Matibabu ya Dawa ya Kisukari

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023 | Imebadilishwa Apr 2023

Kisukari ni ugonjwa wa kudumu maisha yote ambao viwango vya sukari kwenye damu (glukosi) huwa juu sana.

Je, watu wenye kisukari wanahitaji dawa kwa nini?

Ikiwa viwango vyako vya sukari iliyo kwenye damu itabaki juu kwa muda mrefu, utapata matatizo makubwa ya kisukari. Ikiwa kufuata lishe yako na kufanya mazoezi kila wakati hakudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu yako, utahitaji kunywa dawa. Dawa ambayo madaktari huagiza hutegemea aina ya kisukari ulichonacho na jinsi sukari kwenye damu yako ilivyo juu.

Wakati mwingine, dawa za kisukari hufanya kiwango cha sukari kwenye damu yako kuwa chini sana. Kiwango cha sukari kwenye damu kuwa chini inajulikana kama hipoglisemia.

Je, insulinini nini?

Insulini ni homoni asilia ambayo mwili wako hutengeneza ambayo hupunguza kiwango cha sukari kwenye damu yako. Insulini pia ni dawa ambayo unaweza kutumia. Watu wengi wanaohitaji kutumia insulini hufanya hivyo kwa kutumia sindano. Aina mpya ya insulini inaweza kutumiwa kupitia kipulizia.

Je, ni sharti nitumie insulini?

Ikiwa una kisukari cha aina ya 1, ni sharti utumie insulini. Katika kisukari cha aina ya 1, mwili wako hautengenezi insulini yoyote.

Ikiwa una aina ya 2 ya kisukari, huenda hutalazimika kutumia insulini isipokuwa ikiwa dawa zingine hazidhibiti vizuri sukari kwenye damu yako.

Je, ninaweza kutumia aina gani za insulini?

Insulini ipo katika miundo tofauti kulingana na jinsi inavyoanza kufanya kazi haraka na kipindi cha muda itakachodumu:

  • Insulini inayofanya kazi kwa haraka huanza kufanya kazi baada ya dakika 5 hadi 15 na hudumu kwa takriban saa 4—unaweza kujidunga insulini inayofanya kazi haraka kabla ya kula

  • Insulini ya kawaida huanza kufanya kazi baada ya dakika 30 hadi 60 na hudumu kwa takriban saa 6 hadi 8

  • Insulini ya muda wa kati huanza kufanya kazi baada ya saa 1 hadi masaa 2 na hudumu kwa takriban siku moja

  • Insulini ya muda mrefu ina athari ndogo sana katika saa chache za kwanza lakini hudumu kwa takribam masaa 20 hadi 36

Unaweza kutumia aina zaidi ya moja ya insulini. Na unaweza kutumia insulini mara moja au mara kadhaa kwa siku. Aina unayotumia na mara unazotumia inategemea mambo kadhaa, yanayojumuisha:

  • Jinsi viwango vyako vya sukari kwenye damu vinavyoathiriwa na mabadiliko katika lishe na shughuli

  • Mara ambazo uko tayari kupima kiwango cha sukari kwenye damu yako

  • Mara ambazo uko tayari kutumia insulini

  • Jinsi unavyoweza kufuata na lishe na ratiba yako ya mazoezi

Madaktari watabaini aina ya insulini itakayokufaa zaidi. Baadhi ya watu hutumia kiwango sawa cha insulini kila siku. Watu wengine hubadilisha kiasi cha insulini wanachotumia kila siku kulingana na lishe yao, mazoezi na kiwango cha sukari kwenye damu. Mahitaji yako ya insulini yanaweza kubadilika ikiwa utaongeza au kupunguza uzani, utabadilisha kiasi cha mazoezi unayofanya, ikiwa utakuwa na msongo mwingi wa kihisia, au kuwa mgonjwa au kupata maambukizi.

Je, ninapaswa kutumia insulinivipi?

Mara nyingi, utapatiwa insulini kwa kuchomwa sindano chini ya ngozi yako. Kuna njia tofauti za kujidunga sindano za insulini:

  • Sindano ya insulini unayojaza kutoka kwa chupa ya insulini

  • Kalamu ya insulini (kifaa kinachohifadhi dozi kadhaa za insulini)—kalamu hiyo ina sehemu ya kubonyeza ambayo unaweza kutumia ili kurekebisha kipimo cha insulin na kitufe unachofinya ili kujidunga sindano ya insulini

  • Pampu ya insulin (kifaa kinachotumia betri kinachosukuma insulini kupitia sindano ndogo iliyo chini ya ngozi yako)

Njia zisizo za kawaida unazoweza kutumia insulini ni pamoja na:

  • Kifaa cha kipulizia kinachokuwezesha kuvuta insulini

  • Kifaa cha pampu ya hewa kinachopuliza insulini chini ya ngozi yako

Je, insulini inaweza kusababisha matatizo gani?

Ikiwa unatumia insulini nyingi kupita kiasi au huli mara kwa mara, sukari kwenye damu yako inaweza kupungua sana (hipoglisemia).

Baada ya kipindi cha wakati, mwili wako unaweza kuzoea insulini. Hii inamaanisha kuwa mwili wako unaweza kuhitaji insulini zaidi na zaidi ili kupata matokeo sawa.

Pia, sehemu unayojidunga sindano inaweza kuwa na matatizo, kama vile:

  • Mmenyuko wa mzio, kusababisha maumivu, hisia ya kuungua, wekundu, kuwasha na uvimbe

  • Mirundikano ya mafuta, hivyo kufanya ngozi yako kuwa na uvimbe

  • Mashimo kwenye ngozi yako

Unaweza kuepuka meng ya matatizo haya kwa kujidunga sindano katika sehemu tofauti kwenye mwili wako.

Je, ni dawa gani zingine zinazotumiwa kutibu kisukari?

Kando na insulini, aina nyingine kadhaa za dawa hutumiwa kudhibiti sukari kwenye damu ya watu walio na kisukari. Baadhi humezwa na zingine hudungiwa kwa sindano. Wakati mwingine unahitaji zaidi ya dawa moja au unahitaji kutumia insulini pamoja na dawa hizi. Madaktari huchagua dawa zinazofaa kwa kisukari chako ili kiwango cha sukari kwenye damu yako kiwe chini ya udhibiti bila kukisababisha kupungua sana.

Dawa za kisukari hufanya kazi kwa njia tofauti ili kudhibiti sukari kwenye damu yako, njia hizi hujumuisha:

  • Kusisimua kongosho lako (kiungo kilicho kwenye sehemu ya tumbo ambako insulini inatengenezwa) kuzalisha insulini ya mwili wako

  • Kuzuia ini isitoe sukari kwa mtiririko wa damu yako

  • Kuzuia tumbo na utumbo wako usiruhusu sukari iliyo kwenye vyakula kuingia kwenye mtiririko wa damu yako

Dawa za kisukari zinaweza kusababisha hipoglisemia na athari nyingine. Zungumza na daktari wako ili kujua ishara.

Unapotumia insulini au dawa zingine za kisukari, ni muhimu kupima kiwango cha sukari kwenye damu yako mara kwa mara na kumwona daktari wako ili: