Maambukizi ya Muda Mrefu ya Sikio la Kati kwa Watoto

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Maambukizi ya muda mrefu ya sikio la kati ni nini?

Sikio la kati ni sehemu iliyo nyuma ya kiwambo cha sikio. Viini vinaweza kuingia kwenye sikio la kati na kusababisha maambukizi. Maambukizi ya sikio la kati pia hujulikana kama kuvimba sehemu ya kati ya sikio. Maambukizi ya kudumu ni yale yanadumu kwa muda mrefu (hata kwa matibabu) au yale hurejea.

  • Maambukizi ya muda mrefu ya sikio yanaweza kuharibu daima sehemu za sikio ambazo zinasaidia mtoto wako kusikia

  • Kwa kawaida huwa hazisababisha maumivu

Je, nini husababisha maambukizi sugu ya sikio?

Kuna uwezekano mkubwa wa mtoto wako kupata maambukizi ya muda mrefu ya sikio ikiwa mtoto wako ana:

  • Maambukizi makali ya sikio mengi sana

  • Shimo kwenye kiwambo cha sikio (kwa mfano kutokana na jeraha au upasuaji wa sikio), haswa ikiwa maji yakiingia kwenye sikio

  • Bomba la eustachian lililozuiwa (bomba linalounganisha sehemu ya ndani ya sikio na sehemu ya nyuma ya koo)

  • Kasoro fulani za kuzaliwa, kama vile kaakaa wazi, ambayo inaathiri mdomo na uso

  • Ugonjwa wa Down

Maambukizi ya muda mrefu ya sikio yanaweza kuwa mabaya zaidi (kulipuka) baada ya mtoto wako kupata mafua au maambukizi mengine ya pua au koo.

Je, dalili za maambukizi sugu ya sikio ni zipi?

  • Tatizo la kusikia

  • Usaha au kiowevu kinachotoka kwenye sikio—usaha unaweza kutoa harufu mbaya sana

Maambukizi ya muda mrefu ya sikio hayafai kuuma isipokuwa kama maambukizi yameenea kwenye mfupa karibu na sikio. Mwambie daktari wako kama mtoto wako ana maambukizi ya muda mrefu ya sikio na anaanza kupata maumivu.

Madaktari wanawezaje kujua kuwa mtoto wangu ana maambukizi ya muda mrefu ya sikio?

  • Madaktari wataangalia sikio la mtoto wako ili kuona kama usaha unatoka kwenye tundu lililopo kwenye kiwambo cha sikio

  • Wataangalia pia mambo yoyote yasiyo ya kawaida kwenye kiwambo cha sikio

Madaktari wakifikiria kuwa maambukizi yanaweza kuwa yameenea, watafanya uchanganuzi wa CT (tomografi ya kompyuta) au MRI (picha inayoonyesha sehemu ya ndani ya mwili wako).

Je, maambukizi ya muda mrefu ya sikio hutibiwaje?

Madaktari watafanya:

  • Safisha sikio la mtoto wako

  • Weka dawa za kuua bakteria na vitone vya sikio vya kotikosteroidi kwenye sikio la mtoto wako

  • Zuia maji yasiingie kwenye sikio la mtoto wako

Ikiwa maambukizi ni mabaya sana, madaktari watampatia pia mtoto wako dawa za kumeza za kuua bakteria.

Ikiwa kiwambo cha sikio cha mtoto wako kimeharibika au kina kishikizo kisicho cha kawaida kwake, madaktari mara nyingi watafanya upasuaji.