Uvimbe wa Shingo kwa Watoto

(Uvimbe Usio wa Kawaida Kwenye Shingo)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Wewe au mtoto wako anaweza kugundua uvimbe kwenye shingo ya mtoto wako. Utaweza tu kuihisi, lakini wakati mwingine unaweza kuiona pia. Ikiwa si chungu, kwa kawaida huwa inaisha haraka, hata kabla uone daktari.

  • Uvimbe wa shingo ni wa kawaida kwa watoto

  • Uvimbe mwingi wa shingo kwa watoto unasababishwa na maambukizi ambayo huisha yenyewe

  • Uvimbe unaweza au unaweza kosa kuwa na uchungu, kulingana na kisababishaji

  • Ikiwa mtoto wako amekuwa na uvimbe kwa wiki kadhaa, madaktari wanaweza kufanya vipimo iki kuangalia kisababishaji kali zaidi

Ni nini husababisha uvimbe wa shingo?

Kisababishaji cha kawaida sana cha uvimbe wa shingo ni:

  • Vinundu vya limfu vilivyovimba

Nodi za limfu ni mabonge madogo ya tishu ambayo ni sehemu ya mfumo wa limfu na zinasaidia kupigana na maambukizi. Kwa kawaida huwa haugundui nodi za limfu isipokuwa kama zimevimba. Watu wakati mwingine huita hizi "tezi zilizovimba," lakini nodi za limfu si tezi.

Visababishaji vya kawaida vya vinundu vya limfu vilivyovimba vinajumuisha:

Kisababishaji kisicho cha kawaida sana cha uvimbe wa shingo ni:

  • Uvimbe uliojaa maji (kifuko kilichojaa kiowevu)

  • Kuvimba kwenye tezi chini ya ulimi ambazo hutengeneza mate

  • Saratani kama vile limfoma, lukemia, au saratani ya tezi dundumio (saratani hutokea kwa nadra kwa watoto)

Madaktari wanawezaje kujua ni kipi kinasababisha uvimbe wa shingo?

Ikiwa mtoto wako amekuwa na uvimbe wa shingo kwa wiki kadhaa, daktari wa mtoto wako anaweza:

  • Kuchukua sampuli ya makamasi kwenye koo ili kuangalia maambukizi ya koo

  • Kufanya vipimo vya damu vya mono, tatizo la tezi chochezi au lukemia

  • Kufanya kipimo cha ngozi ili kupima kifua kikuu

  • Kufanya kipimo cha eksirei, ultrasound, uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku)

Ikiwa vipimo hivi havitatoa jibi dhahiri, madaktari wanaweza:

  • Kufanya uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi wa uvimbe

Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi inahusisha kuondoa sehemu ndogo ya tishu kwa kutumia sindano. Kisha madaktari huangalia tishu kwa kutumia hadubini.

Madaktari hutibu aje uvimbe wa shingo?

Uvimbe mwingi wa shingo unasababishwa na maambukizi madogo ya virusi. Hivi huisha vyenyewe bila matibabu. Uvimbe wa shingo kutoka kwa visababishaji vingine unaweza kuhitaji matibabu mahususi kama vile:

  • Dawa za kuua bakteria kwa ajli ya maambukizi ya bakteria

  • Upasuaji kwa ajili ya uvimbe uliojaa maji au uvimbe