Ugonjwa wa Kimetaboliki

Imepitiwa/Imerekebishwa Oct 2023

Je, ugonjwa wa kimetaboliki ni nini?

Ugonjwa wa kimetaboliki ni kundi la matatizo ya kiafya yanayohusisha metaboliki yako na yanakufanya uwe na uwezekano mkubwa wa kuwa na ugonjwa wa moyo, kiharusi na kisukari. Metaboliki inarejelea michakato yote tofauti ya kemikali inayoendelea kwenye mwili wako.

Ugonjwa wa kimetaboliki ni wa kawaida sana nchini Marekani. Watu walio na ugonjwa wa kimetaboliki wana:

Je, ni nini husababisha ugonjwa wa kimetaboliki?

Chanzo cha ugonjwa wa kimetaboliki hakijulikani.

Kuna uwezekano mkubwa wa wewe kupata ugonjwa wa kimetaboliki ikiwa una mafuta kwenye eneo la tumbo yako (una umbo la tufaha) badala ya nyonga yako (una umbo la pea). Hii hutokea kwa:

Ugonjwa wa kimetaboliki unaweza kuathiri watoto na vijana vilevile.

Je, dalili za ugonjwa wa kimetaboliki ni zipi?

Ugonjwa wa kimetaboliki wenyewe hausababishi dalili zozote. Lakini unaweza kuwa na dalili za matatizo yake, kama vile:

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa kimetaboliki?

Ugonjwa wa kimetaboliki una ufafanuzi mwingi tofauti. Madaktari mara nyingi hutambua kuwa una ugonjwa wa kimetaboliki ikiwa una kiuno kikubwa—inchi 40 (sentimita 102) au zaidi kwa wanaume na inchi 35 (sentimita 89) au zaidi kwa wanawake—na hali 2 au zaidi ya zifuatazo:

  • Kiwango cha sukari kwenye damu baada ya kutokula usiku kucha (100 au zaidi)

  • Shinikizo la juu la damu (130/85 au zaidi AU unatumia dawa ya kutibu shinikizo la damu)

  • Kiasi kikubwa cha mafuta katika damu yako (trigliseridi ya 150 au zaidi)

  • Kiwango cha chini cha HDL (lehemu "nzuri")

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa kimetaboliki?

Madaktari watakusaidia kupunguza uzani kwa kukushauri kula lishe bora na kufanya mazoezi zaidi. Watakupa pia dawa za kutibu magonjwa yoyote uliyo nayo, kama vile: