Uvimbe wa Wilms

Imepitiwa/Imerekebishwa Jul 2024

Je, uvimbe wa Wilms ni nini?

Uvimbe wa Wilms ni aina ya saratani ambapo uvimbe huota kwenye figo. Mara nyingi huwapata watoto wenye umri chini ya miaka 5.

  • Madaktari hawajui chanzo cha uvimbe wa Wilms, lakini watoto wenye shida fulani za kiafya wakati wa kuzaliwa ndio wenye uwezekano mkubwa wa kuupata

  • Watoto wenye uvimbe wa Wilms wanakuwa na uvimbe kwenye matumbo yao na wanaweza kutapika na kupata maumivu ya tumbo, homa, kupoteza hamu ya kula, na tumbo kuvurugika

  • Mara nyingi uvimbe wa Wilms huathiri figo moja, lakini unaweza kuathiri figo zote

  • Matibabu ni yanajumuisha upasuaji, tibakemikali, na wakati mwingine tiba ya mionzi

Je, nini husababisha uvimbe wa Wilms?

Mara nyingi, madaktari hawajui sababu inayosababisha uvimbe wa Wilms. Wakati mwingine husababishwa na shida ya jeni za mtoto.

Je, dalili za uvimbe wa Wilms ni zipi?

Kwa kawaida dalili ya kwanza ya uvimbe wa Wilms ni:

  • Uvimbe usio na maumivu kwenye tumbo la mtoto

Dalili zingine ni pamoja na:

  • Tumbo lililovimba (wakati mwingine wazazi hugundua kuwa mtoto mdogo mara ghafla anahitaji nepi kubwa)

  • Maumivu ya tumbo, homa, kukosa hamu ya kula, tumbo kuvurugika, na kutapika

  • Damu kwenye mkojo

  • Shinikizo la juu la damu

Ikiwa saratani itasambaa hadi kwenye mapafu, inaweza kusababisha kukohoa na kukosa pumzi.

Je, madaktari wanaweza kujuaje ikiwa mtoto wangu ana uvimbe wa Wilms?

Madaktari huhisi uwepo wa uvimbe wa Wilms iwapo watahisi uvimbe kwenye tumbo la mtoto wako. Ili kuthibitisha, daktari atafanya:

Madaktari pia hutumia uchanganuzi wa CT au MRI ili kuangalia kama saratani yoyote imesambaa hadi kwenye vifundo vya limfu, ini au mapafu.

Je, madaktari hutibu vipi uvimbe wa Wilms.

Ili kutibu uvimbe wa Wilms, madaktari:

  • Watafanya upasuaji wa kuondoa figo ambalo lina uvimbe

  • Wakati wa upasuaji, watachunguza ini lingine ili kuona kama lilna saratani

  • Baada ya upasuaji, watamtibu mtoto kwa kutumia tibakemikali

  • Ikiwa saratani imesambaa, watafanya tiba ya mionzi

Mara chache pale uvimbe unapokuwa mkubwa sana au kwenye figo zote, madaktari watatumia tibakemikali ili kupunguza ukubwa wa uvimbe au viuvimbe kabla ya kufanya upasuaji wa kuviondoa.