Je, retinoblastoma ni nini?
Retina ni tishu ambayo ina hisia kali kwa mwanga iliyo nyuma ya mboni ya jicho. Retino blastoma ni saratani ya retina ambayo huwapata zaidi watoto wadogo.
Retinoblastoma inaweza kurithiwa katika familia
Mara nyingi hutokea kabla ya umri wa miaka 2
Karibu mtoto 1 kati ya 4 mwenye retinoblastoma huwa nayo katika macho yote mawili
Mtoto mwenye retinoblastoma anaweza kuwa na mboni nyeupe, makengeza, au shdia ya kuona
Matibabu ni yanajumuisha upasuaji, tibakemikali, na wakati mwingine tiba ya mionzi
Je, nini husababisha retinoblastoma?
Retinoblastoma husababishwa na tatizo la jeni ambazo hudhibiti maendeleo ya macho. Mtoto anaweza kurithi hili tatizo kutoka kwa mzazi au tatizo linaweza kutokea lenyewe.
Je, dalili za retinoblastoma ni zipi?
Dalili zinajumuisha:
Mboni (doa jeusi ambalo lipo katikati ya jicho) ambayo ni nyeupe badala ya kuwa nyeusi
Macho yanayopishana kwa kutazama pande tofauti (makengeza, pia huitwa macho yaliyopishana)
Iwapo retinoblastoma ni kubwa, matatizo ya kuona
Iwapo saratani itasambaa, watoto wanaweza kutapika, kupoteza hamu ya kula, au kupata maumivu ya kichwa.
Je, madaktari wanawezaje kujua kama mtoto wangu ana retinoblastoma?
Ikiwa daktari atashuku kuwa mtoto wako ana retinoblastoma:
Atafanya uchunguzi maalumu wa macho wakati mtoto wako akiwa amesinzia kutokana na unusukaputi
Ultrasound, CT (tomografia ya kompyuta), au MRI (upigaji picha kwa mfumo wa sumaku) ili kuona retina
Ikiwa mtoto wako ana retinoblastoma, madaktari watafanya vipimo zaidi ili kuona kama saratani imesambaa, ikiwa ni pamoja na:
Kuchunguza mifupa
Kuchukua sampuli ya uboho (kukata kipande cha uboho) ili kuchunguza saratani
Wakati mwingine, kinga majimaji ya uti wa mgongo
Pia madaktari watafanya upimaji wa jenetiki ili kuona kama retinoblastoma ya mtoto wako ni ile aina ambayo inaweza kurithishwa kwa watu wengine katika familia. Kama ndio yenyewe, madaktari pia watapima wanafamilia wa familia ya mtoto. Kaka na dada walio kwenye hatari ya kupata retinoblastoma wanapaswa kufanyiwa vipimo vya maho kila baada ya miezi 4 toka kuzaliwa hadi umri wa miaka 4. Wazazi pia wanapaswa kuchunguzwa, kwa sababu jeni hizo hizo zinaweza kusababisha uvimbe usiokuwa wa saratani katika retina ya mtu mzima.
Je, madaktari hutibu vipi retinoblastoma,?
Matibabu yanategemea eneo ilipo retinoblastoma na kama imesambaa. Ni muhimu kuondoa uvimbe wote, lakini kama inawezekana, madaktari hutumia matibabu ambayo hayaharibu uwezo wa kuona.
Ikiwa retinoblastoma iko katika jicho moja, kwa kawaida madaktari:
Huondoa jicho
Ikiwa retinoblastoma iko katika macho yote mawili, madaktari wanaweza kuona jicho lenye uvimbe mkubwa zaidi na kujaribu kutibu lile lililobaki pasipo kuliondoa ili mtoto wako aweze kuendelea kuona. Matibabu hayo yanaweza kutumia:
Dawa za tibakemikali yanayoingizwa moja kwa moja kupitia ateri kuu ambayo hupeleka damu kwenye jicho
Matibabu kwa baridi/tiba ya baridi
Tiba ya leza
Vipande vya dutu zenye mionzi huwekwa karibu na uvimbe (tiba ya mionzi ya ndani)
Baada ya matibabu, wataalam wanapaswa kumchunguza mtoto wako kila amra ili kuhakikisha kuwa saratani haikurejea.