakati mapafu yako yameathiriwa:

  • Kukohoa matatizo ya kupumua ambayo yanakuwa mabaya zaidi kwa saa chache

  • Shinikizo la chini la damu

Maambukizi ya virusi vya hanta ambavyo huathiri mapafu yako yanaweza kuwa hatari.

Wakati homa ya damu inahusisha figo zako:

  • Wakati mwingine, damu kwenye mkojo au kinyesi au vilia vyako kwenye ngozi yako

  • Wakati mwingine pia una acha kutengeneza mkojo:

  • Wakati mwingine, kuchanganyikiwa kunaosababisha kuzirai

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa virusi vya hanta?

Madaktari wanashuku virusi vya hanta ikiwa una dalili na umekuwa mahali kuna wanyama wagugunaji na kinyesi chao.

  • Ili kuthibitisha, watafanya vipimo vya damu

  • Ikiwa unakohoa au tatizo la kupumua, wanaweza kufanya eksirei ya kifua na ekokadiografia (kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa moyo wako)

Madaktari hutibu virusi vya hanta vipi?

Daktari atakutibu dalili zako.

Ikiwa una aina ya virusi vya hanta ambavyo vinaathiri mapafu yako, madaktari:

  • Watakupea oksijeni ili kukusaidia kupumua

  • Wakati mwingine, kukuweka kwenye kipumuaji ili kukusaidia kupumua

Ikiwa una aina ya virusi vya hanta ambavyo vinaathiri mafigo yako, madaktari:

  • Watakwambia utumie dawa ya kuua virusi ambayo inaweza kutuliza dalili zako

  • Wakati mwingine, kukupatia huduma ya kusafisha damu (hutumia mashine ili kuchuja uchafu kutoka kwenye damu yako kwa sababu figo zako hazina uwezo wa kuchuja)