Nyenzo za Mada
Je, makengeza ni nini?
Makengeza ni hali ya kuwa na jicho moja linalotazama uelekekeo wa tofauti na jicho jingine. Jicho linaweza kuelekea nje (huitwa walleye) au kuelekea ndani (huitwa macho yanayopishana).
Makengeza yanaweza kuanza mwezi mmoja baada ya mtoto kuzaliwa au kuanza wakati wowote utotoni mwake
Kwa kawaida makengeza husababisha uoni hafifu kwenye jicho moja au utofauti katika uvutaji wa misuli ya macho
Mtoto wako anaweza kuwa anaona vitu mara mbili au shingo lililovimba kutokana na kupinda shingo ili aweze kuona vizuri zaidi
Wakati mwingine makengeze hupata ahueni yenyewe, lakini watoto wengi wanahitaji miwani maalumu ya macho, au lenzi za kupachika, au upasuaji
Pasipo matibabu, makengeza makali yanaweza kusababisha kupoteza uwezo wa kuona moja kwa moja
Je, makengeza husababishwa na nini?
makengeza husababishwa na:
Uoni hafifu (kuona vizuri vitu vya mbali kuliko vya karibu)
Utofauti katika uvutaji wa misuli ambayo hudhibiti mahali ambapo macho yanaangalia, hivyo kusababisha macho yatazame katika uelekeo tofauti
Kupooza au udhaifu wa neva ambayo hudhibiti mwendo wa jicho
Hitilafu ya macho ya kuzaliwa nayo
Kwa nadra sana makengeza husababishwa na aina ya saratani ya macho ambayo huwapata sana watoto wadogo (retinoblastoma) au jeraha la jicho.
Watoto wana hatari kubwa ya kupata makengeza ikiwa:
Walizaliwa mapema sana (kabla ya wakati wao)
Kuna watu katika familia wenye makengeza
Wana magonjwa fulani ya kurithi kama ugonjwa wa Down
Mama zao walitumia dawa au pombe haramu wakati wakiwa wajawazito
Dalili za makengeza ni zipi?
DKT P. MARAZZI/MAKTABA YA PICHA ZA KISAYANSI
Unaweza kupata dalili za:
Mtoto wako anachezesha jicho kila mara au anafunika jicho moja
Macho ya mtoto wako yanaonekana kama hayalengi sehemu moja
Mtoto wako analalamika juu ya macho kukaza, shingo kukaza, au kuona vitu mara mbili
Kwa sababu ishara za uonaji kutoka kwenye macho yako mawili hazilingani, ubongo wa mtoto wako unaanza kupuuzia ishara zinazotoka katika jicho lililoathirika. Hii husababisha aina hali fulani ya kupoteza uwezo wa kuona inayoitwa amblyopia. Ikiwa makengeza ya mtoto wako hayatarekebishwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 8, upotevu wa uwezo wa kuona unaweza kuwa wa kudumu.
Madaktari wanawezaje kujua kama mtoto wangu ana makengeza?
Watoto wanapaswa kuchunguzwa macho yao kila mara ili kukagua kama wana matatizo ya kuona au makengeza, kuanzia miezi kadhaa toka walipozaliwa. Madaktari watachunguza uwezo wa kuona kwa macho wa mtoto wako na kuona ikiwa macho yote yanatazama na kuhama kwenye mwelekeo mmoja.
Ikiwa makengeza yamesababishwa na neva dhaifu au zilizopooza, madaktari wanaweza kufanya uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) au MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ya ubongo na uti wa mgongo.
Je, madaktari hutibu vipi makengeza?
Ikiwa mtoto wako ana makengeza, daktari wa macho (mtaalamu wa macho) anaweza kuamua ni matibabu gani ambayo yanatakiwa. Makengeza kiasi au ambayo hutokea na kupotea yanaweza yasihitaji matibabu. Matibabu hulenga kulinganisha macho ili yaweza kutazama upande ule ule na kuona vizuri kwa usawa. Kutegemea na chanzo na dalili za makengeza ya mtoto wako, madaktari wanaweza:
Kushauri kutumia miwani ya macho au lenzi za kupachika
Kumfanya mtoto afanye mazoezi ya macho
Wakati mwingine, kufanya upasuaji ili kulegeza au kukaza misuli ya macho ili macho yaweze kulingana
Ni muhimu kutibu makengeza kwa sababu yanaweza kusababisha amblyopia (macho tetevu).