Hali ya Kiwango cha Sukari Kusalia Juu kwa Muda Mrefu (Hyperosmolar Hyperglycemic)

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Je, hali ya hyperosmolar hyperglycemic (HHS) ni nini?

Hali ya hyperosmolar hyperglycemic (HHS) ni tatizo mbaya inayosababishwa na kisukari. Kisukari ni ugonjwa ambao viwango vyako vya sukari kwenye damu (glukosi) kuwa juu sana.

Katika HHS, damu yako imekolea sana na kiwango cha sukari kwenye damu yako kiko juu sana.

  • HHS ni tatizo la aina ya 2 ya kisukari

  • Unakosa maji mwilini sana, jambo ambalo linaweza kusababisha kuchanganyikiwa, kupoteza fahamu, matukio ya mishtuko, na kifo

  • Matibabu ni kuwekwa majimaji kwenye mshipa wako wa damu na insulini

Je, HHS husababisha na nini?

HHS husababishwa na viwango vya juu sana vya sukari katika damu, kwa kawaida kwa watu walio na aina ya 2 ya kisukari. Watu walio na kisukari cha aina ya 1 huwa hawapati HHS. Badala yake, wanaweza kupata ketoasidosisi ya kisukari. Viwango vya juu sana vya sukari kwenye damu hukusababisha kukojoa mkojo mwingi kuliko kawaida. Hii husababisha upungufu mkubwa wa maji mwilini na hufanya damu yako kukolea zaidi.

Una uwezekano mkubwa wa kupata HHS ikiwa una aina ya 2 ya kisukari na:

  • Zaidi kwa umri

  • Uache kutumia dawa yako ya kisukari

  • Upate maambukizi au mkazo mwingine kwa mwili wako kama vile shambulio la moyo, kiharusi, au upasuaji

  • Hunywi majimaji ya kutosha au huoni kiu

  • Una matatizo ya figo

  • Utatumia dawa fulani, kama vile kotikosteroidi na za kupunguza ongezeko la maji mwilini

Je, dalili za HHS ni zipi?

Dalili za kwanza ni:

  • Kukojoa sana

  • Kuwa na kinywa kikavu na ngozi kavu

  • Kuhisi kiu sana

  • Mabadiliko ya kiakili, kama vile kuchanganyikiwa au kusinzia kupita kiasi

Ikiwa haitatibiwa mapema, inaweza kusababisha pia:

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina HHS?

Madaktari wanaweza kufikiria kuwa una HHS ikiwa una kisukari na unaonekana kuchanganyikiwa. Wanajua kwa hakika kwa kufanya:

  • Vipimo vya damu na mkojo

Je, madaktari hutibu vipi HHS?

Madaktari hukutibu hospitalini kwa kutumia:

  • Majimaji na elektroliti (madini muhimu ya kuufanya mwili wako kufanya kazi kwa kawaida) kwenye mshipa wako wa damu.

  • Kuweka Insulini kwenye mshipa wako wa damu

  • Vipimo vya mara kwa mara vya damu ili kuhakikisha kuwa kiwango cha sukari kwenye damu yako na elektroliti zinarejelea hali ya kwa kawaida

Madaktari hutibu pia tatizo lingine lolote lililosababisha HHS.