Homa ya Manjano

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2024

Homa ya manjano ni nini?

Homa ya manjano ni maambukizi ya virusi yanayoenezwa na mbu.

  • Unaweza kupata homa ya manjano kutokana na kung'atwa na mbu aliyeambukizwa

  • Mbu kwenye maeneo ya tropiki ya Afrika ya kati, Amerika ya Kati na Amerika Kusini zinabeba homa ya manjano

  • Husababisha maumivu ya kichwa, kizunguzungu, maumivu ya misuli na homa

  • Wakati mwingine, ngozi na macho yako hugeuka kuwa ya manjano (homa ya nyongo ya manjano) kwa sababu ugonjwa unaathiri ini lako

  • Homa ya manjano inaweza kuwa hatari ikiwa inaathiri sana viungo vyako vya utumbo

  • Njia zile bora zaidi za kuzuia homa ya manjano ni kwa kupata chanjo (sindano) na kuepuka kung'atwa na mbu

Je, nini husababisha homa ya manjano?

Homa ya manjano husababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu. Ugonjwa huu hutokea tu katika maeneo ya kitropiki ya Afrika ya Kati, kusini mwa Panama, na Amerika ya Kusini. Maambukizi hutokea zaidi wakati wa miezi ya joto, mvua, na unyevunyevu huko Amerika Kusini na wakati wa mwisho wa mvua na misimu ya kiangazi mapema barani Afrika.

Je, dalili za homa ya manjano ni zipi?

Baadhi ya watu hawana dalili zozote.

Dalili za mapema zinajumuisha:

  • Maumivu ya kichwa, homa, mzizimo na maumivu ya misuli ya ghafla

  • Kuhisi udhaifu na kizunguzungu

  • Kuhisi mgonjwa tumboni na kutapika

Dalili hizi zinaisha baada ya siku chache. Watu wengine hawana dalili zingine na hupona kutokana na homa ya manjano. Watu wengine wanapata dalili kali zaidi.

Katika matukio kali zaidi, virusi hivyo vinaweza kuathiri vingi vya viungo vyako, ikijumuisha ini, mafigo na moyo wako. Dalili za baadaye za homa ya manjano zinajumuisha:

  • Homa kali

  • Kutapika damu

  • Ngozi na macho ya manjano (homa ya nyongo ya manjano)

  • Kuvuja damu kutoka kwenye mapua, mdomo au utumbo wako

  • Shinikizo la chini la damu kupita kaisi

  • Kifafa na kuzirai (wakati ugonjwa ni mkali)

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina homa ya manjano?

Madaktari wanashuku homa ya manjano ikiwa una dalili na umekuwa kwenye eneo ambalo kuna matukio ya homa ya manjano. Kwa kuthibitisha, daktari atafanya vipimo vya damu.

Madaktari hutibu homa ya manjano vipi?

Hakuna tiba ya homa ya manjano. Madaktari watatibu dalili zako na kukupatia:

  • Viowevu kupitia kwenye mshipa ili kudumisha shinikizo la damu yako juu

  • Dawa ili kutibu au kusitisha kuvuja damu, kama vile vitamini K, ambayo husaidia damu yako kuganda

  • Wakati mwingine, kukuweka kwenye mashine ili kusaidia figo zako (kusafisha damu) kutoa uchafu kutoka kwenye mwili wako

  • Kukuweka kwenye chumba ambacho kiwewekwa vioo na kunyunyiziwa kinyunyiziaji cha wadudu ili kuzuia mbu kueneza virusi kwa watu wengine

Je, ninawezaje kuzuia homa ya manjano?

Kuepuka ming'ato ya mbu

Ukiishi katika au kutembelea maeneo yaliyo na homa ya manjano, chukua hatua ili kuepuka ming'ato ya mbu:

  • Weka kinyunyiziaji cha wadudu kwa DEET kwenye ngozi yako

  • Nyunyizia au loweza mavazi yako kwa kifukuza mdudu kilicho na permethrin

  • Tumia vyandarua

  • Valia suruali na mashati yenye mikono mirefu

  • Epuka kwenda nje ikiwa si lazima

Pata chanjo ikiwa unaenda kwenye eneo ambalo lina homa ya manjano

Chanjo inapatikana ili kuzuia homa ya manjano na inapaswa kuchukuliwa wiki 3 hadi 4 kabla ya kwenda kwenye eneo lenye homa ya manjano.

  • Katika Marekani, chanjo ya homa ya manjano inatolewa katika kliniki za dawa ya usafiri, zilizo nchi mzima

  • Watu wengi wanaweza kupata chanjo, isipokuwa watoto wachanga kuliko miezi 6, wanawake wajawazito au watu walio na mifumo dhaifu ya kingamwili—ongea na daktari wako kuhusu kupata chanjo