Je, homa ya kutokwa na damu ni nini?
Homa ya kutokwa na damu ni maambukizi hatari ya virusi ambayo husababisha homa na kutokwa damu kwenye mdomo, pua, au ogani zilizo ndani ya mwili wako. Maambukizi haya yanaweza kuwa hatari.
Unaweza kupata maambukizi haya kwa kugusa watu, wanyama, au wadudu walioambukizwa, au maji ya mwili wao, kama vile mate, mkojo, kinyesi au damu
Madaktari wanaweza kujua ikiwa una homa ya kutokwa na damu kwa kufanya vipimo vya damu
Hakuna dawa inayoweza kuponya homa ya kutokwa na damu, kwa hivyo madaktari hutibu dalili zako, kukupa majimaji, na kuhakikisha viungo vyako vinafanya kazi vizuri
Wakati mwingine, watajaribu dawa za kuua virusi
Ni nini husababisha homa ya damu?
Homa za damu zinasababishwa na virusi. Homa za damu ni kikundi cha maambukizi ya virusi yakijumuisha:
Ebola, katika sehemu za Afrika
Homa ya Lassa, katika Afrika Magharibi
Homa ya Dengue, katika Asia na Amerika Kusini
Hantavirus, katika Marekani, Amerika Kusini na Kati, Ulaya na Korea
Homa ya manjano, katika maeneo ya tropiki ya Afrika, Amerika Kusini, na kusini mwa Panama
Je, dalili za homa ya damu ni zipi?
Virusi hivi hufanya mishipa ya damu kwenye mwili wako ivuje damu, hivyo kusababisha:
Kuvuja damu chini ya ngozi yako na kutoka mdomoni, pua au viungo vyako
Zaidi ya kuvuja damu, dalili zingine zinajumuisha:
Homa
Maumivu ya mwili na misuli
Uchovu na udhaifu
Wakati ni kali, kuzirai, mshtuko, na kushindwa kufanya kazi kwa mapafu, ini na mafigo