Angiofibroma ya vijana ni nini?
Angiofibroma ya vijana ni mabonge ya nadra ya mishipa ya damu ambayo yanakua mahali ambapo koo na mwanzi wa pua wa mtoto wako zinapatana (karibu na adenoidi).
Angiofibroma ya vijana ni za kawaida kwa vijana wa kiume
Zinakua polepole na zinaweza kuenea kwenye sehemu kando ya ubongo na tundu la kishimo cha macho
Dalili za angiofibroma ya vijana ni zipi?
Pua iliyojaa
Maumivu ya kichwa
Kutokwa na damu puani ambao kunaweza kuwa kubaya zaidi
Uso uliovimba
Jicho lililofura
Badiliko kwenye umbo la mapua
Madaktari wanawezaje kujua kama mtoto wangu ana angiofibroma ya vijana?
Madakatri kwa kawaida watafanya uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku)
Madaktari hutibu aje angiofibroma ya vijana?
Kwa kawaida, madaktari watafanya upasuaji ili kuondoa bonge
Madaktari wanaweza pia kutumia tiba ya mionzi, haswa ikiwa bonge ni ngumu kuondolewa kikamilifu au ikirudi