Findo na Adenoidi Iliyopanuka

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Findo na adenoidi ni nini?

Findo na adenoidi ni uvimbe wa tishu kwenye sehemu ya nyuma ya koo yako. Zinatega vijidudu na kusaidia mwili wako kupigana na maambukizi. Unaweza kuona findo zako kwenye sehemu ya nyuma ya koo yako. Lakini huwezi kuona adenoidi zako kwa sababu ziko juu nyuma ya paa la mdomo wako.

Locating the Tonsils and Adenoids

The tonsils are two areas of lymphoid tissue located on either side of the throat. The adenoids, also lymphoid tissue, are located higher and further back, behind the palate, where the nasal passages connect with the throat. The adenoids are not visible through the mouth.

  • Findo na adenoidi zinakuwa kubwa zaidi ikiwa una maambukizi

  • Findo au adenoidi kubwa wakati mwingine huifanya iwe ngumu kupumua au kumeza

  • Adenoidi kubwa zinaweza kusababisha matatizo katika upumuaji wakati wa usingizi na kuongeza hatari ya maambukizi ya sikio

  • Wakati mwingine madaktari wanafanya upasuaji ili kuondoa adenoidi ambazo ni kubwa mno

Ni nini husababisha findo na adenoidi kuongezeka kwa ukubwa?

Baadhi ya watoto wanazaliwa na findo na adenoidi ambazo ni kubwa zaidi kuliko kawaida.

Findo na adenoidi za mtoto zinaweza kukua ziwe kubwa mno kwa sababu ya:

Dalili za kuwa na findo na adenoidi zilizopanuka ni zipi?

Findo na adenoidi kubwa mara nyingi hazisababishi dalili: Wakati zinasababisha dalili, watoto wanaweza:

  • Kutoa sauti ni kama wana mafua wakati hawana

  • Kupumua kupitia mdomoni, badala ya mapua yao

  • Kuwa na ugumu wa kupumua au kumeza

Findo na adenoidi iliyopanuka inaweza kusababisha matatizo kali zaidi, kama vile:

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa findo au adenoidi za mtoto wangu ni kubwa sana?

Daktari:

  • Ataangalia findo za mtoto wako kwa kutumia kifinyaji ulimi wakati mtoto wako anatoa ulimi wake nje na kusema "Ah"

  • Angalia adenoidi za mtoto wako kwa kutumia skopu ndogo zaidi inayoingizwa ndani ya sikio la mtoto wako (skopu haiumizi)

Madaktari wanaweza pia kupima matatizo ambayo yanatokana na findo na adenoidi kubwa, kama vile:

  • Maambukizi ya sanasi au sikio, kwa kutumia vipimo vya damu na utafiti wa kutumia picha

  • Kujiunda kwa kiowevu, kwa kutumia vipimo vya kusikia

  • Kupumua kwa shida wakati wa kulala, kwa utafiti wa usingizi

Mtoto wako anaweza kupunguza uzani kwa sababu ya tatizo la kupumua wakati anakula. Daktari atalinganisha uzani wa mtoto wako na chati za ukuaji wa kawaida ili kuona kama kupunguza uzani ni tatizo.

Madaktari wanatibu aje findo na adenoidi zilizopanuka?

Daktari wa mtoto wako anaweza kupea mtoto wako dawa za kutibu maambukizi au mizio ambayo inawasha findo au adenoidi.

Madaktari wanaweza kupendekeza kuondoa adenoidi na findo ikiwa mtoto wako anazo:

  • Kupumua kwa shida wakati wa kulala

  • Wakati mgumu kuongea na kupumua

  • Maambukizi mengi ya koo

Madaktari wanaweza kupendekeza kuondoa adenoidi za mtoto wako pekee ikiwa mtoto wako ana:

  • Maambukizi mengi ya sikio na majimaji yaliyo nyuma ya kiwambo cha sikio ambayo hayawezi kuondolewa.

  • Pua iliyoziba ambayo inafanya iwe vigumu kupumua na kuzungumza

  • Maambukizi mengi ya sanasi

Kwa kawaida watoto wanaweza kwenda nyumbani siku sawa na ya upasuaji. Ikiwa ni tu adenoidi zilitolewa, mtoto wako anapaswa kuhisi vizuri kwa siku 2 hadi 3. Ikiwa findo zilitolewa pia, kupona kunapaswa kuchukua takriban wiki 2.