Ugonjwa wa kuota dutu kwenye njia ya hewa unaorejea (RRP) ni nini?
RRP ni hali ya nadra ambayo husababisha kukua kwa kinyama kimoja au zaidi kwenye kisanduku cha sauti cha mtoto.
RRP ni ya kawaida zaidi kwa watoto wa umri wa mwaka 1 hadi 4
Inasababisha badiliko kwenye sauti ya mtoto na wakati mwingine ugumu katika upumuaji
Kwa kawaida madaktari hufanya upasuaji ili kuondoa vishikizo hivyo
Watoto wengi watahitaji upasuaji kadhaa utotoni wote kwa sababu vishikizo huendelea kurudi
Je, ni nini kinachosababisha RRP?
RRP inasababishwa na virusi vya papiloma vya binadamu (HPV). HPV ni virusi sawa ambavyo husababisha dutu sehemu za siri. RPR inaweza kupitishwa kutoka kwa mama aliyeambukizwa na dutu sehemu za siri kupitia njia ya uzazi hadi kwa mtoto wake wakati wa kujifungua. Kwa bahati, watoto wengi wachanga ambao wameambukizwa na HPV huwa hawapati RRP.
Dalili za RRP ni zipi?
Kulia dhaifu
Sauti ya kishindo au ya kukwaruza
Ugumu katika upumuaji ikiwa vishikizo vimeenea kwenye mapafu au koo ya pumzi
Madaktari wanawezaje kujua kama mtoto wangu ana RRP?
Kwa kawaida madaktari huangalia kwenye koo ya mtoto wako kwa kutumia neli ya kutazama na kuangalia kisanduku cha sauti cha mtoto wako. Wakiona kinyama kilichoota, watatoa sehemu yake ndogo ili kuichunguza kwa kutumia hadubini.
Madaktari hutibu RRP aje?
Kwa kawaida madaktari hufanya upasuaji au kutumia leza ili kuondoa vishikizo hivyo
Matibabu kadhaa yanawezahitajika. Wakati mwingine madaktari pia hutoa dawa za kuua virusi.